Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,315
- 33,109
Kolesteroli na namna iwezavyo kudhibitiwa bila dawa
MAJI HUKINGA NA KUPONYA KOLESTEROLI:
Kwa kusikia tu sentensi Una kolesteroli iliyozidi toka kwa daktari kunaweza kumfanya mtu yeyote kuingiwa na hofu. Hata hivyo, linapokuja suala la kuishi, kila mmoja angependa kuishi maisha marefu na yenye furaha na hivyo kolesteroli inaweza kuwa kizingiti kwa hilo.
Kolesteroli au helemu ni nini? Ni dhahiri na rahisi kabisa, ni kama nta laini ambayo huelea katika damu na katika seli zako zote za mwili. Kwa baadhi ya watu kolesteroli ina mwelekeo wa kujilundika kwenye ateri karibu na moyo au shingoni. Ikiwa mkusanyiko huu wa kolesteroli unaendelea kuwa mwingi kiasi cha kuanza kuzifunga ateri, huweza kusababisha mishtuko au shambulio la moyo (heart attack).
Ukweli ni kuwa kolesteroli si mojawapo ya vitu ambavyo watu hupenda kukichunguza. Isitoshe mwili unaitengeneza kila siku ili kwamba unaweza kufurahi kuwa mzima. Ubongo umetengenezwa kwa kolesteroli, homoni zako zimetengenezwa kwa kolesteroli na hata neva zako zimefunikwa na kolesteroli (myelin sheaths). Bila kolesteroli huwezi kuishi.
Ikiwa kolesteroli ni kitu kibaya sana, kwanini Ini lako huizarisha kwa wingi kiasi hicho
Asilimia 75 ya kolesteroli katika damu hutengenezwa na Ini. Asilimia nyingine 25 hutujia toka kwa kile tunachokula. Kadiri ulavyo kolesteroli nyingi, ndivyo na Ini huitengeneza chache ili kukuweka wa furaha. Ini lako linatengeneza wastani wa mg 900 kwa siku. Kwa wastani, watu hula mpaka mg 300 za kolesteroli kwa siku. Ukichanganya pamoja, mtu wa kawaida ana mg 1200 za kolesteroli katika mfumo wake wakati wowote.
Kwanini katika maisha Ini letu litakuwa linatengeneza mg 900 za kolesteroli kila siku huku tunaambiwa chochote zaidi ya mg 200 ni hatari?, tunaweza kusema tu haileti maana.
Unapokula chakula chochote chenye kolesteroli, kolesteroli lazima iende kwanza katika kuta za tumbo kwa ajili ya kuingia kwenye mkondo wa damu. Cha kushangaza ni kuwa tumbo (intestine) lina uwezo mdogo sana wa kumengenya kolesteroli unayokula. Katika hali hii mwili wako ndio hasa hukulinda usipate kolesteroli nyingi kupitia chakula ulacho. Ikiwa itatokea umekula chakula ambacho kina kolesteroli nyingi, sehemu kubwa ya kolesteroli itatoka nje wakati unapata choo.
Hautapata ishara yeyote ya onyo kwamba una kolesteroli iliyozidi. Namna moja ya kutambua kwa hakika ni kufanya kipimo kiitwacho lipoprotein profile . kipimo hiki kitaonesha jumla ya kolesteroli uliyonayo, HDL cholesterol, LDL cholesterol na usawa wa triglyceride. Kipimo hufanyika baada ya kufunga masaa tisa mpaka kumi na mbili bila chakula, kimiminika au dawa.
Katika miaka ya 1970 kiasi kilichokuwa kinakubalika kama cha kawaida cha kolesteroli mwilini kwa mtu chini ya miaka 30 kilikuwa 120 mpaka 290 huku ikikubalika 150 mpaka 340 kwa mtu wa miaka zaidi ya 40.
Kwa mjibu wa viwango vinavyokubalika sasa, ikiwa majibu ya kipimo cha lipoprotein (protini inapochanganyana na mafuta) profile yanaangukia katika usawa ufuatao, utachukuliwa kama huna tatizo na hutakiwi kuwa na wasiwasi juu ya hilo:
· Jumla ya kolesteroli: chini ya 200 mg/dl
· Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesteroli: zaidi ya 40 mg/dl
· Msongamano wa chini wa lipoprotini kolesteroli: kati ya 100-129 mg/dl
· Triglycerides: chini ya 150 mg/dl
Umeona tofauti kubwa ya kiasi cha kolesteroli iliyokuwa inakubalika 1970 na ile inayokubalika siku hizi?. Kwanini kiasi hiki kilipunguzwa? Ni watu milioni ngapi zaidi wanatumia dawa za kupungunguza/kudhibiti kolesteroli siku hizi kwa sababu kiasi kilichokuwa kinakubalika kilipunguzwa na kwa gharama gani?.
Kwa mjibu wa William Campbell Douglass, M.D., ambaye amekuwa akitibu watu wenye kolesteroli duniani kote kwa zaidi ya miaka arobaini sasa, ikiwa jumla ya kolesteroli yako ni kati ya 200 na 300 na unatumia chakula safi chenye wanga mchache, usijisumbuwe kuwaza kuhusu kolesteroli.
Edward R. Pinckney, M.D. katika kitabu chake The Cholesterol Controversy anatuambia kwamba watu waliolazimishwa kupunguza kiasi chao cha kolesteroli kwa sababu wameonekana kuwa na shambulio la moyo walijikuta wakitokewa kupatwa na shambulio jingine la moyo kuliko wale walioendelea kula kawaida bila kuzidisha.
Je kutoa damu kunaweza kusababisha kiasi chako cha kolesteroli kupanda ju?
Amini usiamini, kwa baadhi ya watu, wazo tu la kutoa damu linaweza pelekea kolesteroli zao kupanda juu mpaka 400 hata kama hawana tatizo na kolesteroli kwa ujumla.
Tuchukulie mfano umefadhaishwa kiasi kidogo tu kwa kupimwa kiasi cha kolesteroli labda kwa sababu ya kushikiwa tu sindano juu ya mkono wako kunakuudhi au kwa sababu tayari unahofu kupima kiasi cha kolesteroli ulichonacho kinachoelea katika mkondo wako wa damu kunaweza kumaanisha una ugonjwa wa moyo hivyo majibu ya kiasi cha kolesteroli yatakayopatikana ukiwa katika hali hii yanaweza kuwa si ya kweli kwa karibu ya asilimia 100.
Wakati unaweza kuwa tu na kolesteroli ya kiasi cha 180 mg ambacho kinachukuliwa kuwa ni cha kawaida, hofu, wasiwasi au woga vyaweza pelekea kupanda kwa kiasi cha kolesteroli na majibu ya maabara yanaweza kutoka na 360 mg kiasi kinachotosha kukufanya wewe (pengine hata daktari wako) kuanza mzunguko usioisha (vicious cycle) kutibu ugonjwa wa moyo kwa madawa.
tangu 1936, utafiti baada ya utafiti umeonesha
hakuna uhusiano kati ya kolesteroli na ugonjwa wa moyo.
Utafiti wa kwanza kuhusu kolesteroli na ujikusanyikaji wake katika ateri (atherosclerosis) umewahi kuchapishwa 1936. majibu ya mwisho yalionesha kuwa hakukuwa na uhusiano kabisa kati ya kiasi cha kolesteroli katika damu na dipositi za kolesteroli katika ateri.
Utafiti mwingine mwaka 1963 ukihusisha askari wastaafu 800 (wa marekani) juu ya miaka 60, ulionesha kwamba ateri za waliokuwa na kolesteroli chache hazikuwa na tofauti na za wale wenye kolesteroli kuzidi.
Dr. Michael DeBakey mtaalamu maarufu mmarekani katika masuala ya upasuaji wa moyo na timu yake ya utafiti walitafiti waathirika 1700 wenye ateri zilizozibika au kukazika (arteriosclerosis). Nane kati ya kumi ya waathirika hawa walikutwa na kolesteroli ya kawaida inayokubalika kwa wamarekani.
Dr. William P. Catelli, mkurugenzi wa utafiti maarufu wa Framingham study, ambaye ametafiti sababu zote zinazoweza pelekea ateri kuzibika au kukazika na ugonjwa wa moyo, alitamka katika historia 1992 kwamba....
.ndani ya Framingham, wengi wa watu, kadiri walivyokula mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fat) ndivyo walivyopata kolesteroli nyingi, na ndivyo watu hao walipata kuwa na kalori/nishati nyingi, na ndivyo watu hao walivyokutwa na damu chache yenye kolesteroli
Tulipata kujuwa kuwa watu waliokuwa wakila vyakula vyenye kolesteroli nyingi, walikula kolesteroli itokanayo na wanyama (saturated fat), walikutwa na kalori nyingi, uzito wa wastani na walikuwa na miili yenye nguvu (physically active.)
Kunywa Maji Mengi kwa afya yako.