Majaliwa Kasimu Majaliwa: Waziri Mkuu ambaye ameweka alama ya Uongozi kuliko Waziri Mkuu yeyote yule toka tupate Uhuru

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Toka tumepata Uhuru Majaliwa Kasimu Majaliwa ndio Waziri Mkuu ambaye ameitendea haki hii nafasi.

Miaka ya nyuma tulikuwa tunashuhudia baadhi wakitumia nafasi hii kisiasa au kujipatia Ukwasi

Lakini leo tunaona Waziri pindi anapofanya ziara mikoani kukagua shughuli za maendeleo jinsi gani anavyokagua report na kipengele kwa kipengele kujiridhisha hasa kwenye matumizi za pesa za Serikali

Ameibua madudu hasa hawa mchwa wanavyotafuna pesa za umma lakini zaidi kuchukua hatua mara moja au kumshauri Boss wake Mh Rais

Halmashauri zetu ndio ilikuwa sehemu au kichaka cha pesa za Serikali kutafunwa kupitia kwa baadhi ya Wakurugenzi ambao sio waaminifu

Mh Rais Magufuli alisema bora ujijonge kuliko kula pesa za awamu yake

Mh Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ameitendea haki nafasi hii kwa viwango na weledi mkubwa sana

Ni matumaini yangu kuona Mawaziri na watendaji wengine wote kufuata nyayo za Mh Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa

Alex Fredrick

Mbeya

FB_IMG_1570378349269.jpeg
 
Wewe Alex unajua maana ya Waziri Mkuu? Hivi huyo unayemtaja kweli unaweza kumlinganisha Waziri Mkuu WA kwanza wa Tanganyika Mwl. Julius Kambarage Nyerere, au Rashidi Mfaume Kawawa, Edward Moringe Sokoine, Cleopa David Msuya, Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Edward Lowassa? Kama unajiomesha Ili uteuliwe DC endelea kulonga.
 
una uhakika sio opportunity ya kuuza sura ya karne ya sasa tofauti na wakati mwingine ? Sokoine alikuwa na miradi mingapi ya kukagua na camera / TV ngapi ya kuhakikisha kila mwenye macho anaona
 
Dah! Ila CCM imesheheni hazina ya viongozi, Majaliwa ukimuangalia tu huna cha kumkosoa ni kiongozi mmoja makini, shupavu, hodari na mfuatiliaji
 
Hii nafasi ya waziri mkuu ambaye sio head of state haijakaa vizuri kwa kweli. Huu ujamaa tuliokuwa tunaiga kutoka kwa akina Mao na Chou En Lai wake inabidi kuuangalia upya
 
Usimlinganishe na wengine, Bali mlinganishe na malengo aliyowekewa na kiongozi wake.
Maana ukilinganisha watu, nyakati zinatofautiana na mazingira ya utendaji kazi wao pia ni tofauti kabisa.
 
Tangu 2015 todate, watanzania wamekuwa wafu wa kufikiri! Just imagine mtu anafikiri hivi!
Huoni kajitaja jina ili apate teuzi?

Hukumbuki jinsi Jerry Muro alivyokuwa anahangaika ili apate teuzi na kweli akapata
 
Sokoine alifanya vizuri sana lakini mie namkubali sana Majaliwa kwa vigezo vyangu
 
Back
Top Bottom