Majengo 22 yaporomoka China

Majengo 22 yaporomoka China

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,286
attachment.php


Majengo 22 yameporomoka katika maeneo ya viwandani katika mji wa Shenzhen, Kusini mwa Uchina kufuatia maporomoko ya ardhi.

Takriban watu 900 waliokolewa kabla ya maporomoko hayo kutokea.

Hata hivyo waokoaji wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanashukiwa kuwa wamekwama ndani ya vifusi vya majengo hayo yaliyoporomoka

Hadi kufikia sasa hakuna mtu aliyeripotiwa kufarika ijapokuwa watu 22 hawajulikani waliko.

Mbili kati ya majumba hayo yalikuwa nyumba za malazi za wafanyikazi wa ujenzi na yamkini watu wanne wametolewa ndani ya vifusi vya majengo yaliyoanguka.

Naibu mwenyekiti wa mji huo Li Yikang, amesema wanawake 5 na wanaume 17 hawajulikani waliko.

Wazima moto 1,500 wanaendelea na shughuli ya uokoaji.

Kulingana na vyombo vya habari mchanga ambao umekuwa ukichimbwa kwa muda wa miaka miwili unaaminika kuwa ulilowa na kuporomoka.

Chanzo: BBC
 

Attachments

  • 151220065446_cn_guangming_collapse_01_624x351_shenzhenmunicipalpublicsecurityfirebrigade_nocredi.jpg
    151220065446_cn_guangming_collapse_01_624x351_shenzhenmunicipalpublicsecurityfirebrigade_nocredi.jpg
    15.7 KB · Views: 1,918
Hata kwao wanajenga majengo yasiyo na standard??
 
Kwa kuchakachua hao ni balaa kila wakati majumba yanaporomoka tu ukiangalia "poor construction in China" utashangaa rushwa katika ujenzi ilivyokithiri,
2008 nyumba zilijengwa kwenye eneo la tetemeko la ardhi bila kuzingatia masharti na rushwa kutawala nyumba 6.5m zilibomoka
 
Guys msiwe watu wa kuhukumu sana majengo yamemoboka kutokana na maporomoko ya ardhi sasa ukisema ni uzembe au majengo yapo chini ya kiwango sizani kama ni sawa.
You cant stop the mother nature
 
Kwa kuchakachua hao ni balaa kila wakati majumba yanaporomoka tu ukiangalia "poor construction in China" utashangaa rushwa katika ujenzi ilivyokithiri,
2008 nyumba zilijengwa kwenye eneo la tetemeko la ardhi bila kuzingatia masharti na rushwa kutawala nyumba 6.5m zilibomoka


Hiyo idadi ya Nyumba zilizobomoka Ni hatari.
 
Hadi kwao wanajenga yaliyo chini ya kiwango??
 
Back
Top Bottom