Maji Ya Baraka/Uzima - (Mke Wangu Niamini Tu)

Mwenyeminazi

Senior Member
May 24, 2012
195
195
Wadau poleni na majukumu na niwatakie weekend njema hasa hii weekend ya mwisho ya mwaka wa 2013.
Si kusudio langu kuwachosha kwa hili langu zito ingawa si zito kuliko mengine ila naomba tupeane ushauri kama ilivyo ada ya hapa nyumbani JF.
Nimeoa na ni miaka mingi sana imepita tukiwa na mke wangu kwa maisha ya furaha kabisa. Miaka kama minne hivi nilimuachisha kazi mke wangu ili asimamie miradi yetu ambayo si haba inafanya vizuri na namshukuru mwanandani wangu kukubali hili.
Mwaka jana katikati nilipandishwa cheo ofisini na kazi imekuwa inaniweka mbali na familia kwakuwa nasafiri sana ndani na nje ya nchi. sometimes huwa inachukuwa hadi miezi 3 siko home. Kikawaida huwa siwezi kaa week hata 1 bila kucheza mechi na mke wangu na analijuwa hilo maana nikiwa nae napiga mechi pale Stamford Bridge hadi anasema hawezi tena na mimi kuiomba huwa nilikuwa namuambia siwezi kaa zaidi ya week 1 bila kazi ya nguvu.
Sasa siku hizi safari zimezidi na mwezi huu niliingia home na kumkuta bibie hayuko sawa na nilipomuuliza kulikono akasema "ahh sijielewi elewi tu mpenzi" nikajua style zao tu hizi za kutaka kukuambia kitu cha ndani.

Usiku ulipowadia kama kawa tukapasha misuli moto na ilipokuwa tayari kwa mechi kuanza huku refa akihesabu kama wachezaji wote wametimia na wako tayari kuanza mechi si mke wangu akaenda chumba cha kubadilishia nguo.

Alipokuwa anarudi karudi na kichupa kina kimiminika nikastuka yelewiiiii mke wangu wameniharibia tayari!!!!!!. Chupa ya nini tena nikidhani ni yale mafuta ya kupaka misuli ili isife ganzi ili ukipiga penalty gloves za kipa zisiweze kudaka na kuzuia goli. Akaniambia mme wangu we nakujua huwezi kaa week hata 1 bila kucheza mechi ngumu sasa niambie umeweza kweli kukaa miezi yote 3 bila mchezo hata wa kirafiki? Nikamuambia ndio siwezi bila wewe lakini nikiwa mbali nawe naweza.

Akasema sasa nakupaka Maji ya uzima/Baraka MGUUNI ili hapa tusiumizane kama ulichezamechi nje ya uwanja wa nyumbani basi ushindwe kucheza leo. Nikabisha akaanza kulia na kuniambia basi utakuwa umefanya. Kwa kumridhisha nikakubali anipake na mchezo uendelee bila longtime delay. Sasa siku hizi imekuwa ndio Tabia kila nikitoka safari.

Hii tabia inaniuzi jamanaiiii. Nimfanyaje huyu laazizi wangu mi naona kama tunachezea maji ya uzima Kwa vile yakipungua tanaenda kanisani kuchukuwa. Huu ujinga atakuwa kautoa wapi? Naombeni ushauri ndugu zangu na haya Maji Ya Baraka ninayopwakwa MGUUNI.
 
byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
909
500
dah...noma sanaaa..ila ataungekuwa wewe lazima uwe na mashaka kama huwez kupitisha wiki sembuse miezi mitatu..ila pia maji ya balaka sio ishu kabisa mapadri wanajitaidi kubalik kumbe nanyinyi manayatumia kubaliki viungo dah..kama bado hanaimani nawewe mwambie atafute njia nyengine ya kufanya sio hiyo....
 
sungura1980

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,910
1,195
Hahahaaaa,pole kaka,na wewe muapishe kwa kumwagia maji hayo hayo,tena kwa sababu wao hata kama hajisikii mtafanya tu,basi muapishe kuwa kama ametoka nje ya ndoa basi akimwagiwa hayo maji awe kipofu!Next week rudi hapa utupe mrejesho!Anajihami huyo inawezekana yeye ndo anatoka anataka kujionyesha mwaminifu!
 
Mwenyeminazi

Senior Member
May 24, 2012
195
195
Hahahaaaa,pole kaka,na wewe muapishe kwa kumwagia maji hayo hayo,tena kwa sababu wao hata kama hajisikii mtafanya tu,basi muapishe kuwa kama ametoka nje ya ndoa basi akimwagiwa hayo maji awe kipofu!Next week rudi hapa utupe mrejesho!Anajihami huyo inawezekana yeye ndo anatoka anataka kujionyesha mwaminifu!
Ahsante mkuu. Duh sasa naanza pata mawazo mengine tena!!!! Anamegwa????
 
sungura1980

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,910
1,195
Ahsante mkuu. Duh sasa naanza pata mawazo mengine tena!!!! Anamegwa????

Huko sasa mkuu usiwe na mawazo hayo asilimia mia moja,wewe siku akikuletea maji hayo kama kawa kubali,then sema,''Ee Mungu kwa maji haya ya baraka mke wangu kama amenisaliti nikimwagia miguuni basi awe kipofu",utamuona tu atakavyobabaika,akikataa husimulazimishe,hayo maji ni ya baraka kweli atakuwa kipofu!
 
Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,200
2,000
maji ya baraka hayana shida wasiwasi anakulinda na kupitiwa na shetani vizuri wakati anakupaka nawe fanya hivyo ikiwezekana muyanywe wote
 
Mwenyeminazi

Senior Member
May 24, 2012
195
195
dah...noma sanaaa..ila ataungekuwa wewe lazima uwe na mashaka kama huwez kupitisha wiki sembuse miezi mitatu..ila pia maji ya balaka sio ishu kabisa mapadri wanajitaidi kubalik kumbe nanyinyi manayatumia kubaliki viungo dah..kama bado hanaimani nawewe mwambie atafute njia nyengine ya kufanya sio hiyo....
Ahsante mkuu nitamuambia atafute njia mbadala hii inaniharibia mood maana huwa nashikwa na hasiraa
 
Mwenyeminazi

Senior Member
May 24, 2012
195
195
Huko sasa mkuu usiwe na mawazo hayo asilimia mia moja,wewe siku akikuletea maji hayo kama kawa kubali,then sema,''Ee Mungu kwa maji haya ya baraka mke wangu kama amenisaliti nikimwagia miguuni basi awe kipofu",utamuona tu atakavyobabaika,akikataa husimulazimishe,hayo maji ni ya baraka kweli atakuwa kipofu!
Kwa imani niliyonayo!!! suppose anakuwa kipofu kwa maombi yangu si mtanikimbia hapa JF kwa usumbufu
 
Mwenyeminazi

Senior Member
May 24, 2012
195
195
nakupongeza kwa kutumia tafsida, umestaarabika ndugu

Ahsante kaka mkubwa. Huku kuna watoto wengi bwana siku hizi. Isije kuwa watoto wetu tunawaharibu wenyewe kisha tunasingizia Utandawazi na hali ya kuwa sisi ndio tunawatandazua
 
Lusa Nise

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
306
250
Pia chunguza kama ameanza kwenda kusali haya makanisa ya `kiokovu`, huko pia wanaribiwa sana kwa kuaminishwa vitu visivyokuwa na maana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom