Sisi Wananchi tunaoishi hapa Mbagala Sabasaba tunapata changamoto ya mazingira kuchafuliwa na kuwa hatari kwa afya kutoka katika Machinjio ya Ng’ombe ambayo yapo kwenye makazi ya Watu.
Maji machafu ambayo yanatoka kwenye machinjio hayo tanatiririka kwenye makazi yetu na hakuna jitihada zinazofanywa na mamlaka kudhibiti hali hii.
Wakati huu wa mvua ndio balaa kabisa, uchafu unasambaa, Watoto wanachezea na kinachotokea ni kuwa tunaweza kuona magonjwa ambukizi yakiibuka.