Majaji wapingana kuhusu Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majaji wapingana kuhusu Katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by mchonga, Dec 31, 2010.

 1. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Jaji Omary Makungu, Mwanasheria mkuu wa Zanzibar (SMZ)

  [​IMG]

  Jaji Fredrick Werema, Mwanasheria mkuu wa Tanzania

  Friday, 31 December 2010 00:14

  Na Salim Said

  MJADALA wa katiba sasa umeingia sura mpya baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Jaji Omar Makungu kutaka iundwe katiba mpya inayokidhi matakwa ya Watanzania, akipingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema anayetaka katiba iliyopo, iwekewe viraka. Jaji Makungu ni mteule wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein mara tu baada ya kuapishwa kuwa rais wa visiwa hivyo, kama ilivyo kwa Jaji Werema ambaye pia ni mteule wa kwanza wa Rais Jakaya Kikwete mara tu baada ya kuapishwa kuongoza nchi katika kipindi kingine cha miaka mitano.

  Jaji Makungu aliliambia gazeti hili jana kuwa katiba mpya ni muhimu kwa sasa kwa kuwa itasaidia kuweka misingi imara ya taifa, akipingana na Jaji Werema ambaye aliweka bayana kuwa "Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa,".

  Lakini Jaji Makungu kwa upande wake alisema "Hoja ya katiba mpya ni nzuri na watanzania wanapaswa kukaa na kutafakari ili kuweka misingi imara ya nchi yao kwa sababu misingi ya nchi inapatikana katika katiba tu,". "Kwa nini kusiwe na umuhimu wa katiba mpya sasa? Nadhali wananchi wamesema na wameonyesha kuwa kuna mahitaji na umuhimu wa kuandikwa Katiba mpya.

  Hilo hatuhitaji kujadili kwa sababu wao ndio wenye nchi," aliongeza Jaji Makungu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Alisisitiza, "Ni vizuri watu wakakaa, wakatafakari na kuandaa mapendekezo ya hoja zao kisha kuyawasilisha serikalini. Serikali nayo ni wanadamu, kukiwa na hoja ya msingi watabadilika. Tume itaundwa na mchakato wa kuandikwa katiba mpya utaanza."

  Jaji Makungu alisema wazo la kuandikwa Katiba mpya ni jema lakini watu wanatakiwa kuwa makini katika kutoa mapendekezo yao, kwa sababu hapo ndio wanapoweza kuweka misingi ya taifa lao, watoto na wajukuu zao.

  "Watu wafanye wasichoke, kama CUF walivyofanya wameandaa mapendekezo yao wamewasilisha serikali, Chadema nao wafanye, NCCR-Mageuzi na vyama vingine, wanaharakati na wadau wengine nao wafanye, serikali itabadilika tu," alisema Jaji Makungu.

  Kwa kauli hiyo Makungu ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, anaungana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan kuunga mkono hoja ya kuundwa katiba mpya.

  Madai ya Katiba mpya pia yamewahi kutolewa na Mamakamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuwa mabaya.

  Wakati Jaji Makungu akisema hayo, baadhi ya Watanzania wanaoishi ughaibuni wamesema suala la kuandikwa kwa katiba mpya ya Muungano halitakiwi kucheleweshwa tena.

  Kauli hiyo ilitolewa na Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nje kusema hatua ya Watanzania kudai katiba mpya kwa nguvu zote inathibitisha uelewa wao wa kiwango cha juu wa mapungufu yaliyomo katika Katiba iliyopo. Watanzania hao wanaoishi katika nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani pia wamekipongeza chama cha CUF kwa uthubutu wao wa kuandaa rasimu ya katiba na kulazimisha kuiwasilisha serikalini kwa maandamano ya amani.

  Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam jana na kusainiwa na Katibu wake Abdulla Abdulla, ilibainisha suala la katiba mpya ni jambo lisiloepukika kwa sasa.

  "Kwanza tunawapa pole na kuwafariji wanachama wa CUF na wananchi wote waliojeruhiwa au kukamatwa katika maandamano ya kuwasilisha rasimu ya katiba mpya; lakini tunawapongeza sana viongozi na wananchi waliojitolea kushiriki katika maandamano hayo na kufanikiwa kuiwasilisha rasimu hiyo," alisema Abdulla.

  Abdulla aliongeza, "Hatua hiyo waliyoichukua inathibitisha uelewa wao wa kiwango cha juu wa mapungufu yaliyomo katika Katiba iliyopo sasa ambayo haikidhi matakwa ya wananchi wengi wa Tanzania." "Tunaamini kuwa rasimu hiyo ni kielelezo halisi cha matakwa ya wananchi walio wengi na itakidhi kabisa hoja zote za kikatiba na kisheria ambazo kwa muda wote zimekuwa ni miongoni mwa matatizo ya msingi yanayoidhoofisha demokrasia nchini," alisema Abdulla.

  Alisema wananataraji hatua iliyochukuliwa na wananchi itakuwa ni changamoto muhimu sana kwa viongozi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ngazi zote na kila mmoja wao ataikubali na kuitafsiri kuwa ni kichocheo cha kufungua kwa upana zaidi milango ya siasa za uwazi na dira kamili ya demokrasia iliyokamilika.

  "Tunaziomba taasisi zote za kiserikali na zile ambazo si za kiserikali kuunga mkono rasimu hiyo ili nchi yetu iweze kupata katiba mpya na tuachane na tabia ya kutia viraka kwani kufanya hivyo ni kuongeza matatizo badala ya kuyatatua," alisema Abdulla.

  SORCE: MWANANCHI
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hawa wote wana matatizo.. uje mwaka mpya tutawasaidia; lakini msimamo ni kuwa tunataka Katiba Mpya, Katiba Bora.. hatutaki Katiba Mpya kwa sababu imeandikwa upya au imeandikwa na watu wengine au kwa vile inaandikwa katika zama hizi. Tunataka upya wa ubora!
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hivi ni werema na Kombani pekee ambao bado wanakigugumizi? Tell them; The revolution will never be televised!
   
 4. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkjj tupe na wewe rasimu ili mjadala uwe juu ya content,wenye nchi tunataka mpya,werema na genge lake hawana uwezo wa kutuzuia
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  naona kama wazenji wamepata loop hole ya kujichomoa kiaina
   
 6. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,075
  Likes Received: 4,658
  Trophy Points: 280
  Happy New Year..!!!, i was questiong my self saaaaaaaaana umepotea wapi? Anyway, new constitution is unavoidable, ni yetu si ya CCM ni ya wananchi
  wote wapenda haki, mafisadi na viongozi walafi wanaogopa bcoz inawabana kila kona, si kuirekebisha ( amendments) ni kuiandika mpya.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu Werema shule yake ikoje katika hii taaluma ya uanasheria???

  Huyu ni mtu mmoja ambaye amekua akitoa majibu juu mambo mazito mazito kwa kuto majibu miepesi miepesi na namna ya kushangaza sana!!! Na ukimuangalia sana unaona hulka fulani hivi ambayo ni kama vile yuko sayari nyingine na sisi wengine Wa-Tanzania wenzake kama tuko jalalani vile.


  Hakika huyu baba simuelewi hata tone. Heko Mhe Makungu kwa kusiliza sauti zetu watanzania wenzako ambao hatuko mbumbumbu saaana bali tu ni kwamba tunatofautiana michango yetu katika jamii.


  Bila washika jembe kama sisi hapa kamwe Werema hatokula cheo hivyo tusidharauliane sana vyeo ni vyeo vipo ila watu hupita.
   
 8. v

  vassil Senior Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  katiba mpya now,now,now werema hana akili nzuri
   
 9. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,075
  Likes Received: 4,658
  Trophy Points: 280
  mara nyingi hata ukienda varsity or kazini or any institution ukakuta mtu anajifanya kama yupo BUSY thru his/ her face, jua hapo
  Uvuvuzela kibao, nothing more, sijawahi ona Lawer kama Werema asiye jua haki or haki anajua then anaipindisha, hafai kabisa huyu
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mtu wa Pwani, pale CCM mlivyomshawishi Sharrif akubali matokeo na kumhakikishia ulinzi na msafara wa mabenz mlifikiri atasahau ahadi zake kwa Wazenji??... Msimamo wa CUF (Makungu) wa katiba mpya, serikali tatu na elimu bure bado uko pale pale! Kuuoanisha na msimamo wa Chadema katika hayo matatu lingelikuwa jambo rahisi kwa serikali zetu na maslahi ya Taifa zima... CCM ubishi na maslahi binafsi yametawala chama. Sasa ndipo hapo mtakapo jua kuwa MAKUNGU si ya kusukumiza ovyo-ovyo kama ndizi WEREMA, yana kokwa ngumu yale!!!!
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Steve Dii, huyu ndiye Mwanasheria Makungu ambaye sikuwahi kumsikia maishani hadi leo hii aliponikonga moyo. Mpaka hapa naseme japo Makungu wote huenda walihitimu mafunzo ya sheria hiyo hiyo lakini huyu Mtanzania mwenzetu Makungu kajifunza pia.

  Huyo baba Dr Shein kwa jinsi nilivyopata kumfahamu, ndio miongoni mwa wazee wachache nchi hii ambao ni WANYENYEKEVU WA KWELI KWETU SISI RAIA WAAJIRI WAKE, MTU MWENYE SUBIRA, HEKIMA NA KUPENDA KUJIFUNZA TOKA KWA WENGINE hata wa hali ya chini tu kama sie huku.

  Hivyo pamoja na kwamba Makungu sikubahatika kumfahamu tangu huko nyuma, kwa kuwa mteuzi wake ni Dr Shein basi sina swali zaidi. Huyu baba nafasi yake namba kumi kwenye timu ya Muungano sasa inaonekana wazi sana tu KUPWAYA HOVYO HOVYO tu!!

  Utaifa kwanza, maslahi binafsi Dowans baadaye. Sasa Makungu tukutake pale uwanja wa taifa mpya, bila vyeo vya maofisini, watu wote kwa cheo kimoja tu - uraia wako kwa taifa hili halafu tujadiliane pamoja kwamba tangu sasa kwenda mbele tungependa utawala wetu uweje.

  Werema mjigambia cheo, siku hiyo usije na cheo chako cha MWANASHERIA MKUU bali tu kile cheo cha kuwa MZALIWA WA TANZANIA tosha kazi!!!
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Uwezo Tunao, Dr. Shein is good people, no doubt about that! Ndiyo tuna m-mock every now and then kuhusu 'mikasi'... but ni mtu mwadilifu, ni almasi iliyo jalalani... kuona mng'aro wake ni vigumu kwa taka zilizoizunguka.
   
 13. King Suleiman

  King Suleiman JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Ndg zangu wana JF na wa Tz wote, huyu AG Warema ni wa kumpuuza mana tunamfahamu hoja zake na mawazo yake toka zamani kwamba ni kibaraka wa watawala waliopo madarakani wanaofurahia unyonyaji uliopo kwenye katiba hii yenye viraka vya kutosha vya kunufaisha walio kwenye serikali
  ni Warema huyuhuyu aliwashitaki upinzani kipindi cha uchaguzi kana kwamba yeye ni mwanasheria wa chama.
  Hana jipya kachaguliwa na mtu ambae katiba imemlinda asishitakiwe kwa uwizi wa kura, tena ni katiba hii imempa mamlaka makubwa hata kufikia kiwango cha kuteua kwa uswahiba, ushikaji na visasi.
  Tuwapuuze hawa wanaopinga katiba mpya tuendeleze mapambano katiba ipatikane maana inawasaidia wenyewe, mbona Kenya wameweza? Tukomaew mpaka ipatikane. "mapambano bado yanaendelea, aluta continuaaaaa"
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kuvuja kwa pakacha..... nafuu ya mchukuzi
   
Loading...