Maisha ya Fidel Alejandro Castro Ruz

Maisha ya Fidel Alejandro Castro Ruz

Umewasahau akina Jonas Savimbi na John Garang
Mkuu Janas Savimbi alikuwa ni pandikizi la Marekani huwezi kumuweka kwenye list hii. Vivyo hivyo kwa John garang ambaye alikuwa pandikizi la Warusi. Ndio maana pia sikumtaja mtu kama Patrick Lumumba.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mkuu Janas Savimbi alikuwa ni pandikizi la Marekani huwezi kumuweka kwenye list hii. Vivyo hivyo kwa John garang ambaye alikuwa pandikizi la Warusi. Ndio maana pia sikumtaja mtu kama Patrick Lumumba.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Hakuna kiongozi au kundi la kivita lisilokuwa na mrengo, fikra na tamaduni. Hivyo basi hao uliowataja kuwaita "pandikizi" ni kudhihirisha kwamba una upande ambao ndio mfumo,sera au itikadi unazo zifuata na kuzitukuza
 
Mkuu vile visa vilivotokea wakati Fidel katembelea Tz, ni vya kweli?
 
Huyu mzee namkubali sana,ngoja ni subscribe kwenye hii post nitamsoma vizuri nikipata nafasi
 
sijui kwa nn shule niliyosoma imepewa jina lake "Fidel Castro Secondary School"
 
Marais wa marekani tangu keneddy waliondoka wakamuacha,kuna kipindi alikuja new york kuhuhutubia UN,-katika hoteli aliyofikia CIA wakaenda kuiba uharo wake kwa kudivert lile bomba la choo alichokua anakitumia, wakakinga na kwenda kupima maabara na wakatangaza Fidel ni mgonjwa atakufa ndani ya miezi 6,leo imepita miaka 40,jamaa anadunda tu
 
Duuuh!
Natamani mtu aweke post ya jinsi na namna gani alivyokoswakoswa mara zote hizo 31.
Wapi @ushiboy?

Nimepata kwa English books.
Ngoja nianze kuitafasiri ikuje kwa Swahili, then niweke fully details.
 
Huyu mzee namkubali sana,ngoja ni subscribe kwenye hii post nitamsoma vizuri nikipata nafasi

Fidel Castro, ameingia madarakani mwaka 1959 baada ya mapinduzi ya mwaka huo ambayo yalimuondoa madarakani dikteta Fulgencio Batista na kuwa waziri mkuu wa Cuba mwaka 1961 na baadaye akaghairisha uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na pia kuipinga katiba ya nchi hiyo. Casrto ameiongoza nchi ya Cuba bila kuongozwa na katiba ya nchi hiyo iliyoandikwa mwaka 1940 mpaka mwaka 1976, ambapo taifa hilo lilitunga katiba mpya ambayo iliruhusu ukomo wa upigaji kura wa Cuba. Baadae mwaka huo wa 1976, Casrto alichaguliwa na bunge la nchi hiyo kuwa rais wa nchi ya Cuba.

Baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Cuba, Castro akaanza taratibu kuingoza nchi hiyo katika misingi ya kijamaa, baada ya kubadilisha mifumo ya kijamii na kiuchumi. Alianzisha pia programu mbalimbali zilizolenga kuongeza idadi ya wasomi katika nchi na kugawa huduma bora za afya kwa kila raia.

Mfumo wa siasa za kijamaa wa serikali ya Cuba, uliwafanya wasomi wengi na watu wa fani mbalimbali kuishi uhamishoni. Hali hii ilitokana pia na mfumo wa serikali wa kukamata biashara, kuondoa chaguzi mbalimbali, kuanzisha mfumo wa kijeshi wa kijamii, kuongoza vyombo vya habari pamoja na sera ya elimu, kulipelekea watu wengi wasiopenda mabadiliko kuhamia uhamishoni katika nchi za Uhispania, Mexico, Ufaransa na Marekani.

Katika kipindi cha vita baridi, Casrto alijiingiza katika ujamaa hasa uliokomaa ambao ulikuwa unaongoza na Umoja wa nchi za kijamaa (USSR) ili kuongeza na kuyapa nguvu mapinduzi ya kujikomboa kwa nchi za Amerika ya kusini na afrika. Katika hili Castro na harakati zake za kijamaa walipata upinzani kutoka Marekani, nchi ambayo ilikuwa rafiki mkubwa na mshirika mkubwa wa kibiashara na cuba.

Marekani iliona kuendelea kufanya biashara na nchi ya Cuba isingekuwa jambo jema kwani nchi ya Cuba ilikamata mali za marekani, hivyo wanasiasa wengi wa Marekani waliona siasa za kijamaa za Castro na kujiunga kwake na umoja nchi za Kisovieti ni tishio la usalama kwa Marekani.

Alikotokea Fidel Castro

Fidel Aljandro Castro Ruz, amezaliwa katika kitongoji kikubwa kilichopo karibu na mji wa Birani katika jimbo la Oriente, nchini Cuba, akiwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto saba. Wazazi wa Castro walikuwa ni wahamiaji kutoka nchini Uhispania.

Alianza elimu yake katika shule ya umma iliyopo karibu na mji wa jirani na kwao wa Mayari. Akiwa shuleni hapo Castro aligundulika kuwa ana kipaji cha kusoma na kutokana na hilo Castro akawa anafundishwa binafsi na baadaye akaandikishwa katika shule ya La Salle iliyoko katika mji wa Santiago de Cuba, ambayo ilikuwa anaendeshwa na makasisi wa kifaransa. Baadae akajiunga na shule binafsi ya kanisa katoliki ya Doleres Colegio, ambayo ilikuwa inasifika kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, lakini pia kiwango cha elimu iliyokuwa inatolewa kilikuwa cha hali ya juu.

Mwaka 1940, Castro alijiunga na shule ya sekondari ya Belen iliyopo mjini Havana, ambako alijifunza historia ya Cuba na kumsoma mwasisi wa taifa hilo ambaye alikuwa mpiganiaji wa uhuru wa Cuba kutoka kwa Uhispania. Mwaka 1945, Castro alijiunga na skuli ya sheria katika chuo kikuu cha Havana, ambapo ilimpa fursa ya kujihusisha na masuala ya siasa ambapo alijiunga na chama cha watu wa Cuba (Party of Cuban people) ambacho kilikuwa kinakosoa kwa wazi serikali ya rais wa wakati huo Ramon Grau San Martin na kulazimisha mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa serikali hiyo.

Chama hicho kilitaka serikali ijenge umoja wa kitaifa miongoni mwa Wacuba, pia kupinga ushawishi mkubwa kutoka mataifa ya kigeni katika mambo ya kijamii, kupendelea zaidi usawa wa kijamii, kuanzisha uhuru wa kiuchumi kwa Wacuba na pia mgawanyo ulio sawa wa utajiri wa taifa hilo kupitia uongozi uliobora wa serikali ambao utasimamia vema mali na uchumi wa taifa. Hotuba zake, mchango wake kisiasa na mambo mengine mengi yalimfanya Castro kutambuliwa kama sio kuwa na nguvu katika chama.

Mwaka 1947, Castro alijiunga na kundi la wanasiasa wahamiaji kutoka katika nchi za Caribbean ambalo liliweka makazi yake nchini Cuba. Pamoja na wanasiasa hao, Castro waliingia katika mapinduzi ya kumpindua dikteta wa Jamhuri ya Dominica Rafael Trujilo, lakini kwa bahati mbaya mapinduzi hayo hayakufanikiwa baada ya mapinduzi hayo kuanzia nchini Cuba.

Katika mwezi Aprili mwaka 1948, Castro alihudhuria mkutano wa tisa wa harakati wa umoja wa Wamarekani weusi uliofanyika mjini Bogota nchini Columbia. Lakini baada ya kuwasili nchi Colombia, Castro na rafiki yake Rafael Del Pino, walivuruga mkutano huo kwa kuonesha ujumbe uliokuwa katika vijitabu (makabrasha) yakiushutumu ushawishi wa nchi ya Marekani katika nchi za marekani ya kusini. Siku chache baadae, kiongozi wa chama cha kudai uhuru cha Colombia Alfredo Gaitan akauawa kwa sababu za kisiasa, hali hii ilipelekea wanafunzi kuandamana mitaani.

Baadae Castro akalaumiwa kwa kuchochea machafuko yaliyojulikana kama Bogotazo, lakini Castro alikuwa ni zaidi ya mtazamaji.

*****

Maisha ya ndoa ya Fidel Castro: mke wake wa kwanza alimuoa Oktoba 11, 1948 na alijulikana kama Mirta Diaz-Balart na walibahatika kupata mtoto wa kiume aliyezaliwa Septemba 1, 1949 na kupewa jina la Fidel Angel “Fidelito” Castro Diaz-Balart aliyekulia nchini Cuba na amewahi kufanya kazi katika tume ya nguvu za atomi ya Cuba kabla hajaondolewa katika nafasi hiyo na baba yake.

Baada ya kuachana na mke wa kwanza mwaka 1955, Castro alioa mke mwingine, Dalia Soto del Valle na kubahatika kuzaa naye watoto watano wa kiume ambao ni Antonio, Alejandro, Alexis, Alexander “Alex” na Angle Castro Soto del Valle.

Lakini wakati anamwoa mke wa kwanza Mirta, Castro alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana Natalia”Naty” Revuelta Clews, aliyezaliwa mjini Havana 1925. Kwa mwanamke huyu alizaa naye mtoto wa kike aliyeitwa Alina Fernandez-Revuelta.

Pia Castro ana mtoto mwingine wa kiume ambaye mama yake hajulikani na mtoto huyo anajulikana kama Jorge Angel Castro. Castro ana mtoto mwingine wa kike anayeitwa Francisca Pupo aliyezaliwa 1953, baada ya kulala na mwanamke mmoja kwa usiku mmoja.

Dada yake Castro, Juanita Castro anaishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960 na akiwa huko uhamishoni amewahi kusema, “Siwezi kujali zaidi nini kinachotokea katika nchi yangu. Kaka zangu Fidel na Raul Castro wamefanya gereza kubwa kupita kiasi lililozungukwa na maji. Watu wamegomewa kwa mateso makubwa yaliyoamriwa na ukomunisti.”
 
Last edited:
Hao ndiyo kiboko ya Marekani
conspiracy tuu. Hamna chochote, Inakuwaje awe na uhusiano mbaya wa kidiplomasia wakati sehemu ya ardhi yake (Guantanamo bay) ipo chini ya udhibiti wa Marekani under Cuban-American Treaty of 1903??? Kama kweli alikuwa shujaa mbona hajapigania wala kudai umiliki wa sehemu ya ardhi ya Cuba??? Anasifika sana kwasababu hakuwa kibaraka wa marekani, Lakini tukumbuke alikuwa kibaraka wa Urusi kipindi cha ujamaa na vita baridi.
 
Last edited:
Namkubali huyu jamaa..Ila namkubali zaidi Che Guevara
Ndio maana nilikuita,nakuaminia.
Ukiiweka uniite mkuu.
Marais wa marekani tangu keneddy waliondoka wakamuacha,kuna kipindi alikuja new york kuhuhutubia UN,-katika hoteli aliyofikia CIA wakaenda kuiba uharo wake kwa kudivert lile bomba la choo alichokua anakitumia, wakakinga na kwenda kupima maabara na wakatangaza Fidel ni mgonjwa atakufa ndani ya miezi 6,leo imepita miaka 40,jamaa anadunda tu
Duuuh!
Natamani mtu aweke post ya jinsi na namna gani alivyokoswakoswa mara zote hizo 31.
Wapi @ushiboy?
Tangu nakua mzee wangu alikuwa anapenda sana kunipa story za huyu mwanaharakati mpaka akaninunulia kitabu cha historia yake kwa kiswahili nikiwa darasa la nne, mzee anapenda ukomunisti mpaka basi humwambii kitu lakini bahati mbaya kazaa Capitalist Nigger.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)
Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC
miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha

baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga kwa Fudel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara hasiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUWAWA
Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA amabye alikuwa akiwakilsha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho ya ache na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake,

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”

Alifungwa kama na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”

Aliacha wake wawili na watoto watano
 
Ukomunisti unamaana sana katika kujaribu kuweka usawa.lakini hauko fairly kwamaana ya individuals.kila mtu aoneshe jitihada za kutafuta. Ukomunisti unalea uvivu na ugoigoi.wachache watateseka ili wengi washibe. Big no
 
Kuna mzee mmoja ni(ret)anaitwa Lt col Patrick marwa nyaborogo aliendaga Cuba kitambo
Alibahatika kuonana na fidel Castro live na wakapeana mikono....
Ana story nyingi sana za fidel castro
 
Back
Top Bottom