Majaribu tumeumbiwa wanadamu

Magoya2000

JF-Expert Member
May 7, 2017
574
1,130
Habari Wana wa JF...

Mimi ni muhanga wa kutalakina. Kesi yangu ya talaka ilifunguliwa tokea 2018 mpk Leo Bado haijaisha. Ilianzia primary court mpk Sasa ipo high court tusijadili maana ndo mambo ya kisheria yaache tu Sheria uchukue mkondo wake. Ipo hivi baada ya kutengana na X wangu nikapata sub mpya Hila alikuwa Dini tofauti nami.

Nilimpenda naye alinipenda maana alikuwa ananipenda tokea udongoni before my marriage. Nimeishi naye for 3 years nilienjoy sana maisha kiasi nikasahau maumivu ya x wangu wa ndoa. Seriously shemeji nilimkubali mno nikaona kama Mungu kanipendelea kwenye maisha. Nilijitahidi kumuhimiza abadili Dini aje kwangu alikataa hivyo nami nikaweka ngumu nikasema Kila mtu abaki na Dini yake hivyo tukaendelea kuishi pasipo kufanya commitment za kujitambulisha.

Ukweli shemeji yenu alikuwa vizuri idara zote, mapishi pia nilienjoy mno maana Kuna vyakula nilikuwa sivipendi kama tambi na majani ya kunde lkn upishi wake umenifanya nivipende mno. Niliishi naye bila stress zozote hila mnamo tar 29 April 2022 alifariki Dunia ndani kwangu kutokana na Maumivu ya koho na kifua ambaya nahisi yalisababishwa na constipation maana alikuwa ana tatizo Hilo muda mrefu.

Sikujua solution zaidi nilikuwa namsisitiza kula matunda Kwa wingi ili apate haja kubwa lkn matunda hayakumsaidia. Baada ya kifo Kuna Daktari ndo kanielimisha kwamba Hilo tatizo alitakiwa kupingwa Bomba kuvutwa uchafu wote ndo tiba. Kutokana na ushauri huu napenda pia kushare na wana jamii forum kuhusu athari za constipation.

Namshukuru Mungu familia yake ilielewa hivyo tukazika salama maana naye alikuwa anaenda kwao na kueleza ugonjwa unaomsumbua. Nimepoteza mpenzi wangu ambaye alinielewa vizuri mno. Chemistry ziliendana. Sasa naanza maisha upya Bado sijafahamu why this happen to me. Mtu ambaye alinifanya kusahau all pain I passed through Leo hii Mungu anamchukua Why this?

Please Wana jamii nahitahi ushauri wenu. Nini Mungu anakimaanisha kwangu? Maana likesi mpk Sasa haliishi Mahakamani. Ni Shida tu!!
 
Pole sana. Najua shemeji amefariki na tumemzika teyari. Ila kumbuka as long as you live and keep her memories she will always be alive. .
 
Mungu hamaanishi kitu chochote kwako. Lakini anachukia kuvunja ndoa. Na anapenda kabla ya kuishi na Mwanamke na kufanya nae tendo la Ndoa basi ufunge ndoa kwanza. Hivo chemistry ilikuwa ni yako ila siyo ya Mungu.

Ninakupa pole kwa kuondokewa na mwenzio. Kama wewe na mtalaka wako hamkuachana sbb ya Usaliti basi. Tengeneza na mke wako kaa nae sahihisha mlipo kosea. Kama Yeye bado anahitaji hiyo ndoa. Wewe sio lazima uhitaji lakini ni takwa. Kama sababu hapo juu ya kwamba labda ulimfumania na unaushahidi ni kweli basi achana nae. Kama sio hiyo Huyo ni mkeo mrudie. Mapungufu yake ndio mapungufu yako. Asante
 
Tuliachana na Mtalaka wangu sababu ni usaliti. Alipata mtu wa ndoto zake hivyo akambilia Mahakamani fasta na kuomba talaka akiamini atakuwa huru kufanya yake. Hivyo sikuwa na Option yeyote maana mapenzi hayalazimishwi.
 
Pole sana mkuu. Mlipata watoto na huyo mkeo wa kwanza? Kwa kini kesi haijaisha mpaka leo?
 
Habari Wana wa JF...

Mimi ni muhanga wa kutalakina. Kesi yangu ya talaka ilifunguliwa tokea 2018 mpk Leo Bado haijaisha. Ilianzia primary court mpk Sasa ipo high court tusijadili maana ndo mambo ya kisheria yaache tu Sheria uchukue mkondo wake. Ipo hivi baada ya kutengana na X wangu nikapata sub mpya Hila alikuwa Dini tofauti nami.

Nilimpenda naye alinipenda maana alikuwa ananipenda tokea udongoni before my marriage. Nimeishi naye for 3 years nilienjoy sana maisha kiasi nikasahau maumivu ya x wangu wa ndoa. Seriously shemeji nilimkubali mno nikaona kama Mungu kanipendelea kwenye maisha. Nilijitahidi kumuhimiza abadili Dini aje kwangu alikataa hivyo nami nikaweka ngumu nikasema Kila mtu abaki na Dini yake hivyo tukaendelea kuishi pasipo kufanya commitment za kujitambulisha.

Ukweli shemeji yenu alikuwa vizuri idara zote, mapishi pia nilienjoy mno maana Kuna vyakula nilikuwa sivipendi kama tambi na majani ya kunde lkn upishi wake umenifanya nivipende mno. Niliishi naye bila stress zozote hila mnamo tar 29 April 2022 alifariki Dunia ndani kwangu kutokana na Maumivu ya koho na kifua ambaya nahisi yalisababishwa na constipation maana alikuwa ana tatizo Hilo muda mrefu.

Sikujua solution zaidi nilikuwa namsisitiza kula matunda Kwa wingi ili apate haja kubwa lkn matunda hayakumsaidia. Baada ya kifo Kuna Daktari ndo kanielimisha kwamba Hilo tatizo alitakiwa kupingwa Bomba kuvutwa uchafu wote ndo tiba. Kutokana na ushauri huu napenda pia kushare na wana jamii forum kuhusu athari za constipation.

Namshukuru Mungu familia yake ilielewa hivyo tukazika salama maana naye alikuwa anaenda kwao na kueleza ugonjwa unaomsumbua. Nimepoteza mpenzi wangu ambaye alinielewa vizuri mno. Chemistry ziliendana. Sasa naanza maisha upya Bado sijafahamu why this happen to me. Mtu ambaye alinifanya kusahau all pain I passed through Leo hii Mungu anamchukua Why this?

Please Wana jamii nahitahi ushauri wenu. Nini Mungu anakimaanisha kwangu? Maana likesi mpk Sasa haliishi Mahakamani. Ni Shida tu!!
Acha upumbavu Chifu, unampangiaje Mungu kuchukua roho ya Mtu aliyemuumba yeye mwenyewe?

Ulitaka achukue roho yako, Baba yako, Kaka yako, Mama yako, au Dada yako wa damu?
 
Endelea na maisha, maswali ya kwanini Mungu mbona hukumuuliza Mungu wakati unampata, pengine akitokea katika maisha yako ili akuvushe hapo ulipokwama
 
Acha upumbavu Chifu, unampangiaje Mungu kuchukua roho ya Mtu aliyemuumba yeye mwenyewe?

Ulitaka achukue roho yako, Baba yako, Kaka yako, Mama yako, au Dada yako wa damu?
Sina maana kama nampangia Mungu. Title yangu umeiona. Hili jaribu naliweza, hata Ayub alipopata jaribu alilahani siku yake kuzaliwa. Hivyo tunapeana moyo tunasonga mbele ndo maisha mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: 5ty
Pole kwa msiba, kipi kinakwamisha kesi mpaka leo?
Ahsante mkuu! Mambo ya Mahakama Yana mlolongo mkubwa especial hizi kesi za matrimonial ndo balaa. Watu hanasota mno hata miaka 5 Hadi 7. Mahakama zetu za Africa Zina changamoto.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom