Maiti yaombewa ifufuke, yagoma

Maiti yaombewa ifufuke, yagoma

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
MAOMBI.jpg

Haruni Sanchawa na Gabriel Ng’osha

HIKI ni kioja! Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege ambaye alipatwa na mauti katika Hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni jijini Dar wiki iliyopita, walifanya tukio la aina yake baada kutokukubali kama ndugu yao amefariki.



Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege wakipeleka mwili wa ndugu yao kanisani kwa ajili ya maombi.

Ndugu hao wa marehemu walizuia mwili huo kupelekwa mochwari na badala yake wakauombea kwa saa sita hospitalini hapo wakiamini ataamka, kwani ugonjwa wake ni wa kulogwa.

Kana kwamba haitoshi, baada ya muda huo kupita, ndugu hao, wanaosadikika kuwa ni waumini wa Kanisa la Ufufuo

na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima, waliupeleka kanisani hapo ambapo uliombewa zaidi ya saa mbili mwili huo ili uamke, ikashindikana.


attachment.php


Mchungaji Gwajima akiwa kazini.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, marehemu ambaye alirejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani alikoenda kuhudhuria mahafali ya mwanaye anayesoma nchini humo, alianza kuumwa kimasihara, hasa kwa vile ugonjwa wake ulikuwa haueleweki licha ya kupelekwa katika hospitali mbalimbali jijini.


Wakati akiumwa, inadaiwa kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni sikio lakini katika vipimo kadhaa alivyopimwa, havikuonyesha ugonjwa.
Kwa mara ya mwisho kuna madai kuwa alikuwa na kansa ya kichwa, kitu ambacho pia kiliwashangaza ndugu ambao walishangaa ni wapi alipoutoa ugonjwa huo mara moja.


attachment.php


Mchungaji Gwajima katika harakati ya kumtoa mapepo mgonjwa.

Inadaiwa pia kuwa wakati akiumwa, mama huyo aliwahi kupigiwa simu na mtu anayehisiwa ni mganga wa kienyeji kutoka Kigoma, ambaye haikufahamika walichoongea.

Inasemekana kuwa mara tu baada ya madaktari wa Hospitali ya Kairuki kuwataarifu kuhusu kifo cha mgonjwa wao, walizuia mwili huo kupelekwa chumba cha maiti wakiamini hajafariki, na kwamba wanataka wafanye maombi ili kumfufua.


attachment.php


Baada ya maombi ya hospitalini na kanisani

kushindikana, mchungaji aliyeongoza ibada hiyo, ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, aliwaambia ndugu hao kuwa marehemu hataweza kuamka na kuwataka waupeleke mwili huo chumba cha kuhifadhia maiti.

Waandishi wetu walimtafuta kiongozi mkuu wa kanisa hilo mchungaji Josephat Gwajima ili aweze kuzungumzia suala hilo, lakini waliambiwa kuwa yuko Japan kwa kazi ya kuhubiri neno.

Hata hivyo, mmoja wa viongozi waandamizi wa kanisa hilo, aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema maombi ya aina hiyo hufanyika kanisani hapo na mara kadhaa, watu waliodhaniwa wamefariki waliweza kuinuka.
 

Attachments

  • 2.jpg
    2.jpg
    25.6 KB · Views: 2,440
  • 3.jpg
    3.jpg
    31.7 KB · Views: 2,437
  • 4.jpg
    4.jpg
    42.8 KB · Views: 2,419
Yaani watanzania bado tuko nyuma kwanini wakatae kwamba sio kansa inaweza kuwa alikuwa nayo muda mrefu huwa hatuna tabia za kupima kila mara binadamu wanataka kumpinga hata mungu alilolipitisha
 
Hata kama ni Imani sio ivyo kwa nini wasiwe na Imani kwamba ndungu yao amekufa kwa ugonjwa na ndio mapenzi ya Mungu hayo kampenda zaidi.
 
kwa matendo kama haya ndo yanalifanya taifa letu kuwa ni miongoni mwa mataifa yanayongoza duniani kwa raia wake wengi kuwa na uelewa mdogo
 
Kazi ipo. Hizi imanizinatufanya vichaa na vituko wakati mwingine. Ni ile imani kuwa Mungu alifufua wafu. Tunasahau kuwa Mungu alikuwa msafi asiyekuwa na dhambi. Leo hii wachungaji wenyewe wafanyabiashara na mazingaumbwe yao ya nguvu za makanisa au wao wenyewe toka Nigeria.
 
Hata kama ni Imani sio ivyo kwa nini wasiwe na Imani kwamba ndungu yao amekufa kwa ugonjwa na ndio mapenzi ya Mungu hayo kampenda zaidi.


Uyasemayo ni kweli ila nafurahishwa zaidi na picha/avatar yako jinsi unavyolia na CCM kukuchezea toka utotoni mwako mpaka hapa ulipofika bila maendeleo yeyote. Je, utaipigia kura mwakani baada ya kukusambaratisha miaka yote hiyo?
 
Hivi kifo si kipo kila mtu anafaham, najua ni uchungu kuondokewa na mpendwa wako lakini inabidi kuukubali huu ukweli mchungu.
 
labda.wangempeleka kwa mganga wa kienyeji kama walivyoamini kuwa kalogwa
 
Back
Top Bottom