Majambazi wadunga watu sindano za sumu Kilimanjaro

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
WANANCHI wa kata tatu za Wilaya ya Moshi Vijijini, wamekumbwa na hofu kubwa inayofuatia kuibuka kwa vitendo vya ujambazi huku kukiwa na madai kuwa majambazi hao hao, wanatumia sindano za sumu kuua watu.

Habari kutoka kata za Kilema Kusini, Kilema Kaskazini na Marangu zinadai kuwa mtandao wa majambazi hao wapatao 30, umekuwa ukilipiza kisasi kwa wananchi wanaojitokeza kutoa ushahidi polisi. Wananchi hao wamependekeza kutumika kwa sheria ya kuwaweka kizuizini watuhumiwa, ili kuepuka uwezekano wa kuua watu.

Habari zilizozagaa katika Kijiji cha Makami Juu, zilidai kuwa usiku wa Septemba 11 mwaka huu, majambazi walimvamia mfanyabiashara, Respich Ngowi na kumuua kwa kumdunga sindano ya sumu, “Waliiba kila kitu na wakamdunga sindano ya sumu, watu hawakuthubutu kutoka nje ya nyumba wakihofia kukatwa mapanga na kufuatiliwa na mtandao huo wa majambazi,”alidai mwananchi mmoja.

Wananchi hao walidai kuwa uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanywa na madaktari, ulithibitisha kuwa mfanyabiashara huyo alichomwa sindano mbili za sumu.

Mtandao huo ndio unaotuhumiwa kuilipua kwa petroli, nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiraracha, Andrew Lekule na kuteketeza mkewe na mtoto wao mdogo wa umri wa miaka mitano.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Kitowo huko Kilema, alidai kuwa mtandao huo ni kama umejitangazia “uhuru” kwa sababu unafanya uhalifu wakati wowote wanapojisikia kufanya hivyo, “Ukiuza nguruwe wanakufuata usiku na hata ukiuza mti wako wanakuja na mapanga wanataka pesa za mauzo. Hali si nzuri hata kidogo karibu kata nzima ya Kilema Kaskazini,”alidai.

Hata hivyo mkazi wa Kijiji cha Ruwa alilidokeza gazeti hili (MWANANCHI) kuwa pamoja na jitihada za polisi kukamata washukiwa lakini wananchi hawataki kutoa ushirikiano ikiwamo kuwatambua wahalifu, “Tatizo hapa ni wananchi ambao hawana mwamko wa ulinzi shirikishi, yaani mtu anavamia nyumbani na anapiga yowe la kuomba msaada, lakini hakuna jirani anayetoka na kutoa msaada” alidai.

Mwananchi huyo ambaye naye hakupenda jina lake litajwe, alidai kuwa kama wananchi wangekuwa na umoja, wangeweza kusambaratisha mtandao huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alikiri kuwapo kwa matukio ya ujambazi, lakini alisema tatizo ni wananchi wanaokataa kuwatambua washukiwa wala kutoa ushahidi.

Source: MWANANCHI
 
Hii story ni kweli nilikuwa kilema Makami juu, Sango, Kisangiro na Marangu kwa Mrema jumatatu hii. Huyo Bwana alielezwa kwenye post hapo alikuwa ni mfanyabiashara wa M-Pesa.
 
poleni sana wanainchi wa kilimanjaro naiomba serikali ilitafutie ufumbuzi wa haraka sana jambo hili kwani linahatarisha amani yetu tanzania ni nchi ya AMANI na tunapenda AMANI:A S-heart-2:
 
wachaga inabidi mbadilike pesa zinatafutwa sio kwa style hiyo,huku kwetu temboni wachaga ndio majambazi wakubwa inafika hatua watu wanakimbia nyumba zao wanaenda kupanga kinondoni
 
Wachagga ni waizi wakubwa? Kweli huna la kuchangia hapa. Badala ya kushauri ni kwa jinsi gani ufumbuzi wa tatizo utapatikana unang'ang'ana na wachagga. Mtu yeyote anaweza kuishi uchaggani na akawa mhalifu. Hata hivyo hiyo inaonyesha ni kwa jinsi gani nchi imekosa utawala bora. Serikali gani inawaacha wananchi wake wapigwe sindano za sumu na majambazi? Wale askari wanaolipua raia wema si wangetumika kuwalipua hawa majambazi? Mungu utusaidie watanzania tunaouawa kwa kukosa ulinzi na usalama.
 
Hawa wakipatikana wahukumiwe kifo cha kuchomwa moto bila kujali haki za binadamu maana si binadamu hawa. Je serikali yetu iliyoahidi maisha bora iko wapi na inanufaikaje na hii hofu kwa wananchi? Bila kukomesha ufisadi na kutoweka maadili ya jinsi ya kupata utajiri wabongo mtamalizana bure.
 
wewe unadhani hawa watapatikana?, kwa njia gani?, si umesikia polisi wamshasingizia kuwa raia hawawapi ushirikiano?, wewe jiulize polisi wanatumia tax payers' money kufanya mafunzo na kununua silaha but when it comes to combating crime wanataka raia ndo waawafanyie kazi!, kwa sasa uharifu ndiyo biashara inayolipa kwasababu waharifu hawabugudhiwi, join now.
 
na ukitoa taarifa ni hao hao polisi wanaowaambia majambazi kwamba fulani na fulani ndio wamekutaja sasa hapo unafikiri ni mwananchi gani atashirikiana na polisi wanafiki.kwa mtaji huu vibaka na wezi watauawa na kuchomwa moto sana.ila usalama wa nchi unazidi kupotea.
 
WANANCHI wa kata tatu za Wilaya ya Moshi Vijijini, wamekumbwa na hofu kubwa inayofuatia kuibuka kwa vitendo vya ujambazi huku kukiwa na madai kuwa majambazi hao hao, wanatumia sindano za sumu kuua watu.

Habari kutoka kata za Kilema Kusini, Kilema Kaskazini na Marangu zinadai kuwa mtandao wa majambazi hao wapatao 30, umekuwa ukilipiza kisasi kwa wananchi wanaojitokeza kutoa ushahidi polisi. Wananchi hao wamependekeza kutumika kwa sheria ya kuwaweka kizuizini watuhumiwa, ili kuepuka uwezekano wa kuua watu.

Habari zilizozagaa katika Kijiji cha Makami Juu, zilidai kuwa usiku wa Septemba 11 mwaka huu, majambazi walimvamia mfanyabiashara, Respich Ngowi na kumuua kwa kumdunga sindano ya sumu, “Waliiba kila kitu na wakamdunga sindano ya sumu, watu hawakuthubutu kutoka nje ya nyumba wakihofia kukatwa mapanga na kufuatiliwa na mtandao huo wa majambazi,”alidai mwananchi mmoja.

Wananchi hao walidai kuwa uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanywa na madaktari, ulithibitisha kuwa mfanyabiashara huyo alichomwa sindano mbili za sumu.

Mtandao huo ndio unaotuhumiwa kuilipua kwa petroli, nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiraracha, Andrew Lekule na kuteketeza mkewe na mtoto wao mdogo wa umri wa miaka mitano.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Kitowo huko Kilema, alidai kuwa mtandao huo ni kama umejitangazia “uhuru” kwa sababu unafanya uhalifu wakati wowote wanapojisikia kufanya hivyo, “Ukiuza nguruwe wanakufuata usiku na hata ukiuza mti wako wanakuja na mapanga wanataka pesa za mauzo. Hali si nzuri hata kidogo karibu kata nzima ya Kilema Kaskazini,”alidai.

Hata hivyo mkazi wa Kijiji cha Ruwa alilidokeza gazeti hili (MWANANCHI) kuwa pamoja na jitihada za polisi kukamata washukiwa lakini wananchi hawataki kutoa ushirikiano ikiwamo kuwatambua wahalifu, “Tatizo hapa ni wananchi ambao hawana mwamko wa ulinzi shirikishi, yaani mtu anavamia nyumbani na anapiga yowe la kuomba msaada, lakini hakuna jirani anayetoka na kutoa msaada” alidai.

Mwananchi huyo ambaye naye hakupenda jina lake litajwe, alidai kuwa kama wananchi wangekuwa na umoja, wangeweza kusambaratisha mtandao huo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alikiri kuwapo kwa matukio ya ujambazi, lakini alisema tatizo ni wananchi wanaokataa kuwatambua washukiwa wala kutoa ushahidi.

Source: MWANANCHI

Jamani wanavijiji wa Kilimanjaro huu uovu unapiliza. Shikaneni na kuwa kitu kimoja kwa kuweka doria hadi muwakamate hawa. Wachagga mnajua kutumia ulinzi shirikishi. Wekeni Sungusungu na atakayekamatwa ashughulikiwe na awe mfano kwa wengine. Mkifanya hivyo mtalala milango wazi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Hakuna mwenye haki ya kupigwa sindano za sumu, kuchomewa nyumba, au kuuliwa. Kila raia ni mlinzi na mnaweza kuwakosha hawa majambazi hata kama wako hamsini. Msikubali kuishi kwa hofu kwa sababu nchi haina serikali, ulinzi, au usalam kwa raia. Wote mkiungana mtatoa ulinzi na usalama kwenu bila hata msaada wa mtu yeyote yule!
 
Mrema hayo si majimbo yake?kwa vile alifanya kazi nzuri sana wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani basi atumie mbinu hizo hizo akiwa kama mbunge wa huko mfano:kuhamasisha wananchi wa maeneo hayo kujenga vituo vya kutosha vya polisi ili kuweza kuzibiti huo ualifu,kuwahamasisha wananchi kuwataja hao wahalifu manake wanajulikana manake wanaishi na jamii.nk
 
Polisi watu wanaostaili kuwaua kwa mabomu hamuwaui mnakua ua raia na waandishi.
Haiwezekani watu waishi kwa hofu kama wako Darfur kisa majambazi what are u people doing RPC OCD na uyo jamaa wa upelelezi sijui title yake.
 
Back
Top Bottom