Maiti inayotembea

Maiti inayotembea

Roisa group

New Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
4
Reaction score
4
Riwaya.
Mtunzi: Roisa.
Number: 0694840213.

Sehemu ya 2.
Nikakumbuka wimbo wa lady jaydee na professor Jay ulitamba kipindi hicho unaitwa Bongo dar es Salaam. Ama kweli nilijionea ndani ya siku moja ilitosha kunipa picha kamili juu ya jiji hilo la wajanja.

Asubuhi, nilipanda magari ya kuelekea mabibo ambapo Chuo kikuu cha dar es Salaam kipo kwa ajili ya kuchukua shahada yangu ya kwanza ya Civil engineering.

Nilipofika geti kuu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), nilisimama kwa dakika kadhaa nikitazama ile nembo. "Hekima ni Uhuru." Nilihisi fahari isiyo na kifani. Mimi, mwana wa mkulima maskini, hatimaye nilikuwa nimefika "Mlimani."

Nilipofika chuo hapo ndipo nilipohisi kitu kigeni moyoni mwangu: mchanganyiko wa furaha na woga. Furaha kwa sababu nilikuwa nimefanikiwa. Woga kwa sababu sasa nilikuwa peke yangu katika ulimwengu mkubwa.

Hakuna mama wa kunipikia ugali, hakuna wadogo zangu wa kunichekesha, hakuna kilimo cha kufanya asubuhi. Ni mimi na vitabu vyangu tu.

Kwenye korido za Idara ya Engineering, nilikutana na vijana kutoka kila pembe ya nchi. Hapo ndipo nilipokutana na Joti. Joti alikuwa kijana mchangamfu kutoka Arusha, aliyejua kila kona ya chuo.

Alikuwa mwaka wa pili akichukua shahada ya Civil Engineering.
Baada ya kuwa nimejuana nae usajili pale yeye ndo aliniongoza hadi ofisi za usajili kwa ajili ya taratibu nyingine zaidi.

“Oya mwanangu masanja karibu Mlimani!” Joti aliniambia huku akinigonga bega. “Hapa ni kusoma tu, lakini usisahau kufurahia maisha. Pia tambua Dar siyo kijijini kwenu watu wanakuja, na ndoto nyingi kichwani lakini zimeishia kuzikwa.”

Aliniambia huku akicheka kwa utani, alionekana kukijua chuo vizuri licha wote tulikuwa alikuwa amenitangulia darasa moja na pia tulikuwa facult moja.

Niliingia ndani, nikitembea polepole kuelekea ofisi ya usajili. Wanafunzi wengine walikuwa wakizungumza kwa sauti kubwa, wakicheka, wengine wakiwa busy na simu janja.

Mimi nilikuwa kimya. Nilikuwa nimezoea maisha ya kijijini, ambapo kelele hazikuwa nyingi. Siku ya kwanza nashukuru nilikamilisha taratibu zangu za usajili na kupewa ID kunitambulisha kuwa mwanafunzi wa kwanza katika chuo hicho chenye hadhi yake ya nyota ya tano.

Wanafunzi wengi tulikuwa tukipishana, mimi ndo naonekana nilikuwa mgeni kidogo wa jiji kwa nguo zangu, nilizoea wadada wakiwa wamevaa nguo ndefu hata kama ni fupi basi ziwe za stara lakini huku walivalia nguo za aibu lakini hakuna aliyejali.

Wadada warembo, weusi, weupe, maji ya kunde, wembamba, saizi ya kati walikuwa wakipishana kila kona.
Siku za kwanza zilikuwa za mshangao. Majengo marefu ya kishindo, maktaba iliyojaa vitabu hadi dari, na wanafunzi waliokuwa wamependeza kwa mavazi ya gharama.

Nilijiona mshamba, nikitembea kwa kunyata na lile sanduku langu. Lakini kila nilipohisi unyonge, nilikumbuka machozi ya mama na ahadi yangu.

Nilipata hosteli za chuo hicho kikuu tayari kwa kuanza maisha ya kiutu uzima, bila mzazi ila mimi ndo nakuwa kama mzazi katika maisha yangu.

Siku iliyofata nilielekea chuo kwa ajili ya orientation, tulipokewa kuingia katika ukumbi mkubwa na tulikuwa wengi sana prof. Edvis Mwalomba vice chancellor wa chuo kikuu alifungua na Dean of student Eng. Dr. Masumbuko Manumbu alihitimisha kwa kutupa nasaha ambayo niliandika katika diary yangu lakini ushauri huo naona nilipuuzia
" ninyi bado ni vijana kwa asilimia kubwa mnategemewa huko mtokapo hivo chuo hiki au jiji hili lisikuchanganye ukapoteza future na destiny yako, mnasoma na watu wazazi wao wameshawaandalia njia hivo tambua hilo.. Life within the university is so short decisions are on your mind either to build and refresh your tomorrow or dig your own hole, and bare in your do not sorely engage in relationships without knowing each other past " alimalizia Eng. Masumbuko Manumbu.

Baada ya mkutano, tulipelekwa kwenye majengo ya faculty yetu College of Engineering and Technology. Majengo yalikuwa mapya kidogo, na harufu ya rangi bado ilikuwa hewani.

Nilitembea kwenye corridors ndefu, nikisoma majina ya madarasa: Fluid Mechanics, Structural Analysis, Engineering Drawing. Moyo wangu ulijaa furaha na woga pamoja.

Hii ndiyo mahali nitakapoanza kujenga mustakabali wangu.
Lakini changamoto ilianza mapema. Pesa ya kujikimu (Boom) ilikuwa bado haijaingia.

Nilianza kuishi kwa kula mlo mmoja kwa siku, mara nyingi nikiishia kula mlo mmoja wa jioni kwa kweli nilianza kuelewa kwa nini watu husema dar pagumu .

Njaa ilikuwa ikiniuma, lakini nilijifariji kwa kusoma kwa bidii. Nilikuwa wa kwanza kuingia maktaba na wa mwisho kutoka. Engineering ilihitaji akili ya chuma, na mimi nilikuwa na azma ya chuma.

Hata hivyo, kuna kitu kimoja ambacho sikukitegemea: Upweke wa mjini. Usiku, nikiwa kwenye chumba cha kulala hosteli ambapo nilifikia , niliwatazama wenzangu wakitoka kwenda "viwanja" (club) au kukutana na wasichana.

Mimi nilibaki nimejikunyata kwenye godoro langu jembamba, nikipiga mahesabu ya fomula za Calculus.

Haikupita siku bila kuwasiliana na familia yangu pia na mchumba wangu Zaituni ambae tuliweka nae miadi ya kuoana kwa baadae.

Ndoto nilizokuwa nazo niliona siku moja nikiheshimisha mama yangu ambae kwa sasa hana msaidizi yeyote na anataabika na kadhia za nyumbani.

Usiku mmoja nikiwa nimepumzika kidogo joti aliingia chumbani “oya twende leo mlimani city angalau ukatembee”, sikuweza mkatalia maana hilo jina mlimani city nilisikia tu kwenye mitandao nikaona hii ndo fursa ya kutembea kidogo.

Tuliondoka na joti alikodi uber mpaka viwanja vya mlimani city kwa kweli tembea uone kila kitu kwangu kilikuwa kigeni kisha tuliondoka tukaelekea maeneo ya club billcanas.

Nikiri kwa kweli ulimwengu wa huko ulinishangaza sana, wadada walivokuwa wamevaa niliona aibu mimi nilizoea kuona kwenye video lakini pazia jeupe naona hayo, joti aliniambia huo ni mwanzo tu. Ikawa desturi kila weekend tunaenda viwanja na rafiki yangu, yeye alikuwa mtumiaji mzuri sana wa kilevi na pia familia iliyotoka haikuwa haba hata kidogo.

“hivi masanja utaishi mwenyewe mpaka lini?” joti aliniuliza
“kwanini umeniuliza hivo?”
“maana mshikaji wangu miezi miwili sasa imepita toka uje sijawahi kukuona, na mrembo yeyote wa hapa chuo au mtaani unaniabisha kinoma sana” joti aliniambia tukiwa tunatoka madarasa ya jioni.

Upole wangu na bidii katika masomo ilikuwa silaha nzuri sana ambayo nilianza nayo sikukosa katika kipindi chochote, nakumbuka somo la fluid mechanics karibia asilimia tisini ya darasa liliwasumbua ila mimi kwangu ilikuwa kama kumsukuma mlevi.

“kwanini nakuwa nakuambia haja ya moyo wangu hupendi kunielewa Masanja?” maneno ya msichana mrembo Hamida ambae alikuwa mwaka wa pili, nilijuana nae kupitia joti siku moja tukiwa tumeenda kwenye birthday yake.

“ lakini nilikuambia kwa sasa focus yangu sio mapenzi hamida”
“I know, but am in deep love with you please receive my request. My heart is like an omen filled with vacuum inside, your the only one to fill space inside”

“No darling, I have no money to spend on your beautiful girl like you need serious attention”

Nilimjibu hamida, aliondoka kwa gadhabu nilimuita ila hakugeuka. Nilikaa nikatafakari kama kweli ananipenda atarudi ila “ mmh sina pesa, anyway aende zake huko Zaituni ni kila kitu kwangu” nilijesemea nikitoka kwenye vimbweta vilivyo maeneo ya chou chetu.

Usiku nilijaribu kumueleza joti juu ya hamida, akacheka sana “goodman that’s a chance ,a lady is good financially so you can stick with her” niliona mawazo yake hayanifai nilijilaza kitandani nikitafakari juu ya safari yangu ya Maisha ambayo niliamini ni bora sana.

Siku zilikatika sasa mwaka wa kwanza ulikuwa ukingoni nilishukuru Mungu kwa kunipa ushujaa sana.

Pesa ya boom niliyopata kwa mara ya kwanza nilimtumia mama kwa ajili ya kurekebisha nyumbani na chakula kidogo wadogo zangu walizidi kuniombea niwe kweli mkombozi wa familia kama Nyerere na Tanganyika.

Ilikuwa ni Jumatano ya mchana nikiwa nimeketi kwenye viti vya mawe nje ya maktaba ya chuo. Ghafla, simu yangu ya kitochi ilitetemeka. Ilikuwa ni ujumbe wa benki. Macho yangu yaling’ara nilipoona salio: Tsh 800,00p. "Boom" langu la pili la mwaka wa kwanza lilikuwa limeingia.

Kwa kijana aliyetoka kwenye umaskini wa Mwanza, ile ilikuwa ni zaidi ya pesa; ilikuwa ni heshima.

Wakati vijana wengine wakikimbilia maduka ya nguo na kumbi za starehe, moyo wangu uliruka kuelekea kijijini kwetu, kule ambako Mama alikuwa akipambana na njaa na baridi.

Nilikimbia hadi kwa wakala wa M-Pesa. Bila kusita, nilituma laki tano kuelekea kwa Mama. Baada ya dakika tano, simu yangu ililia.

"Halo, masanja! Mwanangu!" Sauti ya Mama ilikuwa na mtetemo wa furaha, sauti ambayo iliniaminisha kuwa mimi ndiye mkombozi wa nyumba ile.

"Mwanangu, hii pesa yote ya nini? Kwani chuo wanakulipa mshahara?"
Nilitabasamu, moyo wangu ukiwa umejaa amani. "Hapana Mama, hiyo ni pesa ya serikali kwa ajili ya mahitaji yangu. Lakini siwezi kula kuku Dar es Salaam wakati wewe unakula ugali na chumvi Mwanza. Nunua magunia ya mahindi, lipia deni la duka la Mzee Juma, na ununue kanga mpya mbili za kuvaa kanisani."

"Mungu akubariki mwanangu," Mama alilia kwa furaha. "Mungu akulinde na wabaya wa mjini. Sisi hapa tunakuombea usiku na mchana."
"Usijali Mama," niliongeza kwa sauti ya kishujaa. "Huu ni mwanzo tu.

Nikimaliza hii shahada ya uhandisi, nitakujengea nyumba ya bati, nitakuja kukuchukua kwa gari langu mwenyewe uje uone bahari. Utapumzika Mama, hautashika tena jembe."
Siku hiyo nilikuwa na furaha kuliko mwanachuo yeyote.

Nilijihisi mwanaume kamili. Nilikula chakula cha kawaida Cafeteria, nikanunua madaftari mapya, na kulala nikiwa na amani ya roho. Sikuwa na adui, sikuwa na siri, na damu yangu ilikuwa safi kama maji ya chemchemi.
Hamida alizidi kunisumbua, lakini moyo wangu haukuwa tayari sana kuwa nae kila wakati siku za weekend alikuwa akitamani anitoe out lakini nilikuwa na visingizio vingi sana.

Siku moja tulitoka na rafiki yangu joti kwenda maeneo ya osterbay kufanya maemezi kidogo maana likizo ilikarbia na ilibidi angalau nikaone mama yangu kipenzi na wadogo zangu ambao mwaka sasa sijawatia machoni,
@ kwa leo naishia hapo tuonane j4.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom