Majasusi watauona ufalme wa Mungu?

Ujasusi uko enzi na enzi. Joshua wa Biblia alifanya ujasusi, alikuwa jasusi na hatimaye akawa mrithi wa Musa na kuwa kiongozi mkuu wa wana wa Israel alipigana vita aliangusha ngome za maadui na kuwauwa kisawasawa Huu ni mfano mmoja.

Masharti ya kuingia mbinguni yalikuwa wazi enzi hizo kabla ya ujio wa Bwana Yesu hapa duniani pia yako wazi baada ya kuja kwa Bwana Yesu hapa duniani. Sasa sioni upekee wa jasusi ukilinganisha na binadamu wengine katika kuingia ufalme wa mbinguni. Bwana Yesu ndie njia pekee ya kweli na uzima na kwa Maneno yake Yesu mwenyewe anasema"Mimi ndimi njia ya kweli na uzima mtu haji kwa Baba yangu/Mungu ila kwa kupitia mimi" Huwezi fika kwa Mungu (mbinguni) bila ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Kiongozi wako katika maisha haya tunayo ya ishi. Huu ndio ukweli mchungu kuukubali na kuumeza kwa baadhi yetu. Lakini ndio ukweli ambao mwanadamu kaachiwa aukubali au aukatae kwa hiari na utashi wake mwenyewe.

Kwa kumalizia ndugu majasusi mlio lengwa katika huu uzi jiulize kwa nini pilato alipolazimika kumhukumu Bwana Yesu ilibidi achukue maji na kunawa mikono yake? Fanyeni majukumu yenu kwa utii na uaminifu inapobidi/ikilazimu nawa mikono yako.

Mchina wajF.
Na washawasha!
 
Uislamu upi huo mkuu unao uongelea wewe sunni, kardiani, tablji au ushia? Maana wako wanaojiita waislamu safi na bado tuko tuna dukuliwa.

Mchina wajF.
Na washawasha!

Ujasusi unaoruhusiwa kiiman ni ule wa vitani yaani nchi ikiwa katka vita ya kuokoa wananchi wake....lakini kama unafanya kwaajili ya MTU au kikundi flani hio noo.. Kwanza hata kumpeleleza mtu au jirani ni dhambi kubwa au kusikiliza mambo ya mtu ambayo hakutaka yasikike dini hairuhusu (kwa mujibu wa uislam)
 
Amani iwe nanyi

Katika kuwaza jinsi ya kuingia kwenye Ufalme wa Mungu kuna mambo mengi nimekuwa nikijiuliza ikiwepo akina nani kutokana na nature ya kazi zao wana nafasi nzuri ya kufika Paradiso na akina nani wako destined kutouona Ufalme wa Mungu kutokana na majukumu yao ya kikazi. Hapo ndipo nilipokutana na hii kazi.... MAJASUSI

Inafahamika kwamba kila nchi ina mfumo wake na vyombo vyake vya kiusalama katika kuhakikisha Taifa husika lipo salama.

Kwa mfano Marekani wana CIA(Agency ya kiataifa) /FBI (agency ya ndani ya nchi), Uingereza wana MI6, na Urusi wana GRU. Upande wa China ipo MSS, Pakistan ISS, Israel ipo MOSSAD na South Africa ipo SSA. Hizi ni baadhi ya Agency za kiintelijensia duniani zenye uwezo mkubwa unaosababishwa na teknolojia kubwa waliyo nayo pamoja na Majasusi wabobezi.

Katika kutimiza majukumu yao hawa Wana intelijensia wamekuwa wakifanya mambo mbali mbali ili kufanikisha kazi/assignment zao, na ili kukamilisha kazi zao kwa mtazamo wangu wanalazimika kufanya mambo mengi yasiyo mpendeza Mungu.

Kuua. Kuna misamiati kama ku-eliminate threat imekuwa ikitumika sana, hasa kwenye siasa za Africa, kwenye usalama wa nchi za Asia na dunia na kwenye Uchumi wa nchi za Magharibi. Kinachostua zaidi kuna wakati wanashughulikia hata mwenzao pale wanapoamini anaweza kuwaharibia, wanaita kawa COMPROMISED. Maneno ya Mungu yanasema USIUE.

Kuzini.Kuna majasusi wa kike au hata wa kiume ambao wana jiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi ili kupata taarifa. Wengine wanaingilia mpaka ndoa za watu/target katika kukusanya taarifa zao, wengine mpaka wanapata watoto ili tu kufanikisha kazi zao. Wanazini, maandako yanasema USIZINI.

Kusema uongo. Hii ni kati ya sifa kubwa walionayo wana intelijensia duniani. Hii sifa ipo katika namna mbili, namna ya kwanza ni KUTUNZA SIRI (sio dhambi) lakini kuna wakati ili Kutunza siri wanalazimika kusema Uongo. Kuna wana intelligentsia wengi wanadanganya wanafamilia zao kwamba wanafanya kazi flani kumbe kazi zao ni nyingine. Pia huwa wanasema uongo mkubwa zaidi ya huu katika kufanikisha mission zao.

Kuiba. Katika harakati za kufanikisha kazi zao, hawa jamaa wamejikuta wakiiba, hapa simaanisha fedha ama mali... La hasha, wamekuwa wakiiba taarifa kimtandao, nyaraka katika maeneo mbali mbali n.k ili kupata taarifa ambazo pengine wasingezipata kwa njia ya kawaida.

Je hawa jamaa, wana nafasi ya kuuona Ufalme wa Mungu? Je Walokole/Waislamu washika dini wana nafasi kwenye kazi kama hii?
Mbaya zaidi kuna wachungaji, mapadre, na maimamu ambao ni majasusi na wanahubiri kutoa mawaidha misikitini na makanisani
 
Ukisoma Biblia, katika kitabu cha Yoshua sura ya pili, wanaongelewa majasusi wawili waliotumwa na Yoshua kwenda kuipeleleza Yeriko. Walifikia kwa kahaba mmoja anaitwa Rahabu. Rahabu ili kuwatunza wasiuawe, aliwaficha darini na akadanganya wameshaondoka. Hivyo kupitia uongo wake, aliwaokoa majasusi hao. Pia Rahabu mwisho akaolewa na waisraeli na katika mathayo 4, ametajwa katika ukoo wa Yesu.

Kuna Ibrahimu anayetajwa kama baba wa imani, huyu naye mara mbili alidanganya kuwa Sarah si mkewe ili asiuawe. Je, kwa mifano hiyo michache, Ibrahim na Rahabu hawataingia mbinguni?
 
Nasubiri majibu
 
Hizi nyuzi za kikubwa aisee unaweza ukapita hivihivi bila kuchangia acha mimi niwe msomaji tu.
 
Binadamu wengi hawana mungu nafsini mwao, Hasa viongozi wa nchi.Na kama kila kiongozi au kila binadamu haia duniani angekuwa na mungu moyoni mwake. Kusingekuwa na mauaji. Shetani ndiye anawashawishi watu wafanye maovu.kama wote tungekuwa tunafuata mafundisho na sheria za mungu, shetani asingekuwa na uwezo wa kushawishi nafsi zetu zifanye maovu. Hivyo kwa uejewa wami. Jasusi au muuaji yeyote hana nafasi kwa mungu. Viongozi wanashawishiwa na shetani kufanya maovu kwa matakwa yao binafsi.
 
Umefanya tafasiri ya Amri kumi za Mungu bila kuangalia muktadha wa mada uliyoileta hapa. Siku zote unavosoma Biblia jitahidi kuangalia CONTEXT (Muktadha) na siyo kuangalia TEXT (Maneno tu): Wengi wetu tunaishia kusema Biblia inachanganya kwasababu tumekazana kusoma Mistari michache kama ilivyo na tunasahau kuangalia mazingira na sababu zilizoepelekea hayo mazingira kutokea.

Ukianza kusoma tokea Kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo utaona kabisa Mungu anajidhihirisha katika njia tofuati kabisa na jinsi ambavyo watu wamemzoea. Hili ndilo ambalo Yesu aliwafundisha sana Mafarisayo, Waandishi, Wanasheria na Masadukayo. Wao walikomaa na Torati ya Nabii MUSA bila kuangalia sababu zilizopelekea Jehovah kumpa Nabii MUSSA hizo Amri Kumi.

Mfano mzuri kabisa,
Sheria ya Kikuhani ya MUSSA ilikataza mtu kwenda kula Chakula cha Makuhani kilichowekwa WAKFU au mtu asiye Mlawi kusogelea Madhabanu. Mtu alikuwa akikiuka alikuwa anakufa kabisa au akipona basi ni lazima atoke na ukoma: Kwenye kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati 26:19 Mfalme Uzziah aliamua kwenda kufukiza tu Uvumba lakini akapigwa na Ukoma. Lakini Mfalme Daudi aliumwa na njaa kali sana akaenda kwenye Madhabau akafyala Mikate ya Wonyesho na akawapa na Majemedari wake lakini Mwenyezi MUNGU akaendelea kumpenda sana Daudi.

Ukiangalia hayo ya juu utajiuliza maswali kama:
  1. Hivi Mungu ana upendeleo ??
  2. Hivi Mungu huyu wa Agano la Kale ndiye wa Agano jipya ??
  3. Hivi kweli hata huyo MUNGU yupo kweli ???
  4. Hivi kweli anatujali sisi viumbe wake ???
Ukiona umefikia hatua hii, basi ni lazima ujue kwamba wewe Umesoma Biblia kwa kuangalia TEXT bila CONTEXT. Biblia inabidi isomwe kwa kuangalia Historia ya watu husika na hasahasa Siasa zao na tamaduni zilizokuwepo kipindi hivyo vitabu vinaandikwa.

Tukirudi kwenye mada yetu sasa:
Je, Majasusi watauona Ufalme wa Mungu ???
Mimi MALCOM LUMUMBA kutokana na uelewa wangu mdogo wa BIBLIA na tafasiri zangu nasema "INATEGEMEANA" kwasababu zifuatazo:

MOSI,
Ujasusi katika tamaduni za mwanadamu ni biashara inayofanywa na nchi na wala siyo mtu binafsi. Kila anachokifanya Jasusi ni kwa maslahi ya nchi yake na hawezi kufanya kitu nje ya amri kutoka kwa wakubwa zake. Hii kwenye lugha ya kitaalamu wa Sayansi ya Siasa wanaiita (The Principle of Imputability) au walisoma Biashara au Uchumi wanasema (The Principle of Master and Agent) au Wanasheria wanasema The Law of Agency.

Kifupi ni kwamba huwezi kutenga matendo ya Jasusi husika pamoja na nchi yake.
(The Actions of State Agencies are always attributed to the State they belong to).
Nikupe mifano halisi kabisa ili tuelewane .Miaka kuanzia ya 60's hadi 80's Ufaransa ilikuwa inafanya Majaribio mazito ya silaha za Nyuklia kwenye bahari ya Pacific. Sasa nchi kama New-Zealand na Australia walikereka sana na vile vitendo hasahasa Ufaransa alikuwa anfanya maksudi kwasababu ilikuwa imejitoa NATO baada ya Rais Charles De Gaulle kutotaka kufungamana na Urusi ya Kisovyeti au Marekani kwenye Vita Baridi.

Mara ya kwanza Australia alipeleka kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa (ICJ) lakini bado Ufaransa wakawa wababe. Miaka ya 1980's bado Ufaransa wakawa wanaendelea kufanya majaribio na kundi la wana mazingira likatuma Manowari yao iitwayo RAINBOW WARRIOR ili kuziua hayo majaribio. Ufaransa naye akatuma majasusi wake kutoka shirika lake la kijeshi (DGSE) wakalipua hiyo manowari yote na watu wakafia mle ndani.

Majasusi wa Ufaransa wakadakwa lakini ile ishu ikafika hadi Umoja wa Mataifa na katika kupima kitaalamu wakasema kisheria kuhusu kuangalia uhusika wa nchi katika hili. Wakasema kwamba "Vitendo vya majasusi ni vitendo vya nchi yao" hivyo basi chini ya Sheria za kimataifa kuna nadharia itwayo "STATE RESPONSIBILITY" ikakuta kwamba Nchi ya Ufaransa inatakiwa ijibu kwa matendo ya Majasusi wake.

Ufaransa akakubali na kukubaliana kwamba atawapa hao majasusi adhabu kuwafungia kwenye kisiwa miaka mitatu lakini miaka miwili baadae akatoa. Zaidi ya hayo pia alilipa pesa na gharama ambazo majasusi wake walizisababisha.

Hayo ya hapo juu yalitokea tena mwaka 1988 ambapo ilidaiwa kwamba Majasusi wa nchi ya Libya walilipua ndege aina ya Pan Am Flight 103 na kuuwa watu zaidi ya 270. Libya alikataa hiyo na kuwapeleka kabisa hao waliohusika na hicho kitendo lakini chini ya Sheria za Kimataifa na nadhari ya "STATE RESPONSIBILITY" iliaminika kwamba vile vitendo vya kigaidi vya Majasusi wa Libya vilifanywa ili kuinufaisha nchi yote ya Libya.

Mwaka 2003 Rais Muhammar Qaddafi alikubali kwenye barua aliyoituma kwa Umoja wa Mataifa kwamba wale majasusi walitumwa na Libya kulipua ile ndege hivyo anakubali kulipa gharama zote kwa ndugu na watu walioumizwa na kile kitendo.

NB: Hivyo ninachotaka kuwasilisha hapa ni kwamba kwenye mambo ya Vita na Ujasusi huwa hatuawaangalii Majasusi kama mtu binafsi lakini tunawangalia kama Vyombo vya nchi fulani. Kuna misemo tunayo hapa Tanzania mfano "Serikali ina mkono Mrefu" ikimaanisha kwamba Serikali inaweza kutumia mikono yake ambayo ni vyombo vya Dola kufanya matendo kama ambayo wewe umeyasema hapo juu. (Kuua, kulaghai, kuiba na kulala na watu kimapenzi)

Japo siku hizi kuna changamoto kubwa sana dhidi ya vitendo vya Majasusi na wanajeshi kuwa kweli ni vya Nchi husika kwasababu vitu kama Kugeuza Jeshi na Ujasusi kama vyombo binafsi vya kupatia pesa (Privatization of the Military Industry) na Ugaidi wa kipeke yako. Unakuta siku hizi nchi kama Marekani au Kampuni fulani linakuwa na kitengo cha Kijeshi au Ujasusi ambavyo vinakodishwa na kupata kabisa hela na hapa ndipo matatizo yanapoanza. Majasusi (hawaibi, hawaui au hawadanganyi) kwa maslahi ya nchi bali pesa au kundi fulani fulani la wanasiasa wenye nguvu ndani ya nchi: Hii ni hatua hatari kabisa kwasababu hao majasusi wanafanya lolote lile kwasababu mwisho wa siku hakun anayewaambia lolote. Mfano Mzuri kuna kundi moja la Mamluki (Mercenaries) liko Marekani linaitwa BLACK-WATER lilikodiwa na Wamarekani nchini Iraq ambapo walifanya Ujasusi na Kuua sana watu kwasababu tu wao walikuwa siyo wanajeshi bali walikodiwa. Hapa kwa wataalamu wa Siasa, Sheria na Biashara watelewa tena kanuni iitwayo '' CONTRACT OF SERVICE VS CONTRACT FOR SERVICE)

PILI,
Vitendo viovu (kuua, kuiba na kudanganya) ulivyovisema hapo juu wataalamu wa Biblia wameandikia COMMENTARY. Ambapo Mwanatheolojia wa Marekani kama Dr. Robert Morris anasema hivi. "When God said Thous shalt not steal "He meant to teach people to be selfish, he instead wanted them to care for others and become hard workers". Sababu ni rahisi sana Mwanadamu ataiba tu pale anapokuwa na tamaa au anapokuwa katika shida.

Anaendelea tena "When God said thou shalt not kill, he meant to teach people to control their volatile feelings like hate, envy, anger,jealousy and all other forms of malice and treachery". Hapa kumbuka kabisa Muuaji wa kwanza Duniani alikuwa ni Kaini ambapo aliua kwasababu ya chuki na wivu.

Anaendelea tena "When God said speak the truth, he meant to teach people to be trust-worthy, confident and respectful" Hapa tunaona kabisa anayesema uongo kwa kawaid huwa anamwaminisha jirani yake kuwa yuko salama au aone picha ya dunia isiyo halisi. Hivyo basi ndugu yako aweza kufanya jambo baya kutokana na maneno yako wewe.

Sasa basi ni lazima ukumbuke kwamba Wahebrania ilikuwa ni jamii ya hovyo sana isiyokuwa na misingi ya maadili kwasababu walikuwa hawana dini na wamechoka na maisha hasa baada ya kukaa chini ya Utumwa wa Wamisri kwa zaidi ya miaka 400. Wamisri waliwaaminisha hawa watu kwenye ule msemo kwamba Mwenye Nguvu ndiyo anaishi "SURVIVAL OF THE FITTEST". Huku wakiona jinsi ambavyo nchi ya Misri ikiwa na nguvu na kutawala nchi nyingine za jirani.
Sasa kimtazamo wa theolojia Mungu alikuwa na mpango wa kusafisha ile akili mbovu na ndiyo maana akawapa sheria na kanuni ambazo baadae zikaja kuwa tamaduni za Dini ya Wayahudi.

Katika mtazamo wa kitaalamu,
kama nilivyosema hapo mwanzo kabisa ni kwamba Sheria za dini ziliwekwa baina ya mtu na mtu. Hivyo Majasusi kitaalamu japo ni watu lakini katika kazi zao wao huchukuliwa kama Kiumbe kinacholinda nchi fulani. Nakuahidi kamwe huwezi hata siku moja kukuta kuna Jasusi ambaye anaweza kufanya kazi peke yake bila kutegema jasusi mwingine na kikubwa kabisa bila kupata mkono wa nchi nyuma yao.

Kama ulivyo mwili wa binadamu basi kuna Cells-Tissue-System-Organ-Organism ndivyo zilivyo idara za Kijasusi hapa duniani. Wako wengi lakini wanafanya kazi kama kiungo kimoja kinachotumikia taifa fulani. Hivyo nchi kama nchi ndiyo inayofanya hayo matendo na siyo mtu.

Hebu tusome kitendo cha "KIKATILI CHA KIUAJI"
Uuaji ni kitendo kipana sana chenye sura mbili tofauti(JANUS-FACED)
Mtu anaweza kuuliwa na mtu mwingine kwa Kukusudia (Murder) au kuuliwa kwa kutokusudia (Man-Slaughter). Sitetei uuji hata kidogo lakini Uuaji unaoweza kufanya na mtu fulani kwasababu zake za anazozijua yeye ndiyo uuji ambao BIBLIA na SHERIA imekataza.

Ukisoma THE PENAL CODE OF TANZANIA kifungu cha 196 inasomeka hivi: "Any person who of malice aforethought causes the death of another person by an unlawful act or omission is guilt of murder" Hapa anayezungumziwa ni mtu pamoja na akili yake. Leo hii ukiuua mtu kwasababu una chuki naye (Malice) basi ni lazima ujue umeua kwa makusudi kabisa. Lakini majasusi mpaka wakafikia hatua ya kufanya hivyo siyo kitendo cha mtu mmoja kujiamulia tu. Wataalamu wa kuchambua mambo wanaitwa (Analysts), wataalamu wa kisaikolojia ya nchi husika (Strategic Psychology) wanaitwa na pia majasusi hufanya majaribio ya kuwapima wananchi wa kawaida (Test of a common man) jinsi ambavyo wanaweza kupokea hiyo taarifa ya kifo cha mtu husika. Halafu kuna wale wataalamu wa kucheza na mawasiliono (Information War-Fare) wanawekwa mguu upande kwa ajiri ya kufanya mambo mawili:
  1. Kuwaandaa kisaikolojia nyie raia
  2. kutengeneza propaganda ya kuzima, kupunguza makali au kupindisha ukweli wa taarifa husika. (Mitandao imewarahisishia sana kazi)
Hivyo siyo kitu rahisi rahisi tu kwasababu wanafanya watu wengi na jambo baya zaidi au zuri zaidi ni kwamba Mashirika mengi ye Kijasusi yanaongozwa na kanuni na taratibu za kijeshi (Quasi-Military Regulations) hivyo kutii amri kutoka juu ndiyo kikubwa kuliko vyote (Upende au Usipende) na Ukigoma unashughulikiwa vizuri tu: Ukienda kumtaarifu huyo mtu (Tipping off) Unashughulikiwa vizuri tu: Ukifanya kinyume na amri na kuleta matakwa yako unashughulikiwa vizuri tu.

Kimtazamo Kisheria sasa: Kosa la Jinai ni kosa ambalo anaweza kufanya mtu akiwa peke yake. (Criminal Liability is Individual Liability) Hata kama kosa litafanywa na watu kumi kila mtu atalijibia kivyake na kupewa adhabu yake kutokana na uzito wa kile alichokichangia kwenye lile kosa (Joint Criminal Liability). Katiaka minajili hii ya kufikiri basi Jasusi yeyote akiwa anafanya kazi yake: Haijalishi ameua au amedanganya watu wangapi cha msingi ni kwamba anafanya hayo mambo yake chini ya Mwamvuli wa taifa lake basi hilo siyo kosa lake bali ni kosa la Taifa hilo lililomtuma: Hii kitaaluma huitwa CORPORATE LIABILITY. Hivyo basi Nchi kama nchi haiwezi kufanya kosa la kuua, kudanganya au kuiba kwasababu nchi siyo mtu moja (Individual) kisheria hivyo hata majasusi wake hawafanyi wovu wowote kwasababu wanafuata Sheria za nchi yao na kutimiza matakwa ya kulinda watu wao.

NB: Ikumbukwe kwamba Majasusi pia wanaweza kuua, kuiba na kudanganya kama Binadamu wengine walio nje ya mtandao wa Dola.(Mfano Mzuri ni yule Edward Snowden wa Marekani alivyoliibia taifa lake habari nyeti na kupeleka kwa adui) Inawezekana kabisa, imetokea na itaendelea kutokea kwasababu wao nao ni Binadamu kama mimi na wewe.

Katika hali ya namna hii ndiyo sasa tunaweza kusema kwamba Jasusi kaua yeye mwenye kwakuwa na MALICE AFORETHOUGHT. Kafanya kinyume na taratibu na kanuni za Shirika au nchi yake anayotumikia. Kifupi kaamua kutumia hisia zake binafsi kufanya vitendo vya kijasusi na mwisho wake mtu kama huyu hutangazwa kuwa Gaidi na hupewa Dishourable Discharge.

Upande wa pili Majasusi wanaweza kweli kuua au kufanya maovu yoyote pale ambapo wanaacha kutumikia Taifa au nchi husika na wanaanza kutumikia magenge ya Wanasiasa, Wafanyabiashara au Kikundi chochote chenye nguvu ndani nchi. Hapo ndipo tunasema hawa wanatenda uovu lakini kinyume na hapo sidhani.

NITAKUJA KUMALIZIA VIZURI BAADAE, PAMOJA NA KUJIBU SWALI LAKO.

CC: Consigliere , Red Giant , MSEZA MKULU , izzo, mtembea kwa miguu , Bukyanagandi ,herikipaji, Sesten Zakazaka , kiatu kipya , kipwate , Ntu , Maundu , silasc , TUTUO , UncleBen , baro , mdaharunga , myoyambendi , Dragoon , Prishaz , Ls man , K.Msese , brasy coco , Buhongwa Kwetu , moyes , KipajiTz , CHIEF MP , Mnabuduhe , moses john choyo , DuppyConqueror , kaburungu , Leonard Robert , reyzzap , TASK FORCE, Maalim Shewedy , Tobinho ,mbere , gwijimimi , Bilionea Asigwa, cognition
Mmmmh Lumumba uko more than deep nahisi limeulizwa swali kwenye field yko
 
Only GOD can judge
Khaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu hongera kwa kujibu kwa undani lakini pia kwa rejea mbali mbali.

Lakini katika majibu yako kuna maeneo yenye ukakasi na umejibu kwa 'humane perspective' na sio religious perspective. Mfano unaposema kwamba Jasusi anafanya kazi kwa niaba ya Taifa lake na ukatoa mifano ya ufaransa, Libya n.k. Tukumbuke Mungu anahukumu nafsi/mtu mmoja mmoja na sio kundi (serikali/taifa). Mungu ataita kila mmoja kwa dhambi alizofanya.

Pili, ni vyema ukitambua neno la Mungu sio subjective, halina muda, halina mahali, halina nani aliyelisema. NENO LA MUNGU LITASIMAMA, MAMBO YOTE YATAPITA. Bahati mbaya, binadamu wakiwemo baadhi ya wanathiolojia wamekuwa wakitafsiri neno la Mungu ili kuunga mkono hoja na agenda zao.

Pia niseme kwamba, siku hizi watu wanatumia mbinu nyingi ili ku justify dhambi, ikiwepo hii hoja ya 'Muktadha' wa kile kilichotamkwa kwenye Vitabu vya Mungu. Ukweli ni kwamba, Amri za Mungu zilikuwa na zitaendelea kuwa kipimo cha jambo flani ni dhambi ama si dhambi. Ukizini, Ukiua, Ukidanganya ili kuokoa maisha ya mtu huoni kama hiyo ni dhambi mkuu

Pia Ieleweke, sisemi kwamba mimi ni mwema sana. Pamoja na hilo nimeona bado kuna haja ya kuangazia namna MAJASUSI walivyo na changamoto katika kutafuta Ufalme wa Mungu
 
Ukisoma Biblia, katika kitabu cha Yoshua sura ya pili, wanaongelewa majasusi wawili waliotumwa na Yoshua kwenda kuipeleleza Yeriko. Walifikia kwa kahaba mmoja anaitwa Rahabu. Rahabu ili kuwatunza wasiuawe, aliwaficha darini na akadanganya wameshaondoka. Hivyo kupitia uongo wake, aliwaokoa majasusi hao. Pia Rahabu mwisho akaolewa na waisraeli na katika mathayo 4, ametajwa katika ukoo wa Yesu.

Kuna Ibrahimu anayetajwa kama baba wa imani, huyu naye mara mbili alidanganya kuwa Sarah si mkewe ili asiuawe. Je, kwa mifano hiyo michache, Ibrahim na Rahabu hawataingia mbinguni?
Kuna hoja hapo, ila je wakati huo makatazo yaliyopo kwenye Amri 10 za Mungu yalikwishatolewa?
 
Kwa Ibrahim ilikuwa bado. Kwa habari ya Yeriko, ilikuwa imeshapita miaka takribani 42 tokea Mungu atoe hayo makatazo katika mlima sinai.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom