Amani Dimile
JF-Expert Member
- Jul 27, 2022
- 243
- 399
Professor John Mordechai Gottman, ni kati ya wanadamu ambao ni ngumu kusahaulika sana kwenye dunia hii hasa katika ulimwengu wa masuala ya ndoa na mahusiano. Alizaliwa tarehe 26 April mwaka 1942. Yeye ni mwanasaikolojia wa kiamerika na Professor katika chuo cha Washington.
Aliamua kufanya utafiti juu ya masuala ya talaka na ndoa, na hatimae akaandika kitabu chake bora sana kinachoitwa 'The Seven principles for making marriage work'. Gottman alishirikiana na watafiti mbali mbali kama Lois Verbrugge na James House wote kutoka katika chuo cha Michigan na kuamua kuchunguza sababu na madhara ya talaka kwenye ndoa mbali mbali.
Gottman aliichukua couples tofauti tofauti zaidi ya 50 na kuwaweka pamoja katika nyumba Moja kubwa (apartment) na kuwachunguza mienendo yao mbali mbali. Lakini pia alifanya utafiti katika ndoa nyingi zilizokwisha vunjika na katika miaka yote ya utafiti Gottman alikuja na majibu kwamba:
Katika asilimia 100 za ndoa zinazofungwa asilimia 67 huishia kwenye talaka, tena ndani ya miaka 7 tu ya mwanzoni. Lakini Gottman, aliendelea kusema kwamba wanandoa walioachana huishi maisha mafupi sana kuliko ambao ndoa zao zina furaha. Akasema tena kwamba, walioachana huwa katika hatari ya kupata magonjwa mbali mbali kutokana na kinga za miili yao huwa hazifanyi kazi sawa sawa tofauti na awali.
Magonjwa hatarishi kama pressure ya damu, msongo wa mawazo, kujitenga na hata hatimae wengine kujiua vyote hutokana na ndoa nyingi zilizovunjika ambazo awali zilikuwa zimebeba matumaini ya mioyo ya watu. Si hivyo tu, Gottman katika kitabu chake cha 'The Seven principles of making marriage work' katika ukurasa nambari 4 anaizungumzia tabia ya wanawake wengi kubaki kwenye ndoa zisizo na amani sababu tu ya mtoto.
Professor Gottman anasema kwamba kujilazimisha kuishi kwenye ndoa isiyo na amani wala furaha sababu tu ya mtoto ni lazima iharibu amani ya nyumba lakini pia inamharibu kisaikolojia mtoto mwenyewe.
Gottman anaelezea sababu na njia za kutatua au kufanya ili ndoa ziweze kudumu. Anatajwa kuwa mtaalamu wa masuala ya ndoa kutokana na utafiti wake uliochukua takribani miaka 40.
Soma vitabu upate maarifa, nitarudi tena kwa ajili ya sisi wanandoa ..