Maisha yanavyo changanya usipokua makini.

Maisha yanavyo changanya usipokua makini.

Kampungapunga

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2018
Posts
313
Reaction score
1,100
Habari wana jamvi wenzangu na ambao mko kwenye mfungo hongereni na poleni kwa swaum kua kali.
Binafsi wakati namaliza shule na kuja jiji la watu yaani Dar kwa mara ya kwanza nilifikia kwa kaka yangu ninayemfuata kuzaliwa ambaye yeye alikua na takribani miaka 8 akiwa yuko hapa jijini, nilikuta amepanga chumba kimoja nikaishi kwake wakati huo bado kabisa sijajua maisha yakoje mana kila kitu nilikua ni mtu wa kupewa kwa wakati huo. Wakati naishi hapo nilikua naona vijana wakitaa wanavyoishi ishi vizuri nikawa najiuliza kwanini wengine wanamaisha mazuri kiasi hiki wana magari,nyumba nzuri ,wanavaa vizuri kwanini kaka yangu anamda mrefu huku lakini maisha yake ni ya chini sana.

Jumapili moja tulienda mabibo kumtembelea mjomba wangu mmoja ambaye yeye alikua na miaka kama ishirini hivi akiwa huku dar baada ya kufika kwake nilianza kupata wasiwasi juu ya maisha ya hapa mjini, mana chumba ambacho alikua anakaa kilikua cha hadhi ya chini kuliko hata kile cha bro lakini pia hata vitu alivyokua navyo ndani vilikua vya kawaida kabisa visingeweza kulinganishwa na mda aliokaa huku dar. wakati tunapiga stori mbili tatu alianza kuhadithia story ya dogo mmoja mtoto wa jilani yetu mkoani ambaye yeye alikua na kama miaka mitano amefika dar, kilichonishangaza na kunivuruga kabisa ni pale aliposema kwamba yule dogo sahivi ana pesa ile mbaya kwamba kanunua gari mbili ameoa na anaishi kwake.

Hapo nilianza kujiuliza kwani huyu dogo yeye anatafutaje pesa mpaka awashinde ndugu zangu ambao wanamda mrefu hapa mjini, wakati tunarudi gheto nilimuuliza bro kuhusu yule dogo ambaye mjomba alimuongelea nikamuuliza kwanini yeye amefanikiwa haraka? alichonijibu aliniambia mdogo wangu katika maisha uvumilivu ni kitu cha msingi sana katika utafutaji unaponiona hapa kuna watu nimewakuta hapa mjini ila wananiona mimi nina maisha mazuri sana.

Baada ya miaka sasa nimekuja kugundua kwamba katika maisha unatakiwa usimame wewe kama wewe na usiangalie mwenzio ana nini ila tu kila unachokiona ukakitamani basi kikupe hamasa ya kupambana na kukipata, ila usiumize kichwa chako kujiuliza kwamba huyu mtu kakipataje and kwanini kapata kirahisi Mungu amempangia kila mtu riziki yake kwa wakati wake so unapoona mwenzio kapata basi usiumie endelea kuweka effort mana inawezekana siku ukipata yule aliyekutamgulia kupata akawa hana kitu kwa wakati huo.

Vijana tujiamini na tusikatishwe tamaa na watu kwa kuangalia kile walicho nacho na kujiona kama hatutokuja kupata kile walicho nacho maisha ni duara ambalo huwezi jua nani wa kwanza na nani wa mwisho, wa kwanza leo anaweza kua wa mwisho kesho.

Wakati niko darasa la tano jilani yetu alimnunulia kiatu kizuri sana mdogo wake ambaye nilikua nasoma naye darasa moja siku nilienda kutembea kwao yule jamaaa alinikebehi kwa kuniambia kwamba ni vigumu mimi kumiliki kiatu kama kile ambacho kwa kipindi kile ilikua km elfu 20 , sikuwahi kuwaza wala kuumia kwa ile kauri ila niliweka nguvu ya kupambana lakini leo yule jama akiona style ya maisha yangu kwa sasa anaona aibu sana. Lakini sioni kama alinikosea ila alinipa hasira ya kupambana huku nikijua sina mtu wa kumtegemea kunipa msaada.

vijana tujiamini wala tusikate tamaa haijalishi umetafuta mafanikio kwa miaka mingapi nakusihi usikate tamaaa, acha watu wakuzalau wengine watasema unahonga sana ila usikate tamaaa hii dunia kila mtu kazaliwa kivyake na atakufa kivyake so haina sababu ya kumwonea aibu mtu simama wewe kama wewe maisha yataenda kwa mda ambao Mungu kakujalia kuishi katika huu ulimwengu.
 
Mkuu huku ni kupeana moyo tu, ukweli utabaki pale pale, makosa madogo madogo kwenye maisha ndio yanaeudisha watafutaji wengi nyuma

Mfano kwa kijana, usitafute mtoto kabla hujasimama vizuri itaweza kupotezea muda na nguvu zako nyingi sana mwishowe utajuta tu

Mimi natofautiana na wewe hapo pa kutoangalia kwanini huyu kafanikiwa haraka, binafsi naona ni lazima mtu ujiulize na kuumiza kuchwa kwanini mtu akukute mahali na akupite kimaendeleo?

Habari za kusema kila mtu ana riziki yake ni za kimasikini sana nadhani badala ya kusema kila mtu ana riziki yake tusrme kila mtu kapewa masaa 24 yakupambana kwa siku.

Kaka na mjomba yako labda walikuwa wameshajikatia tamaa, Mkuu maisha ni kupambana na kujilinganisha ma walio juu yako

Ila kikubwa usiwe na dharau wala kebehi kwa watu wote, ishi kwa nidhamu, adabu na kupambana utaona mafanikio yanakuja
 
Maisha..... noma sana hii kitu... kuna watu wamezaliwa hizi shida ndogo ndogo hawazijui kabisaa na sisi wengine tumezaliwa kupambana kwa ajili ya vizazi vyetu

Bahati.... kukomaa kutafuta...

Tunaweza kupata pesa au tusipate kabisa ila lazma tuishi to the fullest....

Lets enjoy the ride
 
Back
Top Bottom