Maji hupunguza msongo wa mawazo

Doncy monco

Member
Jul 26, 2019
38
101
Unywaji maji kwa wingi unasaidia kuimarisha afya ya ngozi na kuifanya ing’ae, iwe laini na yenye muonekano wa kuvutia zaidi. Zipo faida nyingi zilizozijificha za kunywa maji mengi, kupunguza msongo wa mawazo na hasira ni miongoni.

Kama unahitaji njia rahisi na ya asili ya kuepukana na maisha yenye hasira, au yaliyojaa msongo wa mawazo basi jenga utamaduni wa kunywa maji mengi. Ogani nyingi za mwili ukiwamo ubongo, zinahitaji maji ili kufanya kazi kwa ufasaha.

Hivyo, kukosa kiwango stahiki cha maji kinaathiri afya ya ubongo moja kwa moja na kusababisha msongo wa mawazo. Utafiti mbalimbali wa afya uliowahi kufanywa unathibitisha kuwa ukosefu wa nusu lita ya maji kwa siku, kunasisimua na kupandisha kiwango cha homoni inayoratibu mapokeo ya hasira na msongo wa mawazo mwilini.

Homoni hii ambayo kitaalamu inaitwa cortisol humfanya aliyekosa maji hayo kuwa na msongo au sonona, tofauti na mwenye kiwango cha kutosha cha maji mwilini.

Hii haina maana kuwa, kunywa kiwango kikubwa cha maji mfululizo kwa muda wa siku nzima kutaondoa changamoto nyinginezo za kila siku za maisha kama za fedha au familia.
 
Back
Top Bottom