Maisha yanachosha sana

Maisha yanachosha sana

Sio rahisi kihivyo au kila mtu mwenye ideas angekuwa millionaire.

Kwa africa haya mambo ni 40% reality na 60% fantasy.
Sio kila idea inaweza kutengeneza value
Njia ya kwanza ni kutambua fursa kwa kutambua wapi kuna malalamiko?,kivipi unaweza rahisisha kazi au maisha?,kivipi utafanya watu waburudike?,

Ungeelewa nini maana ya neno "value" ingekua rahisi

Halafu kuwa na idea ni jambo moja,na kulikamilisha na jambo jingine
 
Amua tu kuondoa hiyo dhana yako: "Maisha yanachosha..." na kuibadilisha kuanzia kwenye mawazo yako na kufikiri pia kusema: "Maisha yanafurahisha sana..." ikiambatana na utendaji sahihi na kuwa na mtazamo chanja kwa mambo yote.

Pia ujue kuna ulimwengu wa roho na ndio wenye nguvu zaidi ya ulimwengu wa mwili, utumie vyema utaona utamu wa maisha. Lakini usimtumainie shetani na watu wake, bali weka nguvu za Mungu aliye hai zifanye kazi kwenye maisha yako nawe utaona utamu wa maisha.
Naona kuna logic
 
Hapa tusiwe ma "motivational speakers", hiko ulichoandika asimilia kubwa ya vijana tumepitia,tutapitia na tunapitia

Na hapo ulipo huwezi kujitoa wewe mwenyewe,ni UONGO
Hii ni siri niliyoanza kujifunza,unahitaji pesa,sawa?

Hakuna anayeweza kukupa pesa yake bure,eti kwa kumuelezea tu matatizo yako,probability ya watu kama hao ni almost zero

Hivi umeshawahi kujiuliza watu wanatoaje pesa?
Wape kitu kinachoongeza "value" kwenye maisha yao,njoo na bidhaa au idea yenye uwezo wa kutengeneza value kwenye maisha yao

Assume una Tsh 0.00,ila una ubongo
Fikiria kitu gani ukinambia Mimi kwenye Tsh 5,000 mkononi kitanifanya nikupe Tsh 1,000 yangu

Njoo na wazo au kitu kitakacho nipa mimi mwenye Tsh 5,000 value ya Tsh 3,000 halafu niuzie hiko kitu au hilo wazo kwa Tsh 2,000

Hapo tutakua tumetengeneza Tsh 1,000 out of nothing, na kesho nitawambia wezangu wenye Tsh 5,000 na zaidi kuhusu wewe

Huna pesa,usilalamike na kukataa tamaa,hii dunia haina huruma
Ndio maana hata binadam alitengeneza "After Life" kwa ajiri yake tu,ushawahi jiuliza "Sokwe" wakifa wanaenda wapi?

Jifunze kutengeneza pesa out of nothing, jifunze kutengeneza kitu chenye "value"

Jifunze valuable skills,kuwa best kwenye hio skill
Watu watakupa pesa tu
Tough Times Never Last But Tough People Do.
In any situation try to be positive rather than to be negative. Then keep you faith in God and Never Give Up. Finally Success will follow. Always try to remember this "Life isn't as nice as you want." Be blessed and the love of God be with you. Amen
 
Jifunze kufurahi kwa kidogo kinachopatikana, vikubwa vinapatikana japo jasho likutoke kwelikweli,

Usisahau katika hustle zako "dunia haina huruma"
 
Mleta uzi umeandika ukiwa n uchungu mwingi na kukata tamaa. Pole sana Pambana kidogo utakachopata ndio halali yako, ikibidi hama ulipo hamia pengine ili isikuwie vigumu kufanikisha.

Ila kusema kweli Kama hufanikiwi Maisha yanachosha wakati mwingine,japo hatutakiwi kukata tamaa!!
 
Ungeelewa nini maana ya neno "value" ingekua rahisi
Naelewa.
Halafu kuwa na idea ni jambo moja,na kulikamilisha na jambo jingine
Utekelezaji wa Idea unahitaji supportive environment ili idea iweze perform inavyotakiwa.

Huku africa unaweza ukawa na idea itakayoleta faida kwako na kwa jamii nzima ila mazingira yatakuangusha hata kama uwezo wa kutekeleza idea yako upo.

Ila kwa idea hiyohiyo ukiwa marekani ingeweza perform vilivyo kutokana na mazingira yake yalivyo'supportive.

Mazingira ya tanzania kwa asilimia kubwa siyo supportive kwa mafanikio wanayoota vijana wengi.
 
Dah....
c2efdd77a02515ac4f4b968cae8846fe.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikwambie tu pesa kubwa inaletwa na pesa ndogo. Weka vyeti ndani Piga kazi yoyote mkuu wewe kajichanganye stand kuu hapo ulipo unga unga.

Huko ndiko utakutana na connection, amini utavyopiga izo dili wewe ni tofauti sana na darasa la 7.

Kumbuka pesa ndogo ndio inaleta pesa kubwa. Komaa
 
Sio rahisi kihivyo au kila mtu mwenye ideas angekuwa millionaire.

Kwa africa haya mambo ni 40% reality na 60% fantasy.

40% ni kubwa sana shusha shusha hadi 10% reality mkuu alafu 90% fantasy. Haya mambo sio rahisi kutekelezeka kabisaaa. Na ukweli mchungu ni kuwa PESA INAFUATA PESA ILIPO

Ukiwa na idea inatakiwa uwe na pesa yakukufikisha kwa hao utakaowapa iyo idea wakusapoti, lazima uwe na pesa ya kununua kahawa kikombe 6,000 restauranti ili udiscuss idea na vibopa vibopa hawakai kijiweni wana maeneo yao

Sasa watu wengi huu ukweli hawaambiwi wanabaki kukariri tu ooh ukiwa na idea ukipelekea watu utapewa pesa, nani kasemaaa!!?
 
Hiyo ni dhana potofu.

Maisha hayana muda, Maisha hayana wakati.

Maisha hayana mwenyewe.

Maisha hayana ujanja.

Maisha hayana mjanja, Maisha hayana FALA.

Maisha hayana mkubwa, Maisha hayana mdogo.

Maisha hayana kanuni.

Maisha yanabadilika muda wowote.

Wewe endelea kupambana, mambo yatajipa.

Achana na kufikiria Maisha ya watu, wewe ishi Maisha yako.

Jiamini, usikate tamaa.

Utafikia Malengo yako
 
Yaani unawaza wakati umelala unaangalia juu yaa paa la chumba chako,wakati unaowawazia wanapiga kazi kwenye jua kali pole sana mtoto wa mama kama hata kubeba zege huwezi huku ukijivunia elimu yako inayokudanganya
 
Nawasalimu,

Kuna ile Hasira iliyoko ndani yangu ya mafanikio kuna yale mawazo yaliyoko katika ubongo wangu wa namna ya kupata mafanikio, kila nikijaribu nafanikiwaje sioni njia, unakata tamaa asubuhi unajipa moyo labda leo itakuwa siku ya furaha, lakini wapi ukipita barabara unajiuliza mtu amewezaje kupata pesa mpaka akanunua pikipiki mwingine amewezaje kupata pesa mpaka akanunua gari na huyu anapataje pesa ya kujenga unakaa unafikiria inakatisha tamaa.

Unadaiwa na watu wako wote wa karibu unaona kabisa upendo wa ndugu umepungua unajihisi wewe ni binadamu usiye na akili duniani maana unashindwa kufikiria njia ya kupata pesa kama wengine wanavyopata, unaishi mwenyewe hakuna kijana mtu wa makamo hata Mzee wa kukutia moyo na kukushauri, unajihisi mpweke dunia imekuelemea, ukienda kwenye Nyumba za ibada unaona wenzako wanaenda kutoa sadaka wewe unashindwa hata kunyanyuka, unaona namna ambavyo wana ahidi michango mikubwa na mafungu ya kumi ni mamilioni ila unashindwa kutoa elfu moja maisha yanachosha.

Washikaji wanashindwa kukuonyesha hata njia au kukupa madili unaachwa na mchumba kisa unaonekana huna future (angejua yaliko kichwani) hakika asingewaza hayo yote.

Maisha yanachosha umejitahidi kusoma na mpaka sasa yule uliyemzidi elimu amepata mpenyo wa pesa ila ww huna chochote cha kuuza ukiwa na shida, Maswali kichwani hayaishi nifanye nini, nipataje pesa, nitakuwaje tajiri, nitaishi hivi mpaka lini? Nitakuja kuwa na familia siku moja itaishije kama hali yenyewe ndio hii.

Akili imechoka moyo umeondoa tumaini mbili huna nguvu, unatamani kuzima simu maana ukipigiwa simu ni mtu anakumbusha Deni lake.

Maisha yanachosha
Ni kweli yanachosha lakini ni ajabu sana ! Hapo hapo katika Hali uliyonayo wewe ni mwenye nguvu Sana Kama unaweza kuamka asubuhi na kwenda kuchukua carton ya maji kuuza kwa abiria wanaopita barabarani kwenye mabasi.
Wengine hawawezi kwakuwa wanasumbuliwa na matatizo mbali mbali ya kiafya na hawawezi. Kikubwa aliyenacho asimsahau kabisa asiye nacho na mwenye afya azidi kuombea wenye magonjwa wapone na kuwapa faraja.

Kunawakati tunapitia kwenye magumu sio kwamba tutakuwa kwenye magumu hayo daima la. Ni ili tunapofanikiwa tujue hisia za wale walio katika magumu ambayo nasi tuliyapitia na tuwe sehemu ya msaada kwao.
 
Back
Top Bottom