Mkuu wa Kibiti
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 777
- 1,140
Niliandika hii kitu muda mrefu ulio pita,ila kutokana na yanayo endelea ya wenye nguvu kutamani kula akiba ya wanyonge imenikumbusha kupandisha bandiko hili linalo kwenda kwa mtindo wa hadithi simulizi ili pengine wenye macho wataona na wenye masikio wataelewa.
Maisha yalinipelekea kupata mwenzi mpya...ndio ni mwemzi mpya kabisa maishani ni mpenzi wangu mshaufu Njaa.Licha ya nafsi yangu kuwa na woga mno mwanzoni,kadili tulivyo zoeana na kujuana akawa mwenzi mwenye kufariji.Mpenzi njaa...aaah!Niseme nini kwako!?Japo wakati mwingine kwa hasira kuu aliniadhibu,nilijifunza kuchukuliana naye kwa upole.
Tofauti na wenzi wengine ambao mara mpandapo kitandani mashindano huanza;mwenzi huyu ni kinyume.Ni mtulivu mwenye ubaridi asiye gubu,hata tunapo jifunika shuka kwa upendo,daima utahisi mguso wake.Mke wangu wa kwanza kakimbia na watoto;eti kwa hofu ya huyu mpenzi wangu mpya ila nadhani ni wivu tu.Kumekuwa na kelele nyingi kila upande wakidai eti mwenzi wangu huyu ni 'mbaya'!Hawa nao ni majungu na umbea tu kwani pilipili usoila waliaje ukali wake!?
Daima tumekuwa wapweke na watupu tusio na mashaka yajayo,kwani tumezoea kufarijiana na kuchukuliana kimya hata watu nje yetu wasijue kuwa tupo pamoja.
Mpenzi wangu huyu kanifunza mambo mengi ambayo kabla siku yajua:-1Taabu waipatayo wasio nacho
2.Hisia walizo nazo wasio nacho dhidi ya walio nacho
3.Unafiki wa walionacho dhidi ya wasionacho
4.Utii wa wsionacho kuwaelekea wenye nacho
5.Uvumilivu na utulivu
6.Hatari ya kutafuta faraja kwa njia za mkato na kulazimisha kukwepa hasira za mwenzi huyu;e.i.ulevi,wizi n.k
7.Kuukabili ukweli bila kuogopa ili kupona
8.Kuishinda hofu ya kesho na kitisho cha mauti.
Bila mwenzi huyu haya yote yasinge pata hata nafasi ya kuwa walau msamiati kwenye ubongo wangu lakini mwenzi huyu kanisaidia kuyaonja bila shaka.Upweke ni mbaya ila upweke ni rafiki mzuri ukijua kusema naye.
Sikuonja matamu na machungu tu ya mpenzi huyu,alinifunza pia kuepuka yafuatayo kwa kipindi chote tutakacho kuwa pamoja
1.Ushirikina
2.Kijicho
3.Choyo
4.Ubinafsi
5.Masengenyo
6.Chuki zisizo na sababu kwa wengine.
Wakati unawaza una magumu yamekusonga,fikiri wako wenye magumu yaliyo magumu hata tu kufikiria.Hujui kwakuwa hawaja sema kama nao wana magumu pangine ungeyasikia ungejiona uko peponi.Kila mtu ni tajiri kwa kadili ya mazingira yake.
Ama kwa hakika mwenzi huyu hakuwa tu mpenzi mzuri bali pia mwalimu mwema sana.Tujiulize ni kwa kiasi gani tuko tayari kuwalisha wenye njaa wasio na kitu chochote?Unafiki unawala wenye nacho,hujiona wana haki huku wakipepesa kuelekea haki za wengine bila kuambatana na wajibu wao wa kufaidiana ili kujenga amani mioyoni.
"UKITAKA AMANI NYOOSHA MKONO KWA MASIKINI-St Yohanes paulus]]