Majambazi wampiga risasi mke wa kigogo Arusha

Majambazi wampiga risasi mke wa kigogo Arusha

Arusha Leo

Senior Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
120
Reaction score
72
WATU wasiofahamika wamempiga risasi mke wa mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za binadamu (PINGOS), FLORA POROKWA ,ambaye amelazwa hospitali ya selian, tukio ni la jana jioni, na alilazimika kuendesha gari umbali wa kilometa moja akiwa na risasi mwilini baada ya kufumuliwa ubavuni na kutokea mgongoni, baada ya kukaribia nyumbani kwake alizimia na kupoteza fahamu akiwa kwenye gari,hawakufanikiwa kupora chochote.
 
arusha sasa inakuwa kama texas ya marekani ya zamani....enzi za ma cow boys, poleni sana wana arachuga
 
mpe pole sana hali ya arusha karibu vijana wote wanamiliki silaha za moto ndo maana matukio kama haya yanatokea mara kwa mara jeshi la polisi kuweni makini sana na kuhakikisha hali ya usalama wa jiji la arusha uko imara kila siku hawa vibaka wanaosumbua watu kamata weka mahabusu mara moja
 
Maelezo yanajichanganya. Alipigwa risasi. Akaendesha kilometa moja. Akazimia getini. Hao majambazi hawakupora kitu. Maelezo yanatia shaka!
 
Poleni sana ndugu.
Ila Arusha bwana...
Ukiwa na pesa kidogo waitwa milionea au bilionea.
Ukiwa na madaraka kiasi waitwa Kigogo...
 
Lema huyu jamani.....
Watu wanaongelea serious issue ya mtu kupigwa risasi, wewe unaongelea ushabiki wako wa CCM vs CDM.

Hivi kuwa mshabiki wa magamba, ni lazima condition mojawapo iwe akili zako, ziwe 'zimehama' kidogo?!
 
WATU wasiofahamika wamempiga risasi mke wa mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za binadamu (PINGOS),FLORA POROKWA ,ambaye amelazwa hospitali ya selian,tukio ni la jana jioni,na alilazimika kuendesha gari umbali wa kilometa moja akiwa na risasi mwilini baada ya kufumuliwa ubavuni na kutokea mgongoni,baada ya kukaribia nyumbani kwake alizimia na kupoteza fahamu akiwa kwenye gari,hawakufanikiwa kupora chochote.

pole sana ndugu! utawala wa kifisadi wa CCM ndio uliotufikisha hapa.
 
Haya mambo ni mageni sana mjini kwetu, hayakushamiri kabla ya 2010.
 
Jeshi la polisi litatupatia report yake kubaini chanzo...poleni sana wana Arusha.
 
Back
Top Bottom