Evans-Arsenal
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 868
- 1,385
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017. Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akifungua semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika walio katika Mapambano ya Rushwa (APNAC) tawi la Tanzania kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma.