BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Majambazi yateka hospitali Jijini Dar
2008-07-03 11:22:43
Na Mwandishi Wetu
Majambazi yenye silaha wamevamia Hospitali ya Kinondoni maarufu kama kwa Dokta Mvungi, jijini Dar es Salaam na kuwafunga wagonjwa kwenye vitanda, kuwapora mali na kumvua nguo daktari wa zamu.
Watu hao, mbali na kuiba, walimnyanyasa kijinsia daktari wa zamu mwanamke waliyemvua nguo na kumtomasa sehemu mbalimbali za mwili.
Baadhi ya jamaa na wagonjwa waliokuwepo hospitalini hapo walisema majambazi hayo yaliwavamia juzi kati ya saa 8 na saa 9 usiku yakijifanya yameleta mgonjwa.
Walidai kuwa watu hao walikuwa wameambatana na mwanamke na kupokelewa na wauguzi na walipoulizwa shida yao walitoa bunduki na kuwaweka wauguzi wa zamu chini ya ulinzi na kumfunga mlinzi kamba pamoja na kumziba mdomo kwa plasta.
Aidha, walikwenda kwenye wodi na kuwafunga kamba kwenye vitanda wagonjwa waliokuwa wamelazwa na kuanza kuwapora.
``Baada ya kumfunga mlinzi na kuwadhibiti wauguzi waliiba fedha na kompyuta zenye taarifa na mafaili ya wagonjwa na shughuli za tiba zilizokuwa mapokezi.
``Waliiba pia televisheni na mali za wauguzi, wengine nao wakiwa mawodini waliwaibia wagojwa simu, saa, pete na mali nyingine za thamani,`` alisema shuhuda aliyewafungua wagonjwa hao vitandani.
Shuhuda mwingine alisema kuwa mlinzi huyo, licha ya kudhibitiwa hakuwa na silaha jambo lililowafanya majambazi hao kumdhibiti kirahisi pamoja na wauguzi.
Jamaa mwingine aliyekuwa na ndugu yake aliyekuwa wodini alisema wezi hao walitumia karibu saa nzima kuiba na kukusanya mali za wafanyakazi na wagonjwa bila kukamatwa na polisi.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi wa Kinondoni, Bw. Mark Karunguyeye, alipoulizwa juu ya wizi huo alithibitisha kuwa tukio hilo liliripotiwa polisi na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ambapo mpaka jana jioni wakati gazeti hili linakwenda mitamboni hakuna aliyetiwa mbaroni.
Alithibitisha pia kuwa mlinzi huyo alikamatwa na kufungwa plasta mdomoni na kwamba polisi ina taarifa za kuporwa kwa televisheni na kompyuta kadhaa zilizokuwa mapokezi lakini haina habari za wizi uliotokea wodini.
Alipoulizwa juu ya daktari kunyanyaswa kijinsia alisema hana taarifa na pia kuhusu hasara iliyotokana na wizi huo alisema uongozi wa hospitali hiyo haujaifahamisha polisi.
Kadhalika Kamanda Karunguyeye hakuweza kutaja idadi ya wagonjwa waliobughudhiwa kwenye sakata hilo.
Hii ni mara ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni kuripotiwa matukio ya wizi hospitalini ingawa kumekuwa na matukio mengi ya wizi wa watoto wachanga.
SOURCE: Nipashe