Majambazi Dar yaua dereva


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
WATU wanaoaminika kuwa ni majambazi jijini Dar es Salaam, wamemuua kwa kumpiga risasi, mmoja kati ya watu wawili waliowavamia.

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi saa 3:30 usiku katika maeneo ya makutano ya Babara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ile ya Sam Nujoma (Ubungo), baada ya majambazi hao kuvamia gari aina ya Mark II.

Gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Pascal Wiliam wa Kiwanda cha MM, lilikuwa linatokea Mwenge kuelekea Mbezi ya Kimara.

Katika tukio hilo, dereva Wiliam alikufa katika eneo la tukio baada ya kupigwa risasi kichwani na kifuani wakati mtu mwingine alipigwa risasi mbili sehemu ya mbavu.

Habari ambazo gazeti hili ilizipata jana zilisema gari hilo lilikuwa linampeleka Mbezi mfanyabiashara mmoja wa eneo hilo, ambaye inasemekana kuwa katika tukio hilo alinusurika baada ya kujificha chini ya kiti cha gari.

Habari zilisema hata hivyo majambazi walimpiga risasi mbili mgeni wa mfanyabiashara huyo wa kike.

Kwa mujibu wa habari hiyo,majeruhi huyo sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kwa matibabu.

Mwili wa marehemu Wiliam umesafirishwa kwenda Chalinze Msewe, kwa mazishi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kalinga alithibitisha habari kuhusu tukio hilo, lakini alisita hakulizungumzia kwa kina kwa maelezo kuwa taarifa zaidi ziko Kituo cha Polisi Urafiki.
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,580
Likes
39,002
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,580 39,002 280
Majambazi wanaua wasio na hatia...
Hata walinzi wetu pia wanaua wasio na hatia.
 
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
33,728
Likes
36,253
Points
280
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
33,728 36,253 280
kila siku habari ni majambazi!tena yanaua tu hakuna msalie mtume,hali ya uhalifu sasa imezidi,vibaka nao wanatumia magari kupora watu,selander bridge napo eti kuna vibaka wanaibia motorist!masaki oysterbay kote huko kuna vibaka!!kama hawawezi kulinda huko kwao masaki na oysterbay watatulinda sisi wa manzese??hii nchi imeoza kabisa naona kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake kama mbuzi....nafikiri kondoo ndio jina zuri
 
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2008
Messages
2,720
Likes
34
Points
145
M

Mundu

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2008
2,720 34 145
Tanzania ya leo uwajibikaji sifuri... Kuna siku utasikia wanaanza kuteka mafisadi na kuanza kudai fedhwa. Yakianza kuwakuta wao ya jinsi hii, lazima watapata majibu ya matukio haya ya kipuuzi. Yaani sasa hivi wananchi wanauwawa na majambazi, no body cares, madereva wanasababisha ajali na kuua abiria kwa mwendo kasi na careless driving, no body cares, wafanyakazi wa TRL hawalipwi mishahara yao, no body cares; wanafunzi wanafeli kuliko miaka ya nyuma, no body cares!

By the way, who cares?
 

Forum statistics

Threads 1,251,233
Members 481,615
Posts 29,763,433