Majangili waua na kujeruhi.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Jana nilisikitishwa baada ya kuona Wafanyakazi watatu waswahili wa kampuni ya uwindaji ya Robin Hurt yenye makazi yake jijini Arusha, na ambayo ina vitalu na kambi zake za uwindaji huko Makao(Maswa Game Reserve), wakifikishwa hospitali ya Selian hapa Arusha wakiwa hoi bin taaban , baada ya kushambuliwa kwa risasi na majangili.
Walikuwa wametapakaa damu miilini, wamevunjikavunjika viungo, na wanasikitisha sana.

Zaidi sana nilishuhudia mwili wa Mzungu, mmoja wa maafisa wa kampuni hiyo, ambaye ndiye alikuwa PH(Proffessional Hunter) wa kampuni hiyo, ukiwa unashushwa kwenye ndege toka huko porini Maswa.

Inasemekana PH huyo akiwa anaongoza wageni wake kwenye pori la uwindaji, huku wakiwa na hao vijana wa3 wasaidizi wa mwindaji mkuu huyo, walishambuliwa ghafla na kundi la majangili 8 waliokuwa wanafanya uhalifu porini humo, na kwa bahati mbaya, mzungu huyo alipatwa na risasi ya kichwa, na kufariki palepale, huku wasaidizi wake hao wakivunjwa vunjwa kwa risasi.
Wageni waliokuwa wakitembezwa walisalimika.
Majangili hao walifanikiwa kutoroka bila kupatikana.
 
Back
Top Bottom