Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,600
- 217,997
Taarifa kutoka kwa wakazi hao zinasema kwamba kabla ya mfereji huo usiotumika, makazi yao hayakuwahi kukumbwa na mafuriko makubwa kama yale yaliyotokea hivi Majuzi baada ya mvua kubwa kunyesha, hasa baada ya kuzibwa kwa mifereji ya awali huku mfereji huo mpya ukifungwa bila kutumika licha ya kwamba umejengwa, Maandamano hayo yamepangwa kufanyika kesho.
Baada ya tuhuma hizo tukaamua kufuatilia ambapo tumejiridhisha kwamba ni kweli njia ya maji kuelekea baharini Eneo la BP au PUMA imechukuliwa na mfereji huo uliozibwa ambao haufahamiki utakamilika lini, huku msimu wa mvua ukikaribia, juhudi za kumtafuta injinia wa Manispaa ya Temeke zinaendelea huku kukiwa na tuhuma nzito dhidi yake ya kuwasaidia wakandarasi wa kichina kukwepa ramani ya awali ya mradi huo iliyokuwa kwenye Barabara ya kwenda Uwanja wa Taifa kutokea Tameko ili kuepuka gharama na kuanza kuuchepusha kwenye makazi ya watu, jambo linalopingwa na wananchi.
Taarifa zote za mradi huu ambao umeleta usumbufu mkubwa kwa wananchi ikiwemo kubomoka kwa nyumba zao mvua zinaponyesha pamoja na kusababisha vifo kadhaa vya watu huku taarifa zikifichwa tutazileta hapahapa JF, sasa tumeamua kulivalia njuga jambo ili kuepusha mafuriko ya kijinga.
Itaendelea...