Majeshi yetu yafunzwe kuheshimu raia

Nyagahinga

Member
Nov 11, 2010
7
1
Leo asubuhi around saa 3 pale traffic lights Magomeni nimeona askari magareza wakimpa kipigo cha mbwa mwizi dreva wa fuso kisa eti amekaa kupisha gari la wafungwa.

Sisi wapita njia tumesikitishwa sana na kitendo hiki kwa kuwa hakukuwa na ulazima wa kumpiga kiasi hiki kwa sababu hakuwa mbishi na tumeona jinsi busara za askari wengi wa majeshi yetu zilivyo finyu.

Ingekuwa vyema wafundishwe kuheshimu utu wa mwanadamu kwa sababu itafika wakati wananchi watachoka kuonewa na hizo bunduki zao wataziona kama fimbo tu na mifano tunaiona katika nchi za wenzetu.
 
Ndugu ukiwasema sana hao jamaa kuwa akili zao zimezunguka kama kofia zao zilivyo na hazina ncha ya kufikiri zaidi ya wanayoagizwa kufanya utaambiwa unahatarisha amani. Muulize kibanda kwa maelezo zaidi.
 
wanajiona wapo juu ya sheria, nafikiri pia ni uelewa mdogo wa yule dreva Fuso angetakiwa kwenda police kufungua kesi ya kudhalilishwa barabarani. Kuwa police si kigezo cha kuwa juu ya sheria za nchi. barabara zenyewe nyembamba kwa hiyo nipeleke gari kwenye mtaro kisa eti kupisha gari la mageleza - huo ni ukenge.

Wananchi pia tuamuke tujue haki zetu - askari yeyote hana mamlaka ya kumpiga raia - nilo ni kosa kubwa mno alitakiwa huyo askari magereza ariporti kwa traffic ili yule dereva kama ana makosa afunguliwe mashitaka na si vinginevyo.
 
Sometimes level of education talks. Kama level yao ni ndogo then hata thinking capacity will be very poor au?
 
Sijui hawa wanajeshi wana akili gani, kazi yao ni kunyanyasa wanachi na hakuna anae wakemea, hawana ustaarabu hata kidogo. Jambo dogo tu wameshatoa kichapo, mnawanyanyasa hawa wananchi hamjui wao ndio wanawalipa mishahara. hawa jamaa hawana kazi, wapeni kazi ya kuchimba mitaro kujenga barabara kulinda mbuga za wanyama, kulinda madini, wakiwa busy hawatafanya huu upuuzi.
 
tatizo la maafande wengi wa hii nchi ni kujichukulia maamuzi mikononi maana wanajua wao hakuna mtu atakayewauliza,
huu ni upumbavu,na viongozi wao wapo hawawajibishi,ingekuwa ni nchi nyingine,wanajeshi/polisi kamwe hawawezi kuleta usumbufu kwa raia,ila hapa tz ni kinyume
pia nadhani sometimes they are on drug au wanakuwa wamevuta bangi,
inabidi siku afande akijichanganya nikumpa kipondo cha heshima ili nao wajue raia tupo vyema
 
Mkuu kwa ufupi majeshi yetu ni ya kikoloni zaidi, ni kama enzi zile za mwingereza!
 
Back
Top Bottom