twende wote
Member
- Mar 29, 2021
- 50
- 84
- Thread starter
- #41
SEHEMU 4.Sehemu ya tatu,
Samahani atakae taka niendelee asome, Mimi nishasema sio mwandishi mzuri,
Ok,baada ya kupata permit ya ukaazi tulijitenga, mi nikaenda cape Town, Roby akabaki joburg, namshukuru Mungu malezi ya utotoni yalinisaidia kumudu maisha ya sauz, maana kuingia ktk ulevi wa madawa no kugusa tu,kwa maana yapo anywhere, anytime just yo cash..
Basi jamaa yangu Roby tunavoongea ni Teja Ila kwa Sasa anapata ahueni, baada ya kutoka gerezani,ambako alitumikia miaka 7.
Baada ya kuwa cape Town ki ukweli nilipata mwanamke wa umri wa mama yangu, lakn ni shida ndo zilipelekea kuingia ktk mahusiano, lakn sio poa kuoa mzee kisa njaa, ni jela huru uraiani,..
Basi nimekaa na mama huyo miaka 2 na tulipata mtoto wa kiume, wakati tuko na familia mke wangu alikuwa mfanyabiashara, akienda Sweden na kuleta vipuri mbalimbali vya kitambo na magari,Mimi nilikuwa msambazaji wa Oda ktk maofisi ya watu,,
Ilipofika mwaka 2008 tayr niliweza kupata vigezo vya kumiliki paspot ya sauzi, baada ya kupata hiyo pasi niliona tayr malengo yangu yanaenda kutimia, maana Mimi ndoto yangu haikuwa kuishi sauzi,Toka Niko mdogo nawaza Safari ya mtoni,..
Nitaendelea baadae,Ila wakatisha tamaa pungueni
Basi wakati wife analeta mzigo Mimi mapambana mtaani lakini kichwani sijaridhika, naiwaza Safari ya mbele, wife anaenda anarudi huku mi nazichanga,
Siku moja nikamueleza nataka kwnda Sweden kutalii, ikawa poa, kwa South African passport holder ni Visa free kwa nchi nyingi za ulaya, nikajiandaa na tayar nilikuwa na mawasiliano na watoto wa temeke ambao wako Sweden nyundo kibao, Basi, mchizi nikakwea pipa, destination ya kwanza uhoranzi,.ile nashuka airport nahisi kizungu zungu, maana nilikula dag la kutosha ndani ya dege la KLM, airport ni kubwa balaa, ndege yangu inaondoka kwenda Sweden mi sijielewi nimelala.
Baada ya masaa 3 nastuka nafatilia ndege yangu ilishaondoka kitambo, nikawasiliana na agent wangu, nikapewa huduma ya chakula na mahitaji yote,Ila nililipia km Dola 50 tu wenzetu wanajali Sana biashara, kesho yake majura ya saa 6 mchana nikapanda pipa, mpk mjini Oslo..
