Maisha ya Fidel Alejandro Castro Ruz

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Je unamfahamu Fidel Castro? Huyu ni mtu aliyewahi kuwa Rais wa Cuba, mtu ambaye aliwahi kuwa askari wa msituni, mtu ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Kuba naye ni Fidel Alejandro Castro Ruz kwa kirefu
image.php

Fidel Castro alizaliwa Agost 13, 1926 ambapo amewahi kuwa mwanasiasa wa Kuba, mwanamapinduzi wa Kuba, Waziri Mkuu wa Kuba kati ya mwaka 1959 hadi mwaka 1976 na amekuwa Rais wa Kuba huru kati ya mwaka 1976 na 2008

Akiwa mwanasiasa wa Kuba Fidel Castro amekuwa amkifuata misimamo mbalimbali ya siasa za ulimwenguni haswa ule wa Marxist na Lenini na baadaye msimamo wa kimapinduzi wa Kuba.

Fidel Casto ameweza kufanya kazi kama katibu wa kwanza wa chama cha Kimkomunisti cha Kuba kati ya mwaka 1961 na 2011, chini ya utawala wake ambao ulikuwa wa chama kimoja, Castro ameweza kusimamia misimamo yake kimataifa.

Fidel Castro ameweza kuwa katibu mkuu wa umoja usiofungamana na upande wowote ule kati ya mwaka 1979 na 1983 na mwaka 2006 na 2008.

Fidel Castro amekuwa akiamini katika kufanya mapinduzi ya mtutu wa bunduki iwe kwa Latino Amerika, Asia na Afrika. “Kuhoji juu ya mapambano ya silaha kuwa ndiyo njia pekee ya ukombozi ninaweza kujibu kuwa ndani ya hoja hii taifa letu hatuna budi, katika raia wengi wa Kuba na mataifa mengi ya latino Amerika, hakuna njia nyingine ya kujikomboa zaidi ya matumizi ya mtutu. Hii inaonekana kuyafaa ata kwa mataifa mengine ya Asia na Afrika.

Kila mara mabeberu wanatumia kila namna wakiyaunganisha majeshi yao kwa kila taifa kuzuia demokrasia ya mapinduzi. Wanawanyonga watu kwa vitanzi, vitanzi hivi vinaweza kukatwa kwa kutumia mapambano ya silaha tu. Wanamapinduzi hawatumii silaha kama njia sahihi ya kujikomboa bali, hii ni njia inayoeleweka kwa haraka na wakandamizaji.

Kwa hiyo raia wana njia mbili kuvumilia ukandamizaji au kupambana na adui kwa silaha. Ifahamike wazi kuwa adui huyu ana nguvu za uchumi na kila kitu ata tekinolojia. Mapambano yanajumuisha kutumia kila kitu mlichonacho haswa matumizi ya rasimalia watu.” Anasema Fidel Castro katika mahojiano na mojawapo wa vyombo vya habari akiwa msituni.

Huyo ndiye Fidel Castro, ambaye leo hii ni rais msaafu wa Kuba taifa ambalo linaongozwa na mdogo wake Raul Castro.

Chanzo: TBC Tovuti
 
Last edited by a moderator:
Ila mda mwingine ucomunist naona mizinguo tu, kama inanyima Uhuru wana nchi
 
Huyu jamaa nankubali sana pamoja na Hugo Shavez , T Sankara na M Gadafi. The greatest issues of the day can not be decided by fine speeches and majority vote, rather though blood and iron.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Niliwahi soma mahali katika mtu anayeongoza kukoswa koswa na Majasusi ya CIA ni Fidel Castro, Pia anadaia CIA ndio waliomuua Hugo Chavez...
 
Huyu jamaa nankubali sana pamoja na Hugo Shavez , T Sankara na M Gadafi. The greatest issues of the day can not be decided by fine speeches and majority vote, rather though blood and iron.

Mkuu "Blood and Iron" siyo ya kuitamani hata kidogo.
 
Huyu jamaa nankubali sana pamoja na Hugo Shavez , T Sankara na M Gadafi. The greatest issues of the day can not be decided by fine speeches and majority vote, rather though blood and iron.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Umewasahau akina Jonas Savimbi na John Garang
 
Tangu nakua mzee wangu alikuwa anapenda sana kunipa story za huyu mwanaharakati mpaka akaninunulia kitabu cha historia yake kwa kiswahili nikiwa darasa la nne, mzee anapenda ukomunisti mpaka basi humwambii kitu lakini bahati mbaya kazaa Capitalist Nigger.

Je unamfahamu Fidel Castro? Huyu ni mtu aliyewahi kuwa Rais wa Cuba, mtu ambaye aliwahi kuwa askari wa msituni, mtu ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Kuba naye ni Fidel Alejandro Castro Ruz kwa kirefu
image.php

Fidel Castro
Fidel Castro alizaliwa Agost 13, 1926 ambapo amewahi kuwa mwanasiasa wa Kuba, mwanamapinduzi wa Kuba, Waziri Mkuu wa Kuba kati ya mwaka 1959 hadi mwaka 1976 na amekuwa Rais wa Kuba huru kati ya mwaka 1976 na 2008

Akiwa mwanasiasa wa Kuba Fidel Castro amekuwa amkifuata misimamo mbalimbali ya siasa za ulimwenguni haswa ule wa Marxist na Lenini na baadaye msimamo wa kimapinduzi wa Kuba.

Fidel Casto ameweza kufanya kazi kama katibu wa kwanza wa chama cha Kimkomunisti cha Kuba kati ya mwaka 1961 na 2011, chini ya utawala wake ambao ulikuwa wa chama kimoja, Castro ameweza kusimamia misimamo yake kimataifa.

Fidel Castro ameweza kuwa katibu mkuu wa umoja usiofungamana na upande wowote ule kati ya mwaka 1979 na 1983 na mwaka 2006 na 2008.

Fidel Castro amekuwa akiamini katika kufanya mapinduzi ya mtutu wa bunduki iwe kwa Latino Amerika, Asia na Afrika. “Kuhoji juu ya mapambano ya silaha kuwa ndiyo njia pekee ya ukombozi ninaweza kujibu kuwa ndani ya hoja hii taifa letu hatuna budi, katika raia wengi wa Kuba na mataifa mengi ya latino Amerika, hakuna njia nyingine ya kujikomboa zaidi ya matumizi ya mtutu. Hii inaonekana kuyafaa ata kwa mataifa mengine ya Asia na Afrika.

Kila mara mabeberu wanatumia kila namna wakiyaunganisha majeshi yao kwa kila taifa kuzuia demokrasia ya mapinduzi. Wanawanyonga watu kwa vitanzi, vitanzi hivi vinaweza kukatwa kwa kutumia mapambano ya silaha tu. Wanamapinduzi hawatumii silaha kama njia sahihi ya kujikomboa bali, hii ni njia inayoeleweka kwa haraka na wakandamizaji.

Kwa hiyo raia wana njia mbili kuvumilia ukandamizaji au kupambana na adui kwa silaha. Ifahamike wazi kuwa adui huyu ana nguvu za uchumi na kila kitu ata tekinolojia. Mapambano yanajumuisha kutumia kila kitu mlichonacho haswa matumizi ya rasimalia watu.” Anasema Fidel Castro katika mahojiano na mojawapo wa vyombo vya habari akiwa msituni.

Huyo ndiye Fidel Castro, ambaye leo hii ni rais msaafu wa Kuba taifa ambalo linaongozwa na mdogo wake Raul Castro. Kujua kinachoendelea juu ya maisha ya Fidel Castro, sikiliza Habari na Muziki ya TBC Taifa kila siku
 
Back
Top Bottom