Maisha ya Papa Francis

Maisha ya Papa Francis

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,432
Papa FRANCIS ASEMA KUWA HAJAWAHI KUTAZAMA TV KWA MIAKA 25 sasa.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, amesema kuwa hajawahi kutazama runinga kwa miaka 25 sasa. Papa Prancis ambaye amewatamausha wachanganuzi wa kanisa hilo kwa kususia maisha ya kifahari katika makao makuu ya kanisa Vatican alisema alitizama runinga mara ya mwisho tarehe 15 mwezi julai mwaka wa 1990.

Alikoma kutizama runinga baada ya kumuahidi maria mtakatifu kuwa angekoma kushiriki uraibu huo.

Isitoshe raia huyo wa Argentina amesema kuwa hatumii mtandao wa intaneti. Na akitaka kupata habari za kimataifa , Papa anasema kuwa huwa anatenga dakika 10 tu ya muda wake kusoma gazeti la kiitaliano. Papa Francis vilevile anafuatilia habari za klabu yake maarufu huko Argentina kupitia kwa wahudumu wake ambao humsimulia yanayojiri.

Je unaweza kukaa mbali na Runinga yako Simu yako ama mtandao wa Intanet japo kwa siku moja ?
 
hahahahaha, papa anatuuzia chai hapa... mjinga ndiye atakaye amini ....
 
hahahahaha, papa anatuuzia chai hapa... mjinga ndiye atakaye amini ....

Wewe ndiyo mjinga!,ktk Kanisa Katoliki hili jambo mbona ni la Kawaida!!,Wapo watu ambao huwa wanaamua kuishi maisha ya Upweke kwaajili ya Kujitafakarisha juu ya mambo yanayomhusu Mungu,na hii huwa ni maisha yao yote.Tena wapo walio wahi kukaa mapangoni kwaajili ya kujitenga na Malimwengu ili wasiingie ktk vishawishi vya kutenda dhambi watu hao waliitwa WAEREMITE,huko walisoma neno la Mungu,Tafakari na Sala tu!,Nenda Songea kule kuna Watawa wanaitwa WAKILALA,hao ndio hukaa ndani tu pasipo kutoka nje huko hufanya SALA na Kutafakari neno la Mungu,wao si watu wa kuchangamana na malimwengu,Hata ndugu ukienda kumtembelea mnaonana naye dirishani tu!,Hawa hutoka nje mara mojamoja tu!,Wanafanya hivi kwaajili ya kujinyima Starehe na Anasa za dunia.
 
Ni papa wa majini au nchi kavu

Acha dharau!,dharau haifai nani anaidharau au kubeza Imani yako?,basi tuheshimiane,heshima ni kitu bora sana,hata km Kitu fulani au Imani fulani hauiamini basi waache wanaoamini waamini wala usianze dharau na kejeli,tukisema tuanze kudharauliana hakika hatutafika mbali.
 
Papa aache uongo, kwa dunia ya sasa hilo haliwezekani, hasa kwa mtu kama yeye, TV hadi barabarani unazikwepaje, labda awe anavaa miwani ya mbao.
 
well done tusikashifiane kidini hakuna alikufa akarudi akatupa majibu mungu ni dini gani, basi tumheshimu pope kwa nadhiri aliyojiwekea, ni kitu cha kawaida kwa kanisa katoliki kuna masisita wao nadiri yao ni kutokufanya mapenzi, wapo wakapuchini wao hutembea peku, so usishangae pope kutokuangalia tv ni zoezi dogo sana
 
Papa aache uongo, kwa dunia ya sasa hilo haliwezekani, hasa kwa mtu kama yeye, TV hadi barabarani unazikwepaje, labda awe anavaa miwani ya mbao.

Kwako wewe ni kweli haiwezekani lkn Kwa Upande wa Kanisa Katoliki hilo ni jambo la kawaida kabisa,endelea kushangaa na sisi tunakushangaa wewe unavyoshangaa kitu kisichoshangaza.
 
well done tusikashifiane kidini hakuna alikufa akarudi akatupa majibu mungu ni dini gani, basi tumheshimu pope kwa nadhiri aliyojiwekea, ni kitu cha kawaida kwa kanisa katoliki kuna masisita wao nadiri yao ni kutokufanya mapenzi, wapo wakapuchini wao hutembea peku, so usishangae pope kutokuangalia tv ni zoezi dogo sana

Amina!,tupo pamoja mkuu.
 
mkuu CHAULA RICH

Wewe ndiyo mjinga!,ktk Kanisa Katoliki hili jambo mbona ni la Kawaida!!,Wapo watu ambao huwa wanaamua kuishi maisha ya Upweke kwaajili ya Kujitafakarisha juu ya mambo yanayomhusu Mungu,na hii huwa ni maisha yao yote


Kwa karne ya sasa ya utandawazi hakuna hao watu tena......


Tena wapo walio wahi kukaa mapangoni kwaajili ya kujitenga na Malimwengu ili wasiingie ktk vishawishi vya kutenda dhambi watu hao waliitwa WAEREMITE,huko walisoma neno la Mungu,Tafakari na Sala tu!


key word "WALIOWAHI"...... sasa hivi hawapo tena watu wanamna hii....

Nenda Songea kule kuna Watawa wanaitwa WAKILALA,hao ndio hukaa ndani tu pasipo kutoka nje huko hufanya SALA na Kutafakari neno la Mungu,wao si watu wa kuchangamana na malimwengu,Hata ndugu ukienda kumtembelea mnaonana naye dirishani tu!

Hizi ni story tu! haiwezekani mtu maisha yote usitoke nje! ..... kuna kitu kinaitwa VITAMIN D ....


Hawa hutoka nje mara mojamoja tu!,Wanafanya hivi kwaajili ya kujinyima Starehe na Anasa za dunia.


kumbe wanatoka!



 
Mkuu Bujibuji

Hebu fafanua misamiati hii ili tuendelee..

Wachanganuzi
Amewatamausha
Uraibu


BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom