Majawabu ya Kigwangalla: Tunawezaje Kuleta Usawa Kwenye Ubora wa Elimu Yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majawabu ya Kigwangalla: Tunawezaje Kuleta Usawa Kwenye Ubora wa Elimu Yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HKigwangalla, Mar 16, 2012.

 1. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  HUU NI MMOJA WA MICHANGO YANGU KWENYE BAJETI YA ELIMU MWAKA JANA WAKATI BUNGE LIMEKAA KAMA KAMATI.
  MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla!


  MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
  ahsante kwa kunipa fursa hii.


  Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishi niliongelea kwa kirefu
  kuhusu jitihada za Serikali katika ku-foster equity kwenye utoaji wa elimu nchini ili kupunguza gap
  kati ya walio nacho na wasio nacho, na pia ili kuondoa uwezekano wa kuunda matabaka ya watumwa
  na watawala kwa kuruhusu uwepo wa kundi la watu wenye elimu bora na la wale wasio na elimu kabisa.
  Hii inatokana na uwepo wa shule za sekondari za kata zenye ubora huu wa elimu tunaoufahamu, ambazo
  wanasoma watoto wa pangu pakavu na uwepo wa private schools wanazosoma watoto wa wenyenacho. (Makofi)


  Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nimependekeza na kutoa ushauri kwa Serikali ili kuweza kupunguza

  tofauti iliyopo kati ya walio nacho na wasio nacho ni lazima walimu ambao wanafanya kazi katika mazingira
  magumu wapewe motisha maalum ambazo zinaweza zikawa calculated kijiografia au kwa vigezo vingine ambavyo
  vinatokana na tafiti mbalimbali. (Makofi)


  Je, Serikali imejipanga vipi katika kutoa motisha kwa walimu wanaoishi katika
  mazingira magumu ikiwa ni pamoja na nyumba, mikopo ya vyombo vya usafiri na posho
  za hardship katika kazi zao. Ahsante.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Easy does it Dr.

  Sometimes you get carried away and dilute your good qualities....
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa Tanzania kwa nini huwa hamfanyii hata simple calculations hizo nadharia zenu?
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mawazo ya jinsi ya kuboresha elimu yetu pamoja na mfumo wetu wa elimu yamekuwa yakitolewa na wadau mbalimbali na kwa upana sana tena katika mitazamo mbalimbali, lakini binafsi sijawahi kushawishika kama serikali yetu iko tayari kutekeleza maboresho muhimu katika sekta ya elimu yatakayosaidia kuliinua kundi kubwa la masikini ambalo watoto wao wameendelea kupata elimu duni na hatimaye kuishia kufeli na kurudi vijiweni kuvuta bangi na kujiajiri kwa kutembeza soksi na chewing gums barabarani.

  Na hii inafanyika makusudi na watawala kwakuwa wanataka watoto wao na wajukuu wao waendelee kuwaburuza watanzania masikini hawa miaka baada ya miaka. Lakini pamoja na hayo kitu ambacho watawala hawa wanatakiwa kufahamu ni kwamba siku hawa watanzania masikini wakichoka hawatokuwa na cha kupoteza kwahiyo wataamua liwalo na liwe, na siku hiyo ndipo kutakuwa na kilio na kusaga meno.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hivi mheshimiwa kigwangalla ni wakati gani unakaa kwenye ofisi yako kuwasaidia na kukusanya kero za wapiga kura zako muda mrefu upo kwenye vyombo vya habari kama una hamu ya kusema sana nenda kwenye kampeni Arumeru useme mpaka mdomo ukauke
   
 6. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ushauri umekuwa ukitolewa since alipokuwepo Mzee Ruksa mpaka leo hamna kitu.
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu kama unataka kuleta usawa katika elimu ya Tanzania anzia hapa sio kumungunya maneno na kuzunguka

  SALAMA KIKWETE PEDIATRICS DENTISTRY,UK

  Source:
  http://www.moh.go.tz/POSTGRADUATE-TO-BE-SPONSORED.pdf
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hahahah aliyekuambiaukaa ofisini ndo utajua matatizo ya wananchi wako ni nani? magamba bwana, nakupongeza kingwangalla sisi ndo wapiga kura wako tujadili na kuelimishana jinsi ya kuiendesha nvhi hii achana na hawa magamba wenzio wenye upeo mdogo, tatizo la wafanyabiashara kwenye siasa ndo hiloo mkuu!
   
 9. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kila mwajiriwa akiweka report ya vikao vya kazini na jinsi alivyochangia????!!!!!!!!!

  1. Mkuu hii si routine work kwako na you got paid for the job????
  2. Do you believe kuna watu wana attend na Kuchangia mikutano mingi sana kwa mwaka kuliko wewe???
  3. Hawa wote pia watuwekee humu jinsi walivyo participate kwenye ujenzi wa taifa???

  Kwa kiongozi kijana na msomi kama wewe kwa kweli vijana wenzako tunatarajia mengi makubwa kuliko feedback ya kikaoni.

  Angalizo; Vijana wasomi ni wengi sana ambao hawako katika siasa lakini ni miongoni mwa nguvu kazi ya Taifa na yawezekana wana matumaini makubwa juu yenu viongozi vijana mlioelimika. Ni jukumu lenu kuonesha njia kwa vitendo; as you get served from silver plates(available opportunities) your health (productivity) should reflect this
   
 10. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mbona kuna kero nyingi sana za wapiga kura ninazo na bado nahangaika kuzitatua hata sijafika nusu kuzimaliza, sasa unataka niendelee kukusanya tu kero zao kila siku? Halafu unadhani inachukua muda gani ku-copy hansard ya mchango wangu kama huu na kuanzisha mjadala? Hivi unadhani hii ninayofanya hapa siyo kazi yangu? Unaelewa maana ya uraghibishi?
   
 11. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  bora yako umemjibu wewe
   
 12. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Saidimu, sitegemei kila mtu kuweka hapa michango yake yote na hata mimi sijaweka hapa michango yangu yote na tena kila siku. Huu ndiyo mchango wangu mmoja tu nimeuweka hapa leo. Na lengo langu ni kuanzisha mjadala unaohusu jitihada zetu za kuleta usawa kwenye elimu, na hapa sileti kama MB tu eti natoa feedback ya kazi zangu, la. Naleta kama mwanabodi mwingine tu hapa, sema nina kiti cha ubunge pia (utata). Kwa mimi kama MB kuleta mjadala unaohusiana na kazi zangu ni kuamsha mjadala unaopelekea kunipanua mawazo na kunipa fikra mpya kwenye mjadala husika pia kupata picha ya wanachokitaka watanzania wenzangu kama wewe. kwangu mimi hii ni fursa ya kujifunza zaidi na pia kukusanya maoni na kisha kuyafanyia kazi. Ninaamini hii ni njia effective sana ya kufanya uwakilishi unaotarajiwa. Na zaidi nikuambie tu kuwa thru mitandao jamii nimepata marafiki wengi waliojificha nyuma ya kompyuta zao na waliotaka tuonane na kujadili mustakabali wa Taifa letu kwenye mambo mbalimbali, na wengi wamekuwa wakinipa mawazo mazuri na ushauri. Pia mitandao hii wanasoma watu wengi, kuna wahusika watasoma michango yetu hapa na kuifanyia kazi, wewe kama unakuja hapa kucheza unapoteza muda wako na unatakiwa ujifikirie mara mbili, wenzako tuko serious na hii ni kama kazi zetu za kila siku. Na nadhani hii inatosha kukuelewesha kwa nini nachangia na kushiriki hapa effectively.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umepost ili tukupongeze?
  Gamba chovu wewe!
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Naomba msome makala ya Jenerali wiki hii katika RAIA MWEMA la wiki hii....ameeleza vizuri sana
   
 15. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Dr. Hamisi nimeanza kukufuatilia muda mrefu naona unashika hichi unaacha unarukia kingine mpaka unakuwa hueleweki na pia humalizi hebu jaribu ku concentrate kwenye jambo moja liishe ndio uanze lingine unaviporo kibao
   
 16. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mh Mbunge, nilipoona hii title na kuwa imatumwa na wewe, niliacha shughuli zangu na kuifungua haraka sana. Sababu ni kwamba mimi nina shauku sana ya kupata jukwaa litakalojadili hili suala 'kisayansi'. Pamoja na nia yako nzuri ya kuuleta huu mjadala, lakini preamble uliyotoa hata haihamasishi. Can you please carry a litle research and come up with a touching data enriched introduction?
   
 17. p

  pazzy Senior Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 194
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  baada yakutoa mchango huo ulijibiwa nini?je,ulilizishwa na majibu uliyopata?wewe kama mwakilishi wawananchi ulichukua hatua gani au uliishia kuunga mkono hoja na kugonga meza kishabiki? kwayanayo endelea ndani ya nchi hii hakika mwisho wake unakalibia watanzania wasasa wameanza kujua haki zao hawatatishiwa na askali 250 kama walivyopelekwa ARUMERU? Mh kigwangalla unajisikiaje mwisho wa mwezi pale nzega unatoka bank kuangalia ballance unakuta mamilioni yako yameshaingizwa halafu mtaani WALIMU WAPYA wapo kwenye mgomo wakidai mshahara wa 200000?ukipata nafasi yakuzungumza na watawala waambie mtaani tumechoka kusubili MAISHA BORA kwakila mtanzania,tumechoka kuona madini yetu yakisafilishwa nje bila kutunufaisha,tumechoka kuona twiga wetu wakipanda ndege,tumechoka kufanya manunuzi halafu baadae tunaludishiwa chenchi kama ilivyotokea kwenye rada.....TANZANIA YENYE NEEMA NI YETU SOTE"
   
 18. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,546
  Likes Received: 1,327
  Trophy Points: 280
  We jamaa mbunge…nimekusikia ukijishughulisha na maswala ya afya ya uzazi pia……hivi una taarifa gani kuhusu muswada mpya feki wa afya ya uzazi unaohalalisha utoaji mimba(abortion) na ambao unalazimishwa kuletwa TZ kwa shinikizo la international NGOs…..na mtaletewa soon bungeni muupitishe kama kawaida yenu ya wengi wape!!.......Pia unazungumziaje kwa undani muswada huu utakaohalalisha uuwaji wa viumbe(watoto)….uki consider kuwa wanaotaka muswada huu TZ wanasema utachangia kupunguza ongezeko la watu TZ(over population) na pia maternal mortality …wakati takwimu za kidunia zimethibitisha kuwa kwenye nchi zilizowahi kuhalalisha abortion zilijikuta zikiwa na vifo zaidi (maternal mortality) kuliko nchi zile zilizokuwa zimepiga marufuku abortion???.....nataka msimamo wako juu ya hili maana hata spika wako Makinda nimemsikia akiufagilia huu muswada wa kuletwa TZ na NGOs za nje….naona nchi hii sasa mnafanya kazi kwa manufaa ya wageni na si watanzania……..soma hii link kwa mchango wako zaidi……Radical pro-abort bill being pushed on Tanzania by international organizations | LifeSiteNews.com
   
 19. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tatizo tulilonalo si tu tabaka za kielimu, kati ya walionacho na wasionacho. Bali pia ni aina ya elimu itolewayo na shule zetu. Elimu itolewayo si elimu ya kumkomboa mtanzania kutoka katika lindi la umasikini, bali ni elimu ya kumfungamanisha na umasikini na utumwa wa wakati. Wakati tunaongelea kujitegemea, elimu yetu inafundisha utegemezi. Ili tuendelee tunahitaji mapinduzi ya kilimo, viwanda, resources, madini, sekta za huduma n.k. Na ili tuendelee tunahitaji taifa la wabunifu katika sekta zote za uzalishaji mali. Lakini elimu yetu ya sasa inaendeleza utegemezi na ndio maana kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kukosa ajira, kwa sababu maelfu ya vijana wa nchi yetu wamepata elimu ya kutegemea kuajiriwa na sekta rasmi (e.g Serikalini, Mabenki, makampuni n.k). Elimu inayofundisha, Geography, History, Kiswahili, English, Mathematics, Civics, Biology, Chemistry, Physics, Commerce and Book Keeping, kwa mtaala tulionao, vijana wetu walio wengi wanatoka patupu na hauwasaidii chochote, sana sana kuwasindikiza wenzao wachache, kisha kurudi vijiweni kucheza kamari. Kwa nchi yetu mfumo wa elimu utakaotukomboa ni ule utakaoibua vipaji na kuzalisha wabunifu katika nyanja mbalimbali, kwa mfano: -
  1. Fani ya kilimo, tuwe na somo la kilimo na ufugaji (Commercial agriculture) kuanzia darasa la tatu na kuendelea mpaka form 4. Masuala ya agrochemistry, agro commerce, agro financing, crops what what, yoote yapatikane humu. Subject specialisation ianzie form three.
  2. Fani ya biashara, masuala ya biashara na uchumi yaanzie ngazi ya msingi. Biashara ni sayansi ya jamii, na kila shughuli ya kiuchumi katika jamii ni biashara (Business). Watu wetu wanapaswa kuwa na ufahamu wa elimu ya biashara, walau basic knowledge.
  3. Huduma - (Customer service), tunapaswa kufahamu kwamba kila mtu anayesababisha uwepo wa shughuli yako ni mteja wako. Mbunge, wateja wako ni wananchi unaowawakilisha, Polisi ni raia unaowalinda n.k. Ni vema kuwa na elimu ya huduma kwa wateja kwa kila mmoja wetu.
  4. Uraia. Elimu ya kujua haki na wajibu wa kila raia (Suala la kodi, rushwa, usalama wa raia, usalama wa taifa, huduma ya kwanza, uzalendo), ni muhimu kwa kila raia kuanzia darasa la kwanza.
  5. Somo la Sayansi na Ufundi. Lijumuishe aina zote za ufundi (Basics), Specialization ianzie darasa la nne.
  6. Sanaa na Michezo, watoto wafundishwe michezo mbalimbali, wajengwe kimwili na kisaikolojia, specialization ianzie darasa la nne.
  7. Masomo kama Hisabati, Lugha yawe ya lazima kwa kila fani.
  8. Masomo kama Historia, Biolojia, Jiografia, Fizikia, Kemia yawe ni ya lazima kwa ngazi za awali kwa Shule za msingi na Sekondari, kisha yafundishwe kama masomo ya kuchagua.
  Huu ni mtazamo wangu.
   
 20. c

  chikakatata JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani kazi ya MB ni kukaa ofisini tu?
   
Loading...