Maisha ya wakazi wa Dar es Salaam ni magumu sana

mapesa yamejaa

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
1,412
3,403
Baadhi ya maeneo Dar es salamu wanaishi maisha magumu sana hasa wilaya ya Ubungo hasahasa jimbo la kibamba. Ukifika maeneo haya ya jimbo la kibamba kama kule kanisa katoliki msakuzi, kwa lubaba, lipelanya dolphin, mpiji magoe,mbezi misumi n.k maisha ya watu wa kule ni sawa na maisha ya watu walioishi miaka ya 1800.

Yaani sehemu kubwa ya jimbo la kibamba hakuna maji. Wananchi wanavuna maji ya mvua inaponyesha na msimu wa masika ukipita kila mtu atajua kivyake atakapopata maji. Kama ni kufuata kimara au huko mbali yalikoishia maji ya dawasa. Dawasa wao hawana muda wa kupeleja maji huko.

Barabara nayo ni shida tupu. Ukitokea mbezi stand kuu kuelekea mpiji au njia panda ya Goba kwenda Mbezi Misumi na Msakuzi ukiwa na gari yako ni mwendo wa kurukaruka kwenye gari kutokana na mashimo makubwa ya barabarani hadi mwisho wa safari.

Hospitali jimbo zima hakuna. Ukiumwa inabidi uende hosipitali za binafsi au uende SINZA zaidi ya km30.

Nimetoka zangu mikoani kuja kumtembelea ndugu yangu lakini yamenishangaza sana maisha ya huku maana ni zaidi ya jehanamu.

Nimejiuliza maswali mengi, hivi wanaowasifu viongizi kama waziri wa maji, miundombinu na afya kwa watu wa jimbo la Kibamba wanawaelewa kweli?

Poleni sana wakazi wa Dar es salaamu. Serikali wasaidieni watu wa jimbo la kibamba wamechoka kusikia kila taarifa ya CAG kuwa Tanroad wamefisadi zaidi ya trillioni moja ambapo hiyo ingepelekwa huko ingemaliza changamoto za huko.
 
Utashangaa jimbo lenye matatizo namna hiyo linakuwa na Mbunge ambaye hazungumzii shida za wananchi kule Bungeni bali anakwenda kuwa chawa kwa kupendekeza station ya SGR ipewe sina la Samia!!!
Na wanasema utefu wa kamba 😬😬😬😬😬😬😬😬
 
Maisha yako kama magumu don't generalise wengine tunaishi mbwa wewe
Nimeongelea watu wa kibamba,kama na wewe unaishi kibamba unamaisha magumu kwa miundombinu ya kule.halafu mimi sijaongelea kipato cha mtu bali huduma za kijamii mbwa we
 
Kuna hospital kubwa sana imejengwa pale mabwepande...ila naskia mkuu wa wilaya aligoma kuizindua kutokana na ubovu wa Barabara
 
Nimeongelea watu wa kibamba,kama na wewe unaishi kibamba unamaisha magumu kwa miundombinu ya kule.halafu mimi sijaongelea kipato cha mtu bali huduma za kijamii mbwa we
Hao ndo wanaosoma heading tu wanarukia kucomment
 
Back
Top Bottom