Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
Nazungumzia sisi, sisi, ninaposema sisi, wewe haupo. Ni sisi tulizaliwa huko ndanindani bila mpango, japo wazazi walifurahia kuona mtoto wa kiume au wakike amezaliwa.
Sisi wale ambao tuliishi bila malengo, linalotokea mbele yako ndio saizi yako. Sisi ambao tumemaliza chuo hakuna kazi na tumejiajiri kwenye kubeti.
Unakumbuka ile primary, kila ukiulizwa ukiwa mkubwa unataka kuwa nani, kila siku jibu lilikuwa linabadilika, mara askari, mara mwanajeshi, mara daktari yote hii ni kukosa lengo ambalo watoto wa siku hizi wanajengewa tangu wakiwa wadogo.
Tuwataje wale waliokuwa na malengo ya kujenga wakajenga vizuri nyumba, zikafika level Fulani halafu mtu akakopa ili wamalizie nyumba, baadae nyumba ikauzwa irudishe mkopo.
Aah! Malengo yaliyo na focus ni ya mlevi tu, lengo lake ni kulewa.