Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Kazi imeanza haya wenye Kazi zenu hizi za Kijasusi ambao najua mpo wengi mno humu JF na mmejazana hebu tupeni ukweli wa hii taarifa ya Serikali ya nchini Malawi kuwa imewakamata Majasusi wanane ( 8 ) wa Kitanzania wakiwa wanafanya Ujasusi wao.
IMG_20161227_051544.jpg

Source: Gazeti la The Citizen la leo tarehe 27, December 2016 tena ipo front page kabisa.

Je tunaweza pia kuwajua hao Watanzania Majasusi waliokamatwa kwani yawezekana kuna wengine ni Wategemezi wetu wa Kimaisha.

Nawasilisha.
 
Ukishajua itakusaidia nini?

Tambua kuna wengine yawezekana hao waliokamatwa ni Wanafamilia wetu hivyo kupata taarifa zao ni jambo la Kisheria na la Kikatiba kabisa. Siku nyingine jaribu kuhifadhi kidogo ujinga wako hata kwa muda tafadhali! Mbona wale Makomandoo Wetu ambao kimsingi huwa hawatakiwi kujulikana kivile kutokana na Unyeti wao ila Yule mmoja wao alipofariki Watanzania hatukufichwa na tuliambiwa kuwa alikuwa ni Leutenant Rajab?
 
Sasa majasusi gani wanatembea kwa pamoja .
.au masomo waliyofundishwa hawakuzingatia ..ujasusi mission kama iyo inabid mtu ajifanye kuomba kaz hapo hapo na kujifanya mmalawi wa asili
....au ndio huwa hawasomi mossad wanavofanya kazi
 
Ukishajua itakusaidia nini?

1518010-Taxi_to_the_border_Karonga_District.jpg


Mkuu, hapo sehemu kuna mgodi unaoitwa Kayelekera ambapo ndipo pamegunduliwa hiyo Uranium.

Ila Karonga ni rahisi sana kuingia kutokea Tanzania hivyo hao wanaodaiwa wamekamatwa, wanaweza kuwa ni wanakijiji wa jirani na mpakani.

Pengine walikuwa wakishangaashangaa tu eneo hilo maana limewekwa uzio.

Malawi waache propaganda za kijinga.

Majasusi wa Tanzania hawawezi kwenda hiyo sehemu leo kienyeji hivyo wakati tayari wanaweza kuwa wanazo picha za kupigwa kutoka kwenye ndege na taarifa zote huenda wanazo tangu madini hayo yagunduliwe mwaka 2009.

Hivyo ondoa shaka.
 
Majasusi kama nyumbu au kondoo wote wanakaa au kutembea pamoja au hata kuonekana tu wakizoeana? Kama ni wa kitanzania itabidi serikali ipitie upya uaandaaji wa hawa wasalama wake. Ni kushindwa kwa hali ya juu sana katika jicho la kiusalama. Revisit revisit revisit.....
 
Nawachukia watu wanaohusudu lugha ya matusi kwa wenzao

Kumbe neno Ujinga nalo ni tusi? Nilikuwa sijui hilo Mkuu. Kwahiyo kumbe hata Mwenyezi Mungu nae basi ana matusi kwani kama Wewe ni msomaji mzuri wa Maandiko yake yaliyomo katika Vitabu vyake ( sisi Wakristo Biblia ) maneno kama Mjinga na Mpumbavu yametumika / ameyatumia mno. Naomba ufafanuzi wako katika hili Mkuu ili nijue kuwa napoteza muda wangu kwa Genius au J.U.H.A. tu!
 
Sasa majasusi gani wanatembea kwa pamoja .
.au masomo waliyofundishwa hawakuzingatia ..ujasusi mission kama iyo inabid mtu ajifanye kuomba kaz hapo hapo na kujifanya mmalawi wa asili
....au ndio huwa hawasomi mossad wanavofanya kazi

Nakumbuka kuna uzi mmoja huko nyuma tena mwaka huu huu niliandika kuhusu mapungufu makubwa ya Idara husika hasa kwa Watendaji wake wa sasa na jinsi wanavyokuwa recruited ila nilichoambulia ni lawama, kashfa na matusi japo baadhi nashukuru Mungu walinielewa na bahati nzuri leo kile kile nilichojaribu kukizungumzia na madhaifu yake kimejidhihiri huko nchini Malawi na sasa tunaanza kutafutana.

Muwe mnaheshimu mawazo ya Watu humu kwani kuna wengine japo hawapo humo Kwenu Kikazi lakini Umossad wao ulianzia tokea wakiwa tumboni bado hawajazaliwa na wanaweza wakawa wana ujuzi wa haya mambo pengine hata kushinda mlioajiriwa humo.

Mkuu naungana kabisa na Wewe tena kwa 100% kuwa kama hizo Njemba za Kiudukuzi zingekuwa imara wala wasingekamatwa hivyo na jambo la aibu sana. Bado nasisitiza kuwa mabadiliko makubwa sana yanahitajika kufanyika katika hiyo idara hasa kuanzia ngazi ya kugundua Kipaji, Kumfunza na kumfanyia Uchunguzi wa kina ( Vetting ) na kuimarisha kule Vyuoni mwao wanakopikwa.
 
Kwa jinsi wanavyofanya kazi wanaweza kukamatwa na wakafa kwa ajili ya nchi yao bila kusema lolote,pia hata huku ni ngumu kusema kuwa watu wao walikuwa huko wakifanya ujasusi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom