Majembe wajipanga kuidai fidia Sumatra

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAKATI Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), ikijipanga kutekeleza agizo la Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu la kuvunja mkataba wake na kampuni ya Majembe Auction Mart, kampuni hiyo ya udalali imesema inafanya tathmini ya hasara itakayopatikana na hatua inazoweza kuchukua kufidia hasara hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Motema Motto alilieleza gazeti hili jana kuwa, suala hilo sasa liko kwa wanasheria wao.

"Mkataba una mambo mengi na ni wakisheria, kwa sasa hatuna la kusema, tunasubiri Desemba 31, Sumatra itekeleze agizo la waziri," alisema Motto.

Hata hivyo, alisema ni dhahiri kuwa kukatishwa ghafla kwa mkataba huo, kutaiathiri kampuni ya Majembe hivyo ili kukabilianana tatizo hilo, kampuni hiyo sasa inafanya tathmini ya hasara na kupata ushauri wa kisheria.

"Agizo la waziri kutaka mkataba huo uvunjwe Desemba 31 mwaka huu, litafanya mkataba huo uvunjwe mwezi mmoja kabla ya kumalizika jambo ambalo kwa vyovyote, litailetea hasara kampuni," alisema Motto.

Motto alisema mbali na mkataba wa Sumatra na Majembe kumalizika Januari 31 mwakani, kampuni hiyo pia ilikuwa kwenye mazungumzo ya kuomba iongezewe mkataba jambo ambalo limeifanya iongeze wafanyakazi zaidi.


Akizungumzia kauli hiyo ya Waziri jana, Afisa Uhusiano Sumatra, David Mzirai alisema hakuna namna isitekelezwe kwani ni agizo halali la waziri mwenye dhamana.


“Linalotuumiza vichwa sasa ni kwamba tumezoea kufanya kazi na Majembe, sasa tunaangalia tutafanya kazi na nani? Ila sio kujadili kilichoongelewa na waziri,”alisema Mzirai.


Mzirai alisisitiza kwamba, kabla ya kuvunja mkataba huo, Sumatra itakaa na Majembe kujadili namna ya kutekeleza agizo hilo ili kuhakikisha hakuna upande unaumizwa na uamuzi huo.

“Hatuwezi kukurupuka lazima tukae na kuangalia ni madhara yapi yatajitokeza baada ya kuvunja mkataba huo. Ingawa hadi sasa sijaona kipengele cha kuleta madhara, ila hatuwezi kuuvunja kiholela,”alisema Mzirai.


Wiki iliyopita Nundu aliipa Sumatra siku saba kusitisha mkataba na Majembe ikiwa ni njia mojawapo ya kuondoa matatizo ya usafirishaji wa abiria.

Nundu alisema kampuni ya Majembe imekuwa ikifanya kazi za usalama barabarani kinyume cha sheria kwa kukagua matairi, kuangalia leseni za barabara, bima, taa za magari na vioo wakati hawana ujuzi wala mamlaka ya kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine, Sumatra imeandaa mikutano ya kukusanya maoni kuhusu mapitio ya nauli za mabasi ya mijini na mikoani itakayofanyika Januari sita na saba mwakani.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Mawasiliano kwa Umma imeeleza kuwa mikutano hiyo itajumuisha wadau wa sekta ya usafirishaji abiria kwa barabara, wamiliki na watumiaji wa huduma za usafiri na wananchi.

Taarifa hiyo ilisema mikutano hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam na katika mikoa mingine ya Tanzania Bara.

Taarifa hiyo ilisema katika mikutano hiyo viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mikoani (Taboa) na |Chama cha Wamiliki wa Daladala (Darcoboa), watawasilisha mapendekezo yao kuhusu viwango vipya vya nauli
 
majembe walizidi kiherehere hadi wakawa kero kwa raia kuliko hata traffic police.acha wapate akili kwanza kwanza ili wajifunze maana walikua wanajiona wanapower kubwa mno barabarani.
 
hawa majembe walikuwa wanyanyasaji tu.

mbwa kabisa hawa wamekula hongo na sumatra soma hapo juu hilo punguani mziray ati tumezoea kufanya na majembe sijui tutafanya nani...hivi ujui na wewe unapiota anakuja mwingine kukalia kili chako..so kama kuna mtu anatoka mwingine ataingia acha ujinga kenge manyoya we mzirwaaaaaaaaayyyyyiiiiiiiii
 
rushwa ya majembe ilikua tsh 50 000 kwenda juu!yaani kwenye daladala kuna stika 7 zote hizo za kumuumiza raia tuu.WAFIE MBALI MAJEMBE
 
mbwa kabisa hawa wamekula hongo na sumatra soma hapo juu hilo punguani mziray ati tumezoea kufanya na majembe sijui tutafanya nani...hivi ujui na wewe unapiota anakuja mwingine kukalia kili chako..so kama kuna mtu anatoka mwingine ataingia acha ujinga kenge manyoya we mzirwaaaaaaaaayyyyyiiiiiiiii

du inaonekana uko na uchungu sana pole sana ndugu yangu twajua ilikuwa ni mradi wa wakubwa
 
safi sana namshukuru waziri kwa maamzi yake majembe ni watu waliokuwa na power ya ajabu utafikili nchi ilikuwa mikononi mwao
 
Pamoja na kwamba walikuwa wanakula rushwa (nani asiyekula nchi hii? Hata Makamba anakula!) walifanya kazi kubwa ya kuwatia adabu watu wa daladala, kukatisha ruti, kutanua tulishaanza kusahau sasa tutarudi kulekule kwenye vurugu za barabarani
 
Back
Top Bottom