Majangiri ya kiarabu yanaswa


ThinkPad

ThinkPad

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
1,851
Likes
22
Points
135
ThinkPad

ThinkPad

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
1,851 22 135
Askari wa Operesheni Kipepeo wanaoendelea na kazi ya udhibiti wa ujangili ndani na nje ya Pori ya Akiba la Selous na Hifadhi za Taifa hapa nchini, wamewatia nguvuni majangili 11 wakiwemo sita wenye asili ya kiarabu.

Majangili hayo yalikamatwa huko kwenye eneo la Pori la Kimera katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kandokando mwa Pori la Akiba la Selous yakiwa yamepiga kambi tayari kwa kufanya uwindaji haramu.

Mkuu wa Opesherini Maalumu za Jeshi la Polisi nchini Naibu Kamishna (DCP) Venance Tossi, anayeongoza Operesheni Kipepeo, amesema kuwa Majangili hayo yalikamatwa kutokana na taarafa za Wananchi wa Vijiji vinavyozunguuka Pori hilo waliotoa taarifa za kuwepo kwa majangili hayo.

DCP Tossi, amesema kuwa wakati wa upekuzi kwenye kambi ya Majangili hayo zilipatikana silaha tano za aina mbalimbali ikiwemo bastola moja na Rifle nne pamoja na risasi 215 kati ya hizo 90 ni za Rifle na 25 za Bastola.

Ameyataja majangili yaliyokuwa yamepiga kambi kwenye eneo hilo kuwa ni Abdallah Edha, Abdallah Faraji Mbaraka, Mohammed Mbaraka, Ameri saidi, Mbaraka Saidi na Saidi Edha Abdallah wote wakiwa na asili ya kiarabu.

Wengine ni Hamissi Kandi, Hamissi Mohammed, Mbago Kingalu, Mbaraka Salum na Rashidi Urea ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori kwenye vijiji vinavyozunguuka pori la Akiba la Selous.

Naye Meneja wa Hifadhi ya Pori la Akiba la Selous Bw. John Mbwiliza, ambaye alifuatana na DCP Tossi katika ukamataji huo, amethibitisha kuwa Majangili hayo hayakuwa na kibali chochote cha uwindaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori nchini.

Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na taratibu, muwindaji yeyote haruhusiwi kufanya shughuli za uwindaji na kuua wanyama pasipo kuwa na kibali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori.

Majangili hayo yakiwa na magari matatu na majokofu kadhaa yenye barafu ya kuhifadhia nyama yaliamriwa kusimamisha maramoja shughuli za uwindaji katika eneo hilo tengefu la Mapori ya Akiba ya Selous na kwenda kituo cha Polisi kwa hatua zaidi.

Awali mmoja wa majangili hayo Bw. Abdallah Edha Kleb, alisema kuwa wao walikuwa na nia ya kuwinda nyama na kuwagawia bure wananchi wa vijiji vinavyozunguuka sehemu ya Pori hilo la Akiba la Selous.

Hadi sasa Operesheni Kipepeo inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Idara ya Wanyamapori nchini, imewatia nguvuni majangili zaidi ya 70 na kukamata silaha mbalimbali.

Mwisho 

Forum statistics

Threads 1,236,278
Members 475,050
Posts 29,252,638