Majaliwa ni "Diver"na sio "Fire Fighter"

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,943
Naipongeza serikali kwa kumpatia ajira Majaliwa. Lakini ninakosoa aina na mahali walikompeleka.

Majaliwa ni shujaa mzamiaji wa Majini
(Deep Water Diver), kwenye vina virefu vya Maji na siyo majumbani kwenye Swiming Pool au Kwenye Matundu ya vyoo ambako ndio hasa zimamoto wanawajibika.

Lakini pia nimeshangaa kusikia kwamba Majaliwa tayari amesajiliwa na serikali kwenye Jeshi la Zimamoto.
Na tayari yuko mbioni kupelekwa Handeni Tanga, kwa Mafunzo ya Miezi minne na baadae ataanza rasmi kazi yake katika ajira hiyo mpya!

Sasa nikajiuliza maswali haya ya msingi.

Hivi kwa Mafunzo ya miezi minne pekee, tayari mtu anakuwa Askari "Competent" wa uokoaji na Zimamoto?

Hivi kwa miezi minne pekee, unakuwa tayari umepitia mafunzo ya uokoaji wa Mioto ya aina zote, kuanzia
  • Uokoaji na uzimaji mioto kwenye majengo Marefu
  • Uokoaji na uzimaji moto Viwandani.
  • Uokoaji na uzimaji mioto kwenye Sehemu zenye Msongamano mkubwa wa Majengo na watu.
  • Uokoaji na uzima moto katika viwanja vya Ndege
  • Uokoaji na Uzima moto katika vyombo vya Majini.

Hapo bado hatujaongelea mafunzo ya ukakamavu na ujasiri wa mbinu za kijeshi, kwa mtaala wa jeshi lao la zimamoto.

Kama hao askari wa zimamoto huwa wanafundishwa kwa mtindo na speed ya zimamoto ndiyo maana huwa tunawaona wakishindwa kwenye matukio na majanga mengi ya moto nchini.

Miezi minne ni muda mfupi sana kwa mafunzo ya kitengo nyeti kama jeshi la zimamoto!

Hiyo ilipaswa kuwa ni muda wa kukaa darasani pekee, ili kuzijua aina mbalimbali tofauti za mioto. Pamoja na jinsi ya kuzijua chemical husika kwa kila aina ya moto. Baadae ndio angepelekwa kwenye field training.

Lakini pia huyo kijana ni Diver na sio mzimamoto!

Alamsikhi!
10101
 
Kumbe serikali bado inaajiri std 7.? Ingefaa wamuulize anataka nini siyo kukurupuka kumpeleka jeshini wakamsumbue akimbie.
 
Dogo watakuja kumuua bure , watakuja mpeleka kwenye mission ngumu alaf wamtelekeze ajifie , huyo anatakiwa afanye kazi na watu wa Karba yake kama wale wavuvi wenye upendo unaofanana , imagine amedumbukia kwenye maji akazimia wenzake wakamuwah kumtoa , huko kwingine atatekelekezwa tuu
 
Mama Samia nakuomba umtoe huyu kijana Jasiri Majaliwa kwenye kazi ya zima moto na umpeleke NAVI huyo kijana ni mdogo anaweza chukua mafunzo hata miaka kumi walahi
Kwa hisani yako takusihi umtoe huko zima moto jamani uwiii!
 
Hapo wangemuuliza anataka kuwa nani kuliko kumkimbiza tu huko. Mm jeshi naelewa ni moto, huyu dogo atakimbia tu
 
Binafsi najaribu kulitazama hili Kwa jicho tofauti. Huu ni utaratibu wa kutoa ajira nchini? Huyu kijana ilifaa kupo ngezwa na kumpa zawadi. Suala la kumuajiri likipatwa lifuate kanuni na sheria za nchi.
 
Kumbe serikali bado inaajiri std 7.? Ingefaa wamuulize anataka nini siyo kukurupuka kumpeleka jeshini wakamsumbue akimbie.
Kwa taarifa yako,#Majaliwa sio standard 7 yako unayoiongelea.
Ni kijana mwenye O-level tena iliyokaa vizuri.
Sasa hivi kutokana na ukosefu wa ajira,watu wanaangalia fursa zilizopo,na vyeti wamevifunika majumbani.
Sababu vinachakaa kwa kuvitembeza kila ofisi bila mafanikio.

Kwenye machinga pekee....kuna graduates wa kutosha,achilia mbali bodaboda na kwingineko.
 
Dogo watakuja kumuua bure , watakuja mpeleka kwenye mission ngumu alaf wamtelekeze ajifie , huyo anatakiwa afanye kazi na watu wa Karba yake kama wale wavuvi wenye upendo unaofanana , imagine amedumbukia kwenye maji akazimia wenzake wakamuwah kumtoa , huko kwingine atatekelekezwa tuu
Bora hata wangempatia mtaji wa Nyavu na Mtumbwi ili ajiwezeshe akiwa pale pale.
 
naona kama imewakera zimamoto , maana dogo kawaaibisha hivi kila mtu apambane na hali yake
Usiwe simple minded person,sisi au mimi tangu lini nikawa zimamoto?

Muwe mnajafili kitu kwa fikra pevu.

Kama unashindwa,sio lazima uhangaike kuchangia kik**a!
 
Kwa taarifa yako,#Majaliwa sio standard 7 yako unayoiongelea.
Ni kijana mwenye O-level tena iliyokaa vizuri.
Sasa hivi kutokana na ukosefu wa ajira,watu wanaangalia fursa zilizopo,na vyeti wamevifunika majumbani.
Sababu vinachakaa kwa kuvitembeza kila ofisi bila mafanikio.

Kwenye machinga pekee....kuna graduates wa kutosha,achilia mbali bodaboda na kwingineko.
Aliishia form 2
 
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeundwa na kufanya kazi chini ya sheria namba 14 ya mwaka 2007 “FIRE AND RESCUE FORCE ACT”. Majukumu makubwa ya Jeshi
Naipongeza serikali kwa kumpatia ajira Majaliwa. Lakini ninakosoa aina na mahali walikompeleka.

Majaliwa ni shujaa mzamiaji wa Majini
(Deep Water Diver), kwenye vina virefu vya Maji na siyo majumbani kwenye Swiming Pool au Kwenye Matundu ya vyoo ambako ndio hasa zimamoto wanawajibika.

Lakini pia nimeshangaa kusikia kwamba Majaliwa tayari amesajiliwa na serikali kwenye Jeshi la Zimamoto.
Na tayari yuko mbioni kupelekwa Handeni Tanga, kwa Mafunzo ya Miezi minne na baadae ataanza rasmi kazi yake katika ajira hiyo mpya!

Sasa nikajiuliza maswali haya ya msingi.

Hivi kwa Mafunzo ya miezi minne pekee, tayari mtu anakuwa Askari "Competent" wa uokoaji na Zimamoto?

Hivi kwa miezi minne pekee, unakuwa tayari umepitia mafunzo ya uokoaji wa Mioto ya aina zote, kuanzia
  • Uokoaji na uzimaji mioto kwenye majengo Marefu
  • Uokoaji na uzimaji moto Viwandani.
  • Uokoaji na uzimaji mioto kwenye Sehemu zenye Msongamano mkubwa wa Majengo na watu.
  • Uokoaji na uzima moto katika viwanja vya Ndege
  • Uokoaji na Uzima moto katika vyombo vya Majini.

Hapo bado hatujaongelea mafunzo ya ukakamavu na ujasiri wa mbinu za kijeshi, kwa mtaala wa jeshi lao la zimamoto.

Kama hao askari wa zimamoto huwa wanafundishwa kwa mtindo na speed ya zimamoto ndiyo maana huwa tunawaona wakishindwa kwenye matukio na majanga mengi ya moto nchini.

Miezi minne ni muda mfupi sana kwa mafunzo ya kitengo nyeti kama jeshi la zimamoto!

Hiyo ilipaswa kuwa ni muda wa kukaa darasani pekee, ili kuzijua aina mbalimbali tofauti za mioto. Pamoja na jinsi ya kuzijua chemical husika kwa kila aina ya moto. Baadae ndio angepelekwa kwenye field training.

Lakini pia huyo kijana ni Diver na sio mzimamoto!

Alamsikhi!
10101

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 
Naona raia wanabishana na mamlaka ya Rais kwa mujibu wa katiba...
 
Back
Top Bottom