Majambazi wateka vituo vya mafuta, waua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi wateka vituo vya mafuta, waua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 18, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WATU sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za kivita jana jioni walivamia vituo viwili vya mafuta mjini hapa na kuua mtu mmoja wakati wakiwa katika harakati za kufanikisha uporaji wa fedha katika eneo la Nyihogo wilayani Kahama, hapa.

  Kamanda wa polisi mkoani hapa Daudi Siasi amethibitisha kutokea kwa tukio holo akisema lilitokea majira ya saa 12 za jioni, wakati hao waliokuwa na bunduki moja aina ya SMG na mabomu ya kutupa kwa mkono yalipokivamia kituo cha mafuta cha Lake Oil baada ya kufyatua risasi kadhaa na kufanikiwa kupora pesa kikubwa cha fedha ambacho hata hivyo kiasi chake hakikuweza kufahamika.

  Katika uvamizi huo, walimjeruhi begani mtumishi wa kituo hicho, Fatum Hamadi (22) na kumwamuru Abeid Joram (28) atoe pesa ambazo walifanikiwa kumpora na baada ya uvamizi wa kituo hicho wavamizi hao walikimbilia kwenye kituo kingine cha GBP.

  Wakiwa kwenye kituo hicho cha GBP walimwamuru mtumishi wa kituo hicho, Ibrahim Magembe (35) kuwakabidhi fedha zote za mauzo ya mafuta na kufanikiwa kupora kiasi cha fedha ambazo idadi yake pia haijafahamika.

  Kutokana na matukio hayo, polisi waliarifiwa kuhusu uvamizi wa majambazi hao na walipofika eneo la tukio walianza kuurushiana risasi na majambazi na katika majibizano hayo, mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Marco Jumanne (19) mkazi wa kijiji cha Lugela, wilayani Kahama alipigwa risasi ya kichwa na kufa papo hapo.

  Kamanda Siasi alisema, watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika katika matukio hayo na kwamba polisi wanaendelea na upelelezi wa uvamizi huo.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kawaida bongo!
   
 3. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  kahama nay imezidi.
   
 4. WIRELESS

  WIRELESS Senior Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu aliyepigwa risasi ni wale ambao huwa wanakimbilia eneo la tukio. Ni hatari sana.
   
Loading...