Majaliwa kastaafu siasa au kastaafishwa?

Majaliwa kastaafu siasa au kastaafishwa?

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
10,959
Reaction score
13,425
1751481933942.png

Kwa umri wake, katika siasa, Kassim Majaliwa Majaliwa bado ni kinda. Je, sasa inakuwaje hagombei ubunge tena? Je, amestaafu au kastaafishwa? Nani aweza kuwa waziri mkuu baada yake?

Je, hili linasema nini kuhusiana na Mama na Watu wa Jiwe?
 
View attachment 3391785

Mhe.Kasimu Majaliwa kastaafishwa kwa aibu kubwa sana!!
Si angemwambia tu mapema kuwa sikutaki hata Ndani ya Bunge ili Majaliwa aage kwa heshima!!!?
Ona sasa heshima ya Kassimu imeshuka Hadi negative!!
Jana wakati anaongea alikuwa ame frustrate Hadi nywele kashindwa kuchana!!
Pole sana Majaliwa ,ulidhani uchawa wa Kila wakati kumuita " Dakta" utakusaidia!!!
Usicheze na waswahili bwana!! Hii imedhihirisha ulipigwa chini kitambo but ikaonekana gharama yake ni kubwa ikabidi uwe managed!!
Pole sana Majaliwa ila umeondoka kwa aibu sana!!
 
View attachment 3391785
Kwa umri wake, katika siasa, Kassim Majaliwa Majaliwa bado ni kinda. Je, sasa inakuwaje hagombei ubunge tena? Je, amestaafu au kastaafishwa? Nani aweza kuwa waziri mkuu baada yake?

Je, hili linasema nini kuhusiana na Mama na Watu wa Jiwe?
Kusema Mzee Majaliwa ni kinda huo ni unafiki tena unafiki wa mchana kweupe. Umri wa kustaafu nchi hii ni miaka 60, tunawezaje kumuita mzee wa miaka 65 kinda? Tulitakiwa tuipokee taarifa hii kama changamoto kwa wazee wengine wenye umri kama wake au zaidi yake kufuata njia yake. Sio busara akina Ndugai, Lukuvi na wenzao kufukuzana na vijana majimboni. Wazee wetu wasisubiri kustaafishwa kama alivyostaafishwa John Malechela na Livingstone Lusinde, itapunguza heshima yao kwenye jamii. Hawa wazee wanamchango mkubwa kwenye nchi yetu, lakini ni muhimu tukakubali ukweli kuwa utumishi wa umma ni mbio za kupokezana vijiti, ndio maana hata urais una ukomo. Tunawashukuru kwa utumishi wao, ila tuwahimize wapumzike, watatusaidia kushauri tukikwama.
 
View attachment 3391785
Kwa umri wake, katika siasa, Kassim Majaliwa Majaliwa bado ni kinda. Je, sasa inakuwaje hagombei ubunge tena? Je, amestaafu au kastaafishwa? Nani aweza kuwa waziri mkuu baada yake?

Je, hili linasema nini kuhusiana na Mama na Watu wa Jiwe?
Amestaafishwa huyu, influence yake ni kubwa sana na Mama hataki.
 
Wiki mbili nyuma alisema atagombea. Leo kabadili gia angani. Think twice
Alhamis iliyopita , Wala sio wiki mbili ...yena alisema Bungeni ....akisoma hotuba ya kumaliza Bunge la 12....hapo lazima Kuna jambo sio Bure!
Ile kauli ya kutangwazwa kuwa anagombea hakuiyoa bahati mbaya....hata body language yake Jana,yeye na waliomzunguka ilidhihirisha kuwa Kuna jambo limetokea !
 
View attachment 3391785
Kwa umri wake, katika siasa, Kassim Majaliwa Majaliwa bado ni kinda. Je, sasa inakuwaje hagombei ubunge tena? Je, amestaafu au kastaafishwa? Nani aweza kuwa waziri mkuu baada yake?

Je, hili linasema nini kuhusiana na Mama na Watu wa Jiwe?
CCM na Bakwata wametukosea sana kutuletea Mjukuu wa Suktani kuja kutawala Tanganyika badala ya Kutuketea Ndugu Kasimu Majaliwa.

Katiba kwa kweli inampa rais madaraka makubwa sana . Hata kichaa anaweza akatawala kwa misingi ya ukichaa wake kwa sababu wanaomzunguka wanamuogopa kwa sababu ya Katiba na pia wanamuogopa kwa sababu ya ukichaa wake .

Kasimu alitakiwa achukue Form ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Oktoba 2025
Kwanza hana Roho Mbaya .
Pili sio mbaguzi
Tatu sio madini kama aliyepo
Nne ana busara sana
Tano ana uthubutu
Sita anajiamini
Saba ,ana maamuzi sahihi na kwa wakati
Nane anapenda Demokrasia na anapenda watu wa vyama vyote .
Tisa anakubalika
Kumi ana mvuto
Kumi na moja Anaijua nchi vizuri.
Kumi na mbili ,ni Mzalendo wa kweli
Kumi na tatu ,anachukia ufisadi
Kumi na nne hana mambo ya mipasho ya uswahilini
Kumi na tano anapenda maadili mazuri kwa vizazi vyetu
Kumi na sita anakemea Rushwa kwa wazi .
Kumi na saba ana uwezo wa kulinda rasilimali za Tanganyika.
Kumi na nane Hapendi ugaidi na magaidi na fedha za magaidi .
Kumi na tisa hapendi dhulma .
Ishirini Hana tamaa ya madaraka .

Kwa ujumla na muhimu kabisa ni Mtanganyika . Aliyepo sasa hana hata sifa moja katika hizo hapo juu . Lakini pia anatokea Zanzibar ambapo ni nchi yenye Rais. Katika maajabu ya Dunia ni hili la Nchi moja kutoa Marais wawili.
 
Binafsi naona hata kama amelazimishwa wamemsaidia kumjengea heshima utatokaje kwenye u pm afu urudi kugonga meza bora apumzike
 
Back
Top Bottom