Mkuu Jela ni sehemu salama ya kuishi kuliko Mahabusu, Jela Watu wanaheshimiana sana tofauti na Mahabusu, Jela Wafungwa wakitoka kwenye Majukumu yao ya kila siku huwa wanarudi na Mboga Mbadala hususani za Majani then wanakoka moto na kujipikia, Wafungwa kuanzia SAA 10 jioni ni muda wa Michezo kwa wote kasoro wale wenye mahitaji maalum na waliohukumiwa kunyongwa!
Jela ni sehemu pekee ambako unakutana na Wanasheria ambao ukiingia tu unawapa hukumu yako then wanaipitia na kukushauri watakavyoona inafaa, wengi walionewa kwenye hukumu huwa wanashauriwa kukata rufaa na Mara nyingi wanashinda rufaa zao, hao Wafungwa Wanasheria ndio kazi yao hiyo na hawana kazi nyingine.
Wanasheria hao huwa wanakuwepo kwenye Magereza makubwa au kuanzia Magereza ya Mikoa, na ikiwa hakuna atahamishwa kutoka kwenye Magereza mengine.,