Maji hadi mvua ianze kunyesha-SOUWASA SONGEA

Maji hadi mvua ianze kunyesha-SOUWASA SONGEA

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
413
Reaction score
90
TANGAZO KWA WANANCHI WOTE
Sasa yapata miezi miwili kamili wakazi wa Songea wakosa maji rasmi.
Kwa masikitiko makubwa,nawajulisha wananchi wote hasa wanaokuja SONGEA kwa shughuli maalumu kutembea na majaba ya maji kwani huku maji hayatapatika hadi hapo mvua zitakapoanza kunyesha.Jambo hili limethibitishwa na idara ya maji baada ya wateja wengi kwenda kuuliza ofisini hapo.
Aidha tunawapongeza waliompa kura Nchimbi kwani haya ndio malipo ya kura zao.
CHANGAMOTO KWA CCM
Je,hakuna njia yoyote ya kuvuna maji kifuku ili yatufae wanyonge nyakati kama hizi?
ARI MPYA,NGUVU MPYA,KASI MPYA=ANGUKA.
Mbunge wa wanyonge-SONGEA.
 
Ngojea chadema wakishaka dola watawajengea mabomba ya maji na visima kila mtu katika nyumba yake.
 
leo nimeamka saa kumi na nusu usiku kwenda kuchota maji nikakuta foleni. Hawa ccm hawafai kabisa hasa nchimbi
 
Ha,ha,ha,ha,ha,ha nimecheka kweli hv hao souwasa wako serious?,hayo majibu waliyowapa wananchi naona aliyetoa alikuwa na hangover,yani kweli huduma muhmu kama maji mnawaambia wananchi wasubiri mvua?,sasa mvua isiponyesha inakuwaje?,kweli ni hatari!
 
Nchi hii mkoa ukishakuwa mbali na dar es salaam tu ni majanga kuishi
 
TANGAZO KWA WANANCHI WOTE
Sasa yapata miezi miwili kamili wakazi wa Songea wakosa maji rasmi.
Kwa masikitiko makubwa,nawajulisha wananchi wote hasa wanaokuja SONGEA kwa shughuli maalumu kutembea na majaba ya maji kwani huku maji hayatapatika hadi hapo mvua zitakapoanza kunyesha.Jambo hili limethibitishwa na idara ya maji baada ya wateja wengi kwenda kuuliza ofisini hapo.
Aidha tunawapongeza waliompa kura Nchimbi kwani haya ndio malipo ya kura zao.
CHANGAMOTO KWA CCM
Je,hakuna njia yoyote ya kuvuna maji kifuku ili yatufae wanyonge nyakati kama hizi?
ARI MPYA,NGUVU MPYA,KASI MPYA=ANGUKA.
Mbunge wa wanyonge-SONGEA.
Tuache ushabiki wa siasa katika mambo muhimu kama huduma ya maji. Ni kweli kuna tatizo la maji lakini sidhani kama jibu alililosema limetoka katika ofisi za idara ya maji (SOUWASA). Moja ya maeneo ya miji ya Tanzania ambako huduma ya maji hupatikana kwa wakati wote isipokuwa mwezi mmoja au miwili ambapo huduma hutolewa kwa mgawo ni Songea. Kama mtoa mada ni mkazi wa Songea atakumbuka jinsi kulivyokuwa na tatizo la maji miaka ya tisini na mwanzoni wa 2000s. Serikali ya Tanzania pamoja na serikali ya Ujerumani waliwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya Majisafi n majitaka na kuondoa kabisa tatizo la maji. Kumbuka miji yetu inakua kwa kasi kutokana na kasi ya maendeleo yanayofanywa na serikali katika sekta ya barabara, madini n.k. na hivyo kuna changamoto ya utoaji wa huduma za jamii kama maji. Hivyo kuna mgawo wa maji na sio kukosa kabisa, hii sio ngeni kwa wakazi wa DSM hasa eneo la Kimara ambako kuna matanki ya kuhifadhia maji yanayotoka Mlandizi (Ruvu Juu). Tembelea Mamlaka ya maji Songea ujifunze jinsi inavyokabiliana na changamoto hizo kwa juhudi zake yenyewe pamoja na Serikali. Huo ndio uwazi na ukweli acha propaganda za zisizo na mashiko.
 
Magamba wameshachafua hali ya hewa.Wewe ni mkazi wa Songea?Mada inasema wakosa maji rasmi.Wewe unasema mgao.Mmma!Labda mada hujaielewa.Hivi unadhani Nchemba oh Nchimbi tangu apate ubunge kuna maendeleo yoyote kayafanya zaidi ya kumiliki mabasi ya SUPERFEO?Mahali popote penye mbunge wa ccm HAKUNA maendeleo!Angalia jirani zenu TUNDURU kama wana ubavu wa kusafiri kwenda songea kifuku na kufika siku hiyohiyo.Kweli kuitetea ccm ni sawa na kutafuna kaa la moto ukidhani jojo!
 
Back
Top Bottom