Maisha ya Mlimwengu Boarding: 5

Maisha ya Mlimwengu Boarding: 5

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
228
Reaction score
249
Mchawi mpe sifa zake yule mtoto alikuwa kajaliwa yuko natural na umbo lake zuri la kiafrika, ngozi yake laini na nyororo utadhani haogi maji ya ziwani bali anaoga maji ya Dasani. Tulitembea hatua kama kumi tukiwa tumeshikana mikono baadae nikajipiga moyo konde nikamsimamisha mrembo. Mashallah! yule mtoto hakuwa na hiyana akasimama huku macho yako yameangalia macho yangu. Waswahili wanasema ikawa ni eye contact. Kumbuka huyu mrembo alikuwa kidato cha tatu mimi cha kwanza. Nikajikuta automatocally confidence inapungua kwa mbali huku nikitetemeka ndani kwa ndani. Nikaona siyo issue kama mbwai mbwai nikatoa kauli...Samahani kwani wewe kidato cha ngapi? Akanijibu kuwa yupo kidato cha tatu. Hapo bado hata jina lake sijauliza na simjui anaitwa nani? Ila mtu ambaye angetuona wote angejua labda ni wapenzi kama Romeo na Julieth kumbe hamna kitu. Basi wakati nikijitafutisha maneno ya kumuambia mara ghafla nikaona wanaume wote wa bwiru wanakimbia basi na mimi bila kuuliza kuna nini na mimi nikakimbia. Shule zetu tulikuwa kama nyumbu mmoja akianza kukimbia wote tunakimbia pasipokujua tatizo nini na anayetukimbiza yuko upande gani. Nilikimbia valuvalu breki ya kwanza nilikuwa kwenye mawe kuelekea mnarani nikafika sehemu nikazinda kwenye nyasi. Basi kuna watu tulikuwa tumeongozana wakati wa kukimbia tulipofika ndio tunaanza kuulizana kuna tatizo gani? Kila mtu hajui ila hapo akili yangu bado inamuwazia yule mtoto. Tukiwa bado tunaulizana kuna nini akatokea jamaa mmoja anakimbia akatuambia ni Mchizi Mox. Dah huyu mwalimu wanafunzi walimtunga jina la Mchizi Mox kutokana na ukali wake. Kwa ambaye amepitia Bwiru kwenye zama zake atakuwa anamkumbuka. Kumbe ilikuwa zamu yake pale alitutawanisha watu tuwahi lokoo. Basi kwa lile tukio nilimmind sana kwa kunitemesha tonge ambalo limeishafika mdomoni. Ilikuwa haina namna na yule mrembo sikuweza kumpata tena maana nilikuwa sina wa kumuuliza hata namba yake sina na sikuwahi kumuona tena maisha ya shule ingawa nilijitahidi kuhudhuria matukio yote yanayotukutanisha na shule yao. Iwe joint mass za Ukwata, Assa, Tycs na mambo mengine lakini sikubahatika kumpata. Kama unavyojua ukikaa muda mrefu bila kuonana na huyo mtu unasahau na maisha yanaendelea. Nilikubali matokeo na baadhi ya wenzangu wao walifanikiwa kupata girlfriends kupitia disko hilo. Baada ya wiki wanaanza kutumiana barua na sisi ambao hatuna tunabaki kuangalia tu na kutoa maoni yetu. Kwa wengine ili tuwe sawa tutamponda demu wako kuwa ni mbaya au ni mfupi ilikuwa lazima upate kasoro hata tuseme ana masikio makubwa , mwenye moyo mwepesi alikuwa anamuacha mpenzi wake kwa kufuata maneno yetu. Hivi vitu hata kwenye ndoa vipo usipokuwa na msimamo na maamuzi yako. Shuleni kulikuwa na wapenzi wa vitu mbalimbali kuna watu walikuwa wapenzi wa kabumbu wanatoroka usiku kwenda kuangalia mechi za Epl na Uefa, wengine walikuwa wapenzi wa tamthiliya za kifilipino wanaenda mjini au nyumba za walimu kucheki michezo ya La revancha na Promise kwa kipindi hicho. Wengine walikuwa wameishaathirika na hiyo michezo hivyo wanafuatilia kwa kununua magazeti ya Udaku kama Risasi, Amani na Ijumaa. Maisha ya shule bwana wengine ndio ulevi wao kusikiliza redio na kuimba. Na wengine ndio wanatumia muda wao kwenye uvutaji bangi na unywaji wa pombe kijijini tena gongo. Penye wengi kuna mengi kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wazazi wao ni wanajeshi, hivyo baada ya likizo wanakuja na nguo za kijeshi na wengine walienda vijijini na kula bure kwa mama ntiliye na kuwatisha na sare zao. Hata shuleni wengine walikuwa wanazivaa muda ambao siyo wa darasani hadi ikapelekea walimu kupiga marufuku kukutwa na sare za jeshi. Vizaazaa vilikuwa havikosi shuleni kulikuwa kunatishiana kuwa usiku shuleni kuna vibwengo kwa ambao walikuwa wanaogopa mambo ya uchawi wasingeweza kwenda chooni peke yao ikiwa usiku. Ilikuwa stori za sijui nani kakutana na kibwengo zilikuwa haziishi..mwingine eti kafuatwa na bibi yake darasani usiku wa manane yote hayo yalikuwa ni matukio ya mara kwa mara. Na wengine malaria ziliwapanda kichwani na kuwa vichaa...namkumbuka shemeji yangu bwana Iman naye alishakuwa muhanga wa hilo jambo . Lakini hayo matukio yote hayakufanya tusipende shule yetu au tuendelee na masomo ilichukuliwa kama sehemu ya maisha yetu. Asilimia kubwa ya wanafunzi kwa kipindi chetu tuko shuleni walikuwa wameishabelehe. Wengi wao walitumia njia ya punyeto kama mbadala wa kupunguza mihemko yao. Ukienda bafuni inabidi uwe muangalifu unaweza kuteleza kwa kuanguka chini usipokuwa makini. Walikuwa wana njia nyingi za kupiga punyeto kama kutumia Mafuta , sabuni na wengine walipiga kavu. Unakuta mtu kitandani kwake kafunga neti tatu kwa pamoja unajiuliza huyu anazuia mbu au binadamu?. Hayo ndio maisha ya Boys kuna kipindi zilikuwa kampeni za Ishi mashuleni juu ya matumizi ya kondomu na tuliweza kugawiwa za kutosha, ndio unajiuliza hawa wanatupa hizi kondomu tuzitumie wapi?. Waliojiongeza ndio hivyo walizitumia kwa matumizi binafsi na walikuwa wana chama chao. Penye jumuiya nyingi hakukosi vyama basi kuna vyama viliendelea na vilikuwa na wafuasi kama CHAPUTA ( Chama cha wapiga punyeto Tanzania) ambapo mwenywkiti wake sitamtaja kutokana na madaraka aliyonayo kwa sasa na kingine CHAZATA (Chama cha Wazamiaji Tanzania) hawa ilikuwa kwenye shughuli yeyote ya kishule hata kama haimuhusu ila lazima umkute, niliwahi kukaimu nafasi ya uenyekiti baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kufukuzwa shule. Maisha yalizidi kunoga na wengine waliokuwa malimbukeni sana walifukuzwa mapema sana kama wazungu wanavyosema too much of anything always is harmful. Wengine tulijitahidi kuwa vuguvugu siyo wa moto sana wala baridi sana. Shule zetu za boarding bana kiongozi wa chakula lazima uwe mkubwa aidha kwa kuwa na nguvu nyingi au baunsa. Ilikuwa ukikutwa unadabo chakula basi lazima upigwe mabanzi. Enzi hizo tulimkuta Paul Nonga pamoja na Evarist wakiwa viongozi wa chakula ilikuwa akikuangalia tu kama uko nje ya mstari lazima urudi na ole wako ukutwe unadabo ilikuwa lazima uongee na mizimu ya kwenu. Kuna watu ilikuwa matumbo yao kama shimo bila kunywa vikombe zaidi ya vitatu vya uji hajaridhika na chakula lazima apate sahani zaidi ya mbili. Wote hao walikuwa ni sehemu ya shule. Dunia hadaa ulimwengu shujaa siku nyingine tena ilikuwa jumamosi tukaongozana na rafiki yangu. Kabla hatujafika mjini aliniambia nimsindikize kwa rafiki yake huko Ilemela. Tukaongozana hadi Ilemela kumbe alikuwa ananipeleka kwa marafiki zake, tumefika tu nilikuta watu wapo kijiweni zaidi ya 10 na kila mtu alikuwa busy na shughuli yake. Wengine wanavuta bangi, wengine wananusa gundi, wengine wanakunywa pombe. Basi kufika pale kwanza nilishtuka lakini nikaonyesha kutoshtuka kwa macho. Mwenzangu walikuwa wanamjua wakamchangamkia sana kama kaingia mtu wao wa karibu. Na mimi nikachangamkiwa vilevile basi tukakaa chini. Ikasokotwa bonge la bangi kama la Bob Marley baadae ikawashwa. Nikasikia mmoja anasema kwa sauti kubwa kuwa mwenge huwa hauruki kijiji. Basi nikajisemea moyoni leo ndio arobaini yangu imefika. Ikafikia zamu ya mtu aliyekuwa karibu yangu huku mimi natetemeka kwa ndani. Mara akanigusa begani......
Je Mlimwengu nitachukua hatua gani? Na nini kilitokea?
Tukiwa tunaenda kutimiza miaka 100 tangu Bwiru Boys ianzishwe.
Nitakuwa naeleza matukio niliokutana nayo.
Episode 5
Stay tuned
#mlimwengumimi
#BwiruboysAlumni
#100yearsAnniversary
IMG-20190611-WA0017.jpeg
 
Mwenge haurukagi kijij[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom