Majambazi yateka kituo cha polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi yateka kituo cha polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kundi la watu 20 wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za moto wamevamia mji mdogo wa Nyamwaga na kuteka kituo cha polisi Nyamwaga, wilayani Tarime, mkoa wa Mara, ambapo askari wa kituo hicho walilazimika kujifungia ndani kwa saa moja kutokana na kuhofia kuuawa kwa risasi.
  Baada ya kuteka kituo hicho, majambazi hao walipora ngo'mbe sita, mbuzi saba, punda mmoja na fedha taslimu ambazo thamani yake haikuweza kujulikana mara moja.
  Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo baada ya uporaji huo askari wa kituo hicho cha polisi waliokolewa na wenzao waliokuwa doria katika kijiji cha Ganyange, kilichopo kilometa 10 kutoka eneo la tukio.
  Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo jana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Frank Uhahula, wananchi wa kijiji cha Nyamwaga wakiwemo walioibiwa ng’ombe, walisema walishindwa kutoka nje kutokana na hofu ya milio ya risasi zilizokuwa zikifyatuliwa ovyo kila kona.
  Wananchi walioibiwa mifugo ni Pius Mwita aliyeporwa ngo'mbe watano yakiwemo madume manne ya kulimia na mmoja wa maziwa wote wakiwa na thamani ya Sh milioni mbili, Paulo Fransis, aliyeporwa ng’ombe mmoja na mwingine kuuawa kwa kupigwa risasi kichwani, wote wakiwa na thamani ya Sh. milioni moja na Chacha Mahando aliyeporwa mbuzi saba na punda mmoja.
  Wakazi hao walisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5:00 usiku wakati kundi la majambazi zaidi ya 20 wakiwa na silaha za moto walipovamia kijiji hicho na kukizingira kituo cha polisi.
  Waandishi na timu ya maafisa walioongozana na Mkuu wa Wilaya walishuhudia maganda mengi ya risasi yaliyokuwa yameokotwa na wananchi wa kijiji hicho.
  Uhahula aliwasihi wananchi wa jamii ya Wairegi waliovamiwa wasijaribu kulipiza kisasi na badala yake aliwataka kushirikiana na polisi kuwabaini wahalifu hao.
  Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Kirigiti Sasi, aliliomba Jeshi la Polisi lijipange upya na kudai kuwa ushirikiano wa wananchi na jeshi hilo umekuwa mdogo kutokana na polisi kutotilia maanani taarifa zao pindi uhalifu unapotokea.
  Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wamepelekwa askari zaidi eneo hilo kufuatilia mifugo iliyoibwa.
  Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Tarime na Rorya, Costantine Massawe, pampoja na kuahidi kupambana na wahalifu hao, aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wakati wa zoezi hilo.
  Hili ni tukio la pili la uvamizi kutokea ambapo wiki tatu zilizopita majambazi waliokuwa na silaha walivamia kijiji cha Magena, mita 500 toka kizuizi cha polisi cha Magena, kilichopo kilometa tatu, kutoka Tarime Mjini.
  Katika tukio hilo, watu watatu waliuawa na ngo'mbe 19 kuporwa.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...