Majeruhi maandamano Arusha wadai wana risasi mwilini

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173

Majeruhi maandamano Arusha wadai wana risasi mwilini

Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 8th January 2011 @ 23:30


BAADHI ya majeruhi waliojeruhiwa wakati wa vurugu zilizotokea katika Mkutano wa Chadema, baada ya polisi kuwasambaratisha kwa risasi na mabomu, wameomba Serikali kuwasaidia haraka kwa kuondoa risasi zilizo katika miili yao, ambazo bado hazijaondolewa.

Wakizungumza katika wadi ya majeruhi ya Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, mmoja wa majeruhi wa risasi, Frank Joseph aliyejeruhiwa kiunoni, alisema kuwa tangu walazwe, hawajapata huduma ya kuondolewa risasi na hawajui mustakabali wao wa maisha.

Tunaomba Serikali iweze kuingilia jambo hili, kwani sisi wengine tulikuwa tunaendelea na shughuli zetu, lakini wametutwanga risasi,” alidai Frank.

Naye Richard Mtui, yeye alisema kuwa amepigwa risasi na polisi, sehemu za mbavuni, hivyo hadi kufikia jana alikuwa hajatolewa risasi hizo na hajui kinachoendelea juu ya kutolewa risasi hizo.

“Sasa nazidi kupata mashaka, je hizi risasi si zitaondoa maisha yangu, kwa sababu bado ziko mwilini na nazidi kuumia, naomba Serikali itusaidie katika hili,” alisema Mtui.

Akizungumzia suala hilo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Seleshi Toure alisema kuwa wagonjwa hao, mara baada ya kufikishwa kwenye Hospitali ya Mkoa Mount Meru, walipatiwa huduma kwa haraka.

“Huduma tulizowapatia ni kuwapiga picha ya X-Ray, kuwatundikia dripu, kuwaosha vidonda, na kuwapa dawa ya kutuliza maumivu makali waliyokuwa nayo,” alisema Dk. Toure.

Alisema kuwa, baada ya kuwapatia huduma hizo, kwa upande wa risasi alikiri kuwa bado kazi ya kuziondoa miilini mwao haijaanza na kusisitiza kuwa, siyo kwa makusudi, bali ni kazi inayohitaji umakini wa kitaalamu wa hali ya juu, hadi kufikia maamuzi kuwatolea au la.

“Unajua ndugu Mwandishi, sio wote wanaopigwa risasi, wanaondolewa mwilini, la hasha, bali mpaka tujue tukitoa je haina madhara au la kama kuna madhara basi hatutoi, ili mradi hupotezi maisha na kama kuna madhara mwilini tutatoa,” alisema Dk. Toure na kushauri walioathirika wasiwe na hofu, bali wawaache wataalamu, wafanye kazi zao.
 
Tunaomba Serikali iweze kuingilia jambo hili, kwani sisi wengine tulikuwa tunaendelea na shughuli zetu, lakini wametutwanga risasi," alidai Frank.

Hivi serikali hii kweli itapenda kuziondoa hizo risasi au ingependelea kuona hawa jamaa wanapoteza maisha yao?
 
Du....hatari sana hii!
Poleni sana ndugu zetu, kama mmeandikiwa maisha mtakuwa salama tu...
Tuko pamoja nanyi.
 
Back
Top Bottom