Maisha yanachosha sana

Maisha yanachosha sana

boyson onlye

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2015
Posts
1,109
Reaction score
1,398
Nawasalimu,

Kuna ile Hasira iliyoko ndani yangu ya mafanikio kuna yale mawazo yaliyoko katika ubongo wangu wa namna ya kupata mafanikio, kila nikijaribu nafanikiwaje sioni njia, unakata tamaa asubuhi unajipa moyo labda leo itakuwa siku ya furaha, lakini wapi ukipita barabara unajiuliza mtu amewezaje kupata pesa mpaka akanunua pikipiki mwingine amewezaje kupata pesa mpaka akanunua gari na huyu anapataje pesa ya kujenga unakaa unafikiria inakatisha tamaa.

Unadaiwa na watu wako wote wa karibu unaona kabisa upendo wa ndugu umepungua unajihisi wewe ni binadamu usiye na akili duniani maana unashindwa kufikiria njia ya kupata pesa kama wengine wanavyopata, unaishi mwenyewe hakuna kijana mtu wa makamo hata Mzee wa kukutia moyo na kukushauri, unajihisi mpweke dunia imekuelemea, ukienda kwenye Nyumba za ibada unaona wenzako wanaenda kutoa sadaka wewe unashindwa hata kunyanyuka, unaona namna ambavyo wana ahidi michango mikubwa na mafungu ya kumi ni mamilioni ila unashindwa kutoa elfu moja maisha yanachosha.

Washikaji wanashindwa kukuonyesha hata njia au kukupa madili unaachwa na mchumba kisa unaonekana huna future (angejua yaliko kichwani) hakika asingewaza hayo yote.

Maisha yanachosha umejitahidi kusoma na mpaka sasa yule uliyemzidi elimu amepata mpenyo wa pesa ila ww huna chochote cha kuuza ukiwa na shida, Maswali kichwani hayaishi nifanye nini, nipataje pesa, nitakuwaje tajiri, nitaishi hivi mpaka lini? Nitakuja kuwa na familia siku moja itaishije kama hali yenyewe ndio hii.

Akili imechoka moyo umeondoa tumaini mbili huna nguvu, unatamani kuzima simu maana ukipigiwa simu ni mtu anakumbusha Deni lake.

Maisha yanachosha
 
Amua tu kuondoa hiyo dhana yako: "Maisha yanachosha..." na kuibadilisha kuanzia kwenye mawazo yako na kufikiri pia kusema: "Maisha yanafurahisha sana..." ikiambatana na utendaji sahihi na kuwa na mtazamo chanja kwa mambo yote.

Pia ujue kuna ulimwengu wa roho na ndio wenye nguvu zaidi ya ulimwengu wa mwili, utumie vyema utaona utamu wa maisha. Lakini usimtumainie shetani na watu wake, bali weka nguvu za Mungu aliye hai zifanye kazi kwenye maisha yako nawe utaona utamu wa maisha.
 
Bora umejua kuna kusali safi sana

Maisha hayafanani
Kila mtu ana mkondo wake wa riziki
Usijarb hata mara 1 kupata ukweli wa mafanikio ya mtu

Unapo fanya biashara acha kupiga hesabu kali sana na za faida ya haraka.

Chagua kundi la watu la kuongea nao jaribu kusikia changamoto zao na ujitahd kutafuta utatuzi.

Jiweke kwenye vikundi vya hisa (vikoba) ili vikupe hamasa ya kutafuta iwe kama deni
 
Nawasalimu

Kuna ile Hasira iliyoko ndani yangu ya mafanikio kuna yale mawazo yaliyoko katika ubongo wangu wa namna ya kupata mafanikio, kila nikijaribu nafanikiwaje sioni njia, unakata tamaa asubuhi unajipa moyo labda leo itakuwa siku ya furaha, lakini wapi ukipita barabara unajiuliza mtu amewezaje kupata pesa mpaka akanunua pikipiki mwingine amewezaje kupata pesa mpaka akanunua gari na huyu anapataje pesa ya kujenga unakaa unafikiria inakatisha tamaa

Unadaiwa na watu wako wote wa karibu unaona kabisa upendo wa ndugu umepungua unajihisi wewe ni binadamu usiye na akili duniani maana unashindwa kufikiria njia ya kupata pesa kama wengine wanavyopata, unaishi mwenyewe hakuna kijana mtu wa makamo hata Mzee wa kukutia moyo na kukushauri, unajihisi mpweke dunia imekuelemea, ukienda kwenye Nyumba za ibada unaona wenzako wanaenda kutoa sadaka wewe unashindwa hata kunyanyuka, unaona namna ambavyo wana ahidi michango mikubwa na mafungu ya kumi ni mamilioni ila unashindwa kutoa elfu moja maisha yanachosha

Washikaji wanashindwa kukuonyesha hata njia au kukupa madili unaachwa na mchumba kisa unaonekana huna future (angejua yaliko kichwani) hakika asingewaza hayo yote

Maisha yanachosha umejitahidi kusoma na mpaka sasa yule uliyemzidi elimu amepata mpenyo wa pesa ila ww huna chochote cha kuuza ukiwa na shida, Maswali kichwani hayaishi nifanye nini, nipataje pesa, nitakuwaje tajiri, nitaishi hivi mpaka lini? Nitakuja kuwa na familia siku moja itaishije kama Hali yenyewe ndio hii

Akili imechoka moyo umeondoa tumaini mbili huna nguvu, unatamani kuzima simu maana ukipigiwa simu ni mtu anakumbusha Deni lake,

Maisha yanachosha
Kufikiri wenye pesa wote wana akili zaidi kuliko wewe ni kujiumiza bure tu.

Kuna watu wana pesa kwa sababu wana mazingira ya kupata pesa. Ndiyo maana Tanzania, to my knowledge, ina bilionea (in US dollars terms) mmoja na Marekani inao wengi tu.

Yani hapo mtu kuzaliwa Tanzania na mwingine kuzaliwa Marekani tu, yule aliyezaliwa Marekani nafasi zake za kuwa bilionea zinakuwa juu zaidi ya aliyezaliwa Tanzania.

Sasa wewe mazingira yako yakoje na unaojilinganisha nao wakoje?

Pia kuna watu wamepata pesa kwa kufanya vitu haramu kama kujiuza miili yao au kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Hawa pengine hawajakuzidi akili, wamekuzidi tamaa ya pesa na maadili mabaya. Unataka kushindana nao kwenye ligi ya maadili mabaya?

Kuna watu wamepata pesa kwa bahati. Wamekuwepo sehemu sahihi, kwa wakati sahihi. Hii kama inarudi kule kwenye mazingira lakini ni pana zaidi. Kuna watu wanashinda bahati nasibu, au wanajiingiza katika biashara nzuri si kwa kuwa wana akili na kupanga vizuri, bali kwa bahati tu, hawa ukiumia kwamba wamekuzidi akili utajiumiza bure tu.

Kitu muhimu ni kujipanga upate maendeleo unayoyataka kwa kujilinganisha vizuri na vinavyostahili bila kuumia kwa sababu ya maendeleo ya wengine.

Ukiumia sana kwa sababu ya maendeleo ya wengine unaweza kuwadhuru wao bila wewe kufaidika.
 
Hapa tusiwe ma "motivational speakers", hiko ulichoandika asimilia kubwa ya vijana tumepitia,tutapitia na tunapitia

Na hapo ulipo huwezi kujitoa wewe mwenyewe,ni UONGO
Hii ni siri niliyoanza kujifunza,unahitaji pesa,sawa?

Hakuna anayeweza kukupa pesa yake bure,eti kwa kumuelezea tu matatizo yako,probability ya watu kama hao ni almost zero

Hivi umeshawahi kujiuliza watu wanatoaje pesa?
Wape kitu kinachoongeza "value" kwenye maisha yao,njoo na bidhaa au idea yenye uwezo wa kutengeneza value kwenye maisha yao

Assume una Tsh 0.00,ila una ubongo
Fikiria kitu gani ukinambia Mimi kwenye Tsh 5,000 mkononi kitanifanya nikupe Tsh 1,000 yangu

Njoo na wazo au kitu kitakacho nipa mimi mwenye Tsh 5,000 value ya Tsh 3,000 halafu niuzie hiko kitu au hilo wazo kwa Tsh 2,000

Hapo tutakua tumetengeneza Tsh 1,000 out of nothing, na kesho nitawambia wezangu wenye Tsh 5,000 na zaidi kuhusu wewe

Huna pesa,usilalamike na kukataa tamaa,hii dunia haina huruma
Ndio maana hata binadam alitengeneza "After Life" kwa ajiri yake tu,ushawahi jiuliza "Sokwe" wakifa wanaenda wapi?

Jifunze kutengeneza pesa out of nothing, jifunze kutengeneza kitu chenye "value"

Jifunze valuable skills,kuwa best kwenye hio skill
Watu watakupa pesa tu
 
Ndo umpe sasa ideas za kutengeneza pesa out of nothing..maana hapo tatizo ndo lilipo
 
Ndo umpe sasa ideas za kutengeneza pesa out of nothing..maana hapo tatizo ndo lilipo
Unaweza kujifunza jinsi gani ya kutengeneza idea itakayo tengeneza thamani/value

Ila sio kupewa tu hizo idea,
Atazame wapi kuna malalamiko,hapo ndipo kuna fursa

Halafu aje na jawabu lake kuhusu namna ambayo anaweza kutumia fursa iliyopo kwa kuondoa hayo malalamiko

Hilo jawabu au idea atakayo kuja nayo ndiyo itakayo mpa pesa kwa kuwa imetatua malalamiko yaliyopo na kuweka value kwa walalamikaji

Kama hilo jawabu lipo ndani ya skill alizonazo ni vyema,kama linahitaji skill mpya ajifunze au atafute wenye hizo skills

Kama jawabu lake linahitaji pesa ili likamilike,atoke kwenye "comfort zone" yake na kutafuta watu atakao washawishi kufadhili jawabu au idea yake as long as watafaidika

Ni hivyo
 
Life isn't fair.

Acha kuangalia wengine na acha kujifananisha nao au subiri kufa kwa stress.
Kila mtu kazaliwa peke yake na atapita njia yake na atazikwa peke yake.

Hatua ya kwanza anza na kufuta Instagram kwenye phone yako.

NB: au utakufa kwa stress.
 
Hapa tusiwe ma "motivational speakers", hiko ulichoandika asimilia kubwa ya vijana tumepitia,tutapitia na tunapitia

Na hapo ulipo huwezi kujitoa wewe mwenyewe,ni UONGO
Hii ni siri niliyoanza kujifunza,unahitaji pesa,sawa?

Hakuna anayeweza kukupa pesa yake bure,eti kwa kumuelezea tu matatizo yako,probability ya watu kama hao ni almost zero

Hivi umeshawahi kujiuliza watu wanatoaje pesa?
Wape kitu kinachoongeza "value" kwenye maisha yao,njoo na bidhaa au idea yenye uwezo wa kutengeneza value kwenye maisha yao

Assume una Tsh 0.00,ila una ubongo
Fikiria kitu gani ukinambia Mimi kwenye Tsh 5,000 mkononi kitanifanya nikupe Tsh 1,000 yangu

Njoo na wazo au kitu kitakacho nipa mimi mwenye Tsh 5,000 value ya Tsh 3,000 halafu niuzie hiko kitu au hilo wazo kwa Tsh 2,000

Hapo tutakua tumetengeneza Tsh 1,000 out of nothing, na kesho nitawambia wezangu wenye Tsh 5,000 na zaidi kuhusu wewe

Huna pesa,usilalamike na kukataa tamaa,hii dunia haina huruma
Ndio maana hata binadam alitengeneza "After Life" kwa ajiri yake tu,ushawahi jiuliza "Sokwe" wakifa wanaenda wapi?

Jifunze kutengeneza pesa out of nothing, jifunze kutengeneza kitu chenye "value"

Jifunze valuable skills,kuwa best kwenye hio skill
Watu watakupa pesa tu

Labda nikikuwa nahitaji hii kitu mkuu umeelewa nilichokiandika nashukuru
 
Unaweza kujifunza jinsi gani ya kutengeneza idea itakayo tengeneza thamani/value

Ila sio kupewa tu hizo idea,
Atazame wapi kuna malalamiko,hapo ndipo kuna fursa

Halafu aje na jawabu lake kuhusu namna ambayo anaweza kutumia fursa iliyopo kwa kuondoa hayo malalamiko

Hilo jawabu au idea atakayo kuja nayo ndiyo itakayo mpa pesa kwa kuwa imetatua malalamiko yaliyopo na kuweka value kwa walalamikaji

Kama hilo jawabu lipo ndani ya skill alizonazo ni vyema,kama linahitaji skill mpya ajifunze au atafute wenye hizo skills

Kama jawabu lake linahitaji pesa ili likamilike,atoke kwenye "comfort zone" yake na kutafuta watu atakao washawishi kufadhili jawabu au idea yake as long as watafaidika

Ni hivyo
Sio rahisi kihivyo au kila mtu mwenye ideas angekuwa millionaire.

Kwa africa haya mambo ni 40% reality na 60% fantasy.
 
Life isn't fair.

Acha kuangalia wengine na acha kujifananisha nao au subiri kufa kwa stress.
Kila mtu kazaliwa peke yake na atapita njia yake na atazikwa peke yake.

Hatua ya kwanza anza na kufuta Instagram kwenye phone yako.

NB: au utakufa kwa stress.
Umeongea point ya msingi sana. Mtoa mada anatakiwa kuacha kuangalia maisha ya wengine! Kila mtu ana siri ya mafanikio yake. Unaweza ukamuona mtu anaendesha gari, kumbe ni la mkopo tu!!

Muhimu anatakiwa atambue siku zote maisha ni vita! Hivyo ni lazima kupambana mwanzo mwisho! Asipo pambana, maisha yatamchosha kweli!!!
 
Back
Top Bottom