Huyu jamaa mimi simuelewi ukiangalia hiyo picha kwa makini unaona kabisa anachosema si kweli, kama alikuwa na Vincent iweje aonekane anamuangalia Nassari! na anasema Nassari alikuwa anaamlisha vijana wa Chadema wamchome moto, kwa mazingira ya kawaida mtu anayetishiwa kuchomwa moto angekuwa na sura ya kutishika maana usalama wake ungekuwa hatarini lakini tofauti na yeye anavyoonekana kwenye picha akiwa na furaha sana,ina maana alikuwa anafurahia tishio hilo! haya ndio matatizo ya waganga wa kienyeji kuwa wana siasa!mbona sasa hatishii kulishitaki na Tanzania Daima maana nalo lilipandika picha hiyo!