Ni sahihi kabisa.Ndugu mtoa mada nakuunga 100%.ni kama ulikuwa kwenye mawazo yangu na ni siku mbili nimetoka kulitafakari hili.
1-Mtu apewe nafasi ya kuonesha jambo,awe nacho kipaji au asiwe nacho nae anastahili kupewa moyo kwa kile anachokiamini.Kwao inaweza kuwa mchezo wa kujibu bila kujari hisia za washiriki ila kwa mshirika amefika pale kama njia moja wapo ya kutafuta mafanikio.Tusizisemee vibaya. juhudi za watu kwa kuwakatisha tamaa.
2-Kwa majaji kinaweza kuwa si kiwangi bora au pengine ni kiwango kidogo mshiriki anachoonesha but,atleast amejaribu kufanya.Kama BSS ni kutafuta vipaji,kwanin hawawi chachu ya watu vipaji kukuwa?wanaangalia kuweza ikiwa hawajui mazingira waliokulia watu licha ya kuwa wanavipaji.Waliwahi kukiri kuwa harmonize huyu sio yule,hapo ni baada ya kumkejeri,je kama ANGEYABEBA YALE ANGEKUWA WAPI?ni wangap wameshindwa kufikia ndoto zao kwa kuaminishwa na majaji hawawezi ikiwa wanaweza?
Rai yangu.
Ni vizuei kwa washiriki kutiwa moyo ili waweze kujipanga zaidi na zaidi.wengi tumefanya vizuri shuleni kwa kauli tu ya mwl "unajitahidi sana,usiniangushe mitihani hii".Neo huimarisha ndoto ya mtu na neno huua ndoto ya mtu.haina haja ya kuwajibu vibaya kisa kuwafurahisha watazamaji,mnacheza na hatma za watu wanaoamini katika ndoto zao.Ni nyinyi wenyewe mnasema ukiamini unaweza,kwann hamuwaongezei watu imani au hamtaki waweze?.Acheni ubinafsi kwa kucheza na hatma za watu kwa mlengo wa kunogesha.