Maisha ya depo

Tunaoamini mwezi huu hauishi bila kupata muendeleze TUFOLENI hapa
 
MAISHA YA DEPO


SEASON-4


EPISODE 01


“Woyoo woyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooh” lilikuwa ni shangwe kutoka kwetu ama baada ya kuruhusiwa.

Shangwe hilo lilikuwa ni ngumu kuepukika kwani ukiachana na njaa iliyokuwa imeota mizizi matumboni mwetu lakini kwetu ilikuwa ni sawa na wafungwa waliotoka kifungoni kwa msamaha wa Raisi kwa kauli ile iliyotoka kinywani mwa Matroni.

Haikuwa ruhusa ya kwenda kula tu bali kwetu ilikuwa ni furaha ya uhuru baada ya kutoka kwenye kifungo cha INTRO chini ya msitu wa makamanda WADOSOAJI.

Yalikuwa ni mateso ya masaa kadhaa mikononi mwa makamanda waliochafukwa roho kwenye siku tuliyokuwa tukisimuliwa kwa vitisho kana kwamba ni kiyama cha peke yetu.

Kwa upande mwingine hata kile kitendo cha kuwasikiliza watu walioshiba ilihali sisi wasikilizaji tukisikia njaa ilihali tumejichokea kimwili na kiakili nacho kilikua ni kifungo ambacho tulistahili kushangilia baada ya kupatiwa uhuru wake.

Tulikuwa tukishangilia huku tukikimbia kuelekea MAHANGANI ambako tulichukua vyombo na kuanzisha vita ya kusukumana milangoni kila mmoja akitaka kuwa wa kwanza kupata huduma ya MZABUNI.

Baada ya mapigano kwenye milango hiyo ikazuka marathoni kuelekea MESI ambako wengi wetu kituo cha kwanza kilikuwa ni kwenye matanki ya maji ambako tulikusanyika na vikombe vyetu tukipambana kukinga maji ya kunywa.

Ilikuwa ni vita ya wenye nguvu na aliyekuwa nayo zaidi ndiye aliyeshinda vita hiyo na kufanikiwa kukinga maji.

Kama wasemavyo waswahili “kuzaa si kupata” ndicho kilichotokea maana hata yule aliyebahatika kukinga hakufanikiwa kuyanywa yote kwani baada ya kikombe kujaa ilikuwepo vita nyingine ya kukitoa kikombe kwenye msitu wa vikombe.

Nakumbuka tukiwa shule tukijisomea siku moja mwanadada Linda aliyekuwa akijisomea somo la Fizikia aliniambia kuwa katika mashine kuna kitu kinaitwa ufanisi yaani uwiano kati ya kinachotoka kwenye mashine na kile kilichoingia kwa kimombo wanaita efficiency.

Wafizikia hao wametafiti na kugundua kuwa uwiano huo ukizidishwa kwa 100% huwezi kupata ufanisi wa 100% hata jua lichomoze kusini na kuzama kaskazini.

Tafsiri yake ni kuwa kinachotoka kwenye mashine ni kidogo kuliko kilichoingia kwa lugha nyepesi ukienda kusaga kilo 5 za mahindi utakachopata ni kilo pungufu za unga Linda alikuwa akinilazimisha mno nifuate nyendo zake kuijua PCM na alifanikiwa sana.

Hali hiyo ilifanana kabisa na kile kilichotokea pale bombani kwani baada ya kutoa kikombe kilichojaa maji kwenye msitu ule wa vikombe ikawa mpaka mtu anafanikiwa kutoa kikombe basi kilifika mdomoni kikiwa na maji nusu ama robo kabisa.

Kilichokuwa kikitokea kwenye matenki hayo wataalamu wa maji wanakiita “upotevu wa maji” yaani maji mengi yalikuwa yakimwagika pasipo kutumiwa zilihitajika busara kuiepusha hali hiyo.

Tukio hilo lilikuwa likihudhuriwa na kamanda wa zamu wa kikosi ambaye ni BAKABAKA ila kwa wakati huo hakuvaa sare yenye mchanganyiko wa rangi maarufu kama KOMBATI ya jeshi ama BAKABAKA.

Sare aliyovaa afande yule ilikuwa ikinitatiza maana sikuwahi kuona ikivaliwa mtaani nilikuja kuiona ikivaliwa kikosini hapo mpaka wakati huo sikuwa najua tofauti ya sare hizo zaidi ya kujua tofauti kati ya sare ya BAKABAKA inayotumika na askari wa Jwtz na ile KARANGA inayovaliwa na askari wa Jkt.

“Nyie si ni watu wazima nyie na mna akili timamu isitoshe ni wasomi mnaotarajiwa kwenda chuo siku zijazo hamuwezi kujiongeza mkauepuka huo upuuzi mnaoufanya” ilikuwa ni sauti wa kamanda huyo aliyekuwa akisogea pale tulipo.

“Hembu fungeni hayo maji haraka yaani wasomi tunaowategemea muwatoe ujinga darasa la saba tulionao kikosini ndiyo mnakuwa vinara wa huu ujinga nimesema fungeni hayo maji” aliendelea kuongea zaidi huku akisogea ilipo koki hiyo ya maji baada ya kuona hatumjali kwa kile anachokiongea.

“Mnajua maji ni ya shida lakini bado mnayamwaga mwaga hovyo mnashindwa kupanga foleni mkakinga mmojammoja hembu tokeni hapa” awamu hii alikuwa akiongea huku mkono wake ukiwa kwenye koki ya maji na kufunga maji yaliyokuwa yakimwagika bila kukingwa.

“Angalieni sasa hapa chini maji kibao yamemwagika pengine kuliko hata mliyokunywa hivi huo usomi wenu mtautumia wapi sasa au ndiyo mnataka mkautumie huko chuo” aliendelea kujiongelesha afande huyo huku akituonesha maji yaliyopotea chini karibu na koki ya tenki hilo.

“Msijidanganye KURUTA tabia ni kama Ngozi ya mwili mkishindwa kutumia akili hapa hata ukifika huko chuo utajikuta unashindwa kutumia hiyo akili uliyo nayo kwasababu siyo tabia yako kutumia akili” afande huyo aliendelea kuongea kwa lafudhi yake ya kiunguja ambayo ilitushawishi kuendelea kumsikiliza.

“Akili…… jifunzeni kutumia akili au kwa sababu akili ni nywele ndo sababu ya kuwafanya msiwe na akili kutokana na hiyo mipara yenu hembu jitahidini kutumia akili KURUTA akili……” aliendelea kusisitiza huku akielekeza kidole chake cha shahada cha mkono wa kulia kwenye kichwa kama msisitizo wa kutumia akili.

“Haya hembu mmoja wenu aende jikoni pale akalete ndoo mkinge maji na nyie mliokwishakunywa maji muende mkapange FOLENI ya chakula kule” alituambia tukabaki tumetulia kumshangaa na akosekane mtu wa kwenda kufuata hiyo ndoo aliyoagiza.

Afande huyo alininyooshea kidole cha uteuzi na kuniagiza kuifuata bila pingamizi lolote nilienda jikoni na kuomba ndoo ambayo mwanzo nilikataliwa ila nilipotoa maelezo yaliyonyooka kuwa nimeagizwa na poti huyo mwenye lafudhi ya watu wa visiwani ndipo nikapatiwa.

“Haya njoo mwangu uikinge hapa uwagawie maji hao MANANGA” aliniambia afande huyo baada ya kwenda nayo bombani hapo nikafanya hivyo.

“Kama una kiu kinga kikombe chako unywe KURUTA” afande alinipa nafasi hiyo nami nikaitumia barabara. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,



…………………………………………………………………….…………….………………….…Itaendelea………………………………………………………………………………………….…………….……………
 
Sasa mbona fupi kuruta
 
kuna siku nilikutana na Afande wa kike akiwa na maafande wenzake wa kiume , hapo nimechoka sana baada ya kula doso la kutosha, akaniambia baby umesema unataka nikutambulishe shemeji zako. Kilicho endelea baada ya hapo ni maumivu tu aiseee😂

Yaani nilihisi hawa jamaa ni Kama vichwani mwao kumejaa funza tu, wana akili mbovu sana aiseee
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 dah
 
PUBLIC ANNOUNCEMENT

Hello, here to announce that, the continuation of our narrative "Maisha_ya_depo" will commence on first-day of next month. This means that in the first week of September 1st, which will be a Monday, there will be a series of episodes released from Maisha_ya_depo-4. Do you remember where we ended last season? Would you be interested in knowing what happened after the day of "introduction to the camp"? Do you know anything about the vigil? Do you want to know what happened in "six weeks"? Don't worry, prepare your package(data/MBs), remember where we ended up, and then leave the responsibility of telling the story to me.

Naomba kizungu kiishie hapa, nilikuwa nataka kujua tu kama ada ya Mzee Mjuzi haikwenda bure kikubwa nili-miss kuwasimulia (yaani nilikuwa nikiendelea na majukumu mengine mkono ulikuwa unaniwasha kusimulia ila ndo hivyo tena kudra hushinda jitihada). Kama nilivyokwisha kuwaambia kwenye hivyo vifungu vya Mfalme Charles hapo juu kazi ya kusimulia niachieni mimi, MCHAWI BANDO.
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-4

EPISODE 01

“Woyoo woyooooooooh! Wooooszaaaaaaaah! Bahobahobahooooh!” hili lilikuwa ni shangwe baada ya kuruhusiwa.

Haikuwa ruhusa ya kwenda kula tu bali kwetu ilikuwa ni furaha ya uhuru baada ya kutoka kwenye kifungo cha INTRO.

Yalikuwa ni mateso ya masaa kadhaa mikononi mwa makamanda WADOSOAJI waliochafukwa roho kwenye siku tuliyokuwa tukisimuliwa kwa vitisho kana kwamba ni kiyama cha peke yetu.

Tulikuwa tukishangilia huku tukikimbia kuelekea MAHANGANI ambako tulichukua vyombo na kuanzisha vita ya kusukumana milangoni kila mmoja akitaka kuwa wa kwanza kupata huduma ya MZABUNI.

Baada ya mapigano kwenye milango hiyo ikazuka marathoni kuelekea MESI ambako wengi wetu kituo cha kwanza kilikuwa ni kwenye matanki ya maji ambako tulikusanyika na vikombe vyetu tukipambana kukinga maji ya kunywa.

Ilikuwa ni vita ya wenye nguvu na aliyekuwa nayo zaidi ndiye aliyeshinda vita hiyo na kufanikiwa kukinga maji.

Kama wasemavyo waswahili “kuzaa si kupata” ndicho kilichotokea maana hata yule aliyebahatika kukinga hakufanikiwa kuyanywa yote kwani baada ya kikombe kujaa ilikuwepo vita nyingine ya kukitoa kikombe kwenye msitu wa vikombe.

Nakumbuka tukiwa shule tukijisomea siku moja mwanadada Linda aliyekuwa akijisomea somo la Fizikia aliniambia kuwa katika mashine kuna kitu kinaitwa ufanisi yaani uwiano kati ya kinachotoka na kile kilichoingia kwenye mashine kwa kimombo wanaita efficiency.

Kwa mujibu wa wanafizikia hao wanasema kuwa uwiano huo ukizidishwa kwa 100% huwezi kupata ufanisi wa 100% hata jua lichomoze kusini na kuzama kaskazini.

Tafsiri yake ni kuwa kinachotoka kwenye mashine ni kidogo kuliko kilichoingia kwa lugha nyepesi ukienda kusaga kilo 5 za mahindi utakachopata ni kilo pungufu ya 5 za unga kusema kweli Linda alikuwa akinilazimisha mno nijue wanachokisoma na alifanikiwa sana.

Hali hiyo ilifanana kabisa na kile kilichotokea pale bombani kwani baada ya kutoa kikombe kilichojaa maji ilibidi tena kupambana kwenye msitu wa vikombe hivyo mpaka mtu anafanikiwa kutoa kikombe basi kilifika mdomoni kikiwa na maji nusu kikombe.

Kilichokuwa kikitokea kwenye matenki hayo wataalamu wa maji wanakiita “upotevu wa maji” yaani maji mengi yalikuwa yakimwagika pasipo kutumiwa.

Tukio hilo lilikuwa likihudhuriwa na kamanda wa zamu wa kikosi ambaye ni BAKABAKA ila kwa wakati huo hakuvaa sare yenye mchanganyiko wa rangi maarufu kama KOMBATI ya jeshi ama BAKABAKA.

Sare ile aliyovaa afande sikuwahi kuona ikivaliwa mtaani nilikuja kuiona ikivaliwa kikosini hapo mpaka wakati huo sikuwa najua tofauti ya sare hizo zaidi ya kujua tofauti kati ya sare ya BAKABAKA inayotumika na askari wa Jwtz na ile KARANGA inayovaliwa na askari wa Jkt.

“Nyie si ni watu wazima wenye akili timamu isitoshe ni wasomi mnaotarajiwa kwenda chuo siku zijazo hamuwezi kujiongeza mkauepuka huo upuuzi mnaoufanya?” ilikuwa ni sauti wa kamanda huyo aliyekuwa akisogea pale tulipo.

“Hembu fungeni hayo maji haraka yaani wasomi tunaowategemea muwatoe ujinga darasa la saba tulionao kikosini ndiyo mnakuwa vinara wa huu ujinga nimesema fungeni hayo maji” aliendelea kusisitiza afade huyo huku akisogea ilipo koki hiyo ya maji baada ya kuona hatuzingatii kile alichokuwa akikiongea.

“Mnajua fika maji ni ya shida lakini bado mnayamwaga mwaga hovyo mnashindwa kupanga foleni mkakinga mmojammoja kweli!” awamu hii alikuwa akiongea huku mkono wake ukiwa kwenye koki ya maji na kufunga maji yaliyokuwa yakimwagika bila kukingwa.

“Angalieni sasa hapa chini maji kibao yamemwagika pengine kuliko hata mliyokunywa hivi huo usomi wenu mtautumia wapi sasa au ndiyo mnataka mkautumie huko chuo” aliendelea kujiongelesha afande huyo huku akituonesha maji yaliyopotea chini karibu na koki ya tenki hilo.

“Msijidanganye KURUTA tabia ni kama Ngozi ya mwili mkishindwa kutumia akili hapa hata mkifika huko chuo mtajikuta mnashindwa kutumia hizo akili kwasababu siyo tabia yenu kutumia akili” afande huyo aliendelea kuongea kwa lafudhi yake ya kiunguja ambayo ilitushawishi kuendelea kumsikiliza.

“Akili…… jizoesheni kutumia akili au kwa kuwa akili ni nywele ndiyo maana mnakuwa hamna akili kwasababu ya hayo mapara yenu hembu tumieni akili basi……” aliendelea kusisitiza huku akielekeza kidole chake cha shahada cha mkono wa kulia kwenye kichwa kama msisitizo wa kutumia akili. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,



……………………………………….…Itaendelea……………………………………………
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-4

EPISODE 02

“Haya hembu mmoja wenu ende jikoni pale akalete ndoo mkinge maji na nyie mliokwishakunywa maji muende mkapange FOLENI ya chakula kule” alituambia tukabaki tumetulia kumshangaa na akosekane mtu wa kwenda kufuata hiyo ndoo aliyoagiza.

Afande alininyooshea kidole cha na kuniteua kuifuata bila pingamizi lolote nilienda jikoni na kuomba ndoo ambayo mwanzo nilikataliwa ila nilipotoa maelezo yaliyonyooka kuwa nimeagizwa na poti huyo mwenye lafudhi ya watu wa visiwani ndipo nikapatiwa.

“Haya njoo hapa soja uwagawie maji hao MANANGA” aliniambia afande huyo baada ya kwenda nayo bombani hapo nikafanya hivyo.

“Kama una kiu kinga kikombe chako unywe KURUTA” afande alinipa nafasi hiyo nami nikaitumia barabara.

“Kama hujatosheka ongeza KURUTA mpaka kiu ikate yaani mimi nawaagiza mfuate ndoo mnanikodolea macho sasa ni mpaka atosheke aliyeifuata ndiyo mfuate nyie MANANGA” kikweli niliitumia vizuri hii nafasi nakumbuka nilipiga vikombe kama vitatu hivi wastani wa lita moja na kidogo.

Baada ya ndoo kujaa nilifunga koki na kusogea mbele kidogo sehemu ambayo ilikuwa ni kavu kama alivyonielekeza afande ambaye aliwaambia wapange foleni na mimi nikawa nawagawia mmoja baada ya mwingine hata hivyo afande alizuia matumizi ya koki na aliifunga akiagiza kila aliyetaka kukinga maji kutumia FOLENI hiyo.

“We KURUTA hakuna kumuongeza mtu maji hapo kama anataka kuongeza mwambie arudi nyuma kule akapange foleni tena usimpe maji ambaye hayuko kwenye mstari” yalikuwa ni maagizo kutoka kwa kamanda huyo wa zamu.

Haikuchukua muda ndoo ile ya maji iliisha nikaenda kuikinga tena ingawaje ulionekana ni utaratibu unaopoteza muda lakini uliepusha sana upotevu wa maji kwani hata huo muda ambao tungeuokoa kila mmoja akipigana kwenye koki usinge tuhakikishia kupata maji kwa ufanisi unaotakiwa.

Baada ya ndoo hiyo kujaa utaratibu wa mwanzo ukaendelea na afande akamuagiza mmoja wetu kusimama kwenye koki isije kufunguliwa na mwingine zaidi yangu.

Aliondoka na kwenda zake jikoni ambako alitakiwa kwenda kusimamia ugawaji wa chakula hivyo akatuacha kwenye balaa hilo ambalo halikuwa jepesi kwakweli ama kweli ni bora kuwaongoza watoto wa chekechea kuliko watu wazima wenye akili zao

Baada ya muda afande alirudi akiwa na ndoo mkononi alinikuta nikikabiliana na kundi la watu kwenye koki nikiwazuia waache kuteka maji na kufuata utaratibu tulioachiwa.

Nilibahatika kuwashawishi wengi wao huku wengine wakiwa hawajakubaliana nami swala ambalo ni la kawaida kwenye jamii huwezi kukubaliwa na wote lazima litatokea kundi lenye kukupinga afande aliikuta hali ile akawatoa watu hao na kisha akawatenga na kuwapa DOSO.

“Yaani mimi natoa utaratibu nyie mnakaidi sawa nimeondoka sipo namuacha kiongozi awasimamie anajitahidi kuwaambia taratibu zilivyo mnamsukuma kuonesha nyie ni vidume kunja ngumi KURUTA” afande alikuwa akiwaambia wale jamaa aliokuwa akiwaadabisha kitu ambacho kuanza kwa kozi kwani tulipokuwa WAZALENDO hakukuwa na maswala ya kupena adhabu wakati wa kula.

“Na ninaondoka tena naenda kusimamia foleni ya chakula nawaacha na viongozi wenu waendelee kuwasimamia sasa itokee nije nikikute kidume kinajifanya hakitaki kuwasikiliza viongozi atanieleza natokea Wete, Chakechake au Nungwi” ulikuwa ni mkwara kutoka kwa afande huku akionekana mwenye kukasirishwa na kilichotokea.

“Nyie viongozi mkimaliza mtaniletea hizo ndoo zangu jikoni na nyie MANANGA hapo natoka ila nitarudi nikija niwakute hapohapo sasa ole wenu muondoke na akitokea mwingine hawasikilizi nyie viongozi waunganisheni na hawa akiwapinga mleteni kwangu mmenielewa KURUTA”.

“Ndiyo afande” tulimjibu afande huyo akaelekea zake kwenye foleni.

Nikiwa naendelea na majukumu hayo nilisikitishwa na kitu kimoja ambapo katika wale waliokua wakiadhibiwa alikuwepo jamaa yangu Amosi.

Kilichonisikitisha siyo yeye kuadhibiwa ila ni kuwepo kwake kwenye lile BOGI inamaana kuwa kipindi mimi natuliza fujo yeye ndo alikuwa akihamasisha fujo walikuwa sahihi wahenga waliposema “Kikulacho ki nguoni mwako yaani mwana naye alikuwa akinikataa”.

Aliwahi kuimba Mr. kikulacho “Unacheka naye, unakula naye kumbe mwenzako anaona gere” hivyo ndivyo walimwengu walivyo amini usiamini snitch naye mwana.

……………………………………….…Itaendelea……………………………………………
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-4

EPISODE 03

Alikuta mambo yapo kama yalivyotakiwa kuwa alitupongeza na kuteua wengine wasimamie kazi hiyo kisha sisi akaturuhusu kwenda kufuata chakula.

Wale jamaa waliokuwa kwenye DOSO aliwaruhusu wakaamka na kuendelea na shughuli zao kisha tukaondoka naye na kumuacha afande Mbega akiwasimamia jamaa zetu pale bombani.

Moja kwa moja tulienda mbele ya foleni tukiwa na afande ambaye alimwambia mgawaji atuwekee chakula cha kushiba tuliwekewa nguna, finyango zetu mbilimbili na chuzi bwerere.

Tukiwa tunaelekea kuumanga KURUTA waliokuwa kwenye foleni walikuwa wakituangalia huku macho mengi yakiwa kwangu na kila aliyeniangalia hakuacha kuangua kicheko nilielewa hakuna kingine zaidi ya kile kituko kilichowafanya wacheke tukiwa UWANJA WA DAMU.

Tulifuta ule msosi ila tumbo bado lilikuwa likidai tulishauriana na yule jamaa kipi kifanyike majibu yakawa ni KUBASTI.

“Yaani WAZALENDO mnabembelezwa kuongeza ubwabwa mnaringa shauri yenu mtaukumbuka tu kozi ikinoga wakati mnatoka zenu kwenye MAFATIKI huko mta BURST zaidi ya mara saba na bado hamtashiba” nilijikuta nimeyakumbuka maneno ya SM ile siku ya kwanza kutinga kikosini ambapo wagawaji walituita tukaongeze tukawa tunaringa.

Swali likawa je, tutafanyaje ingali watu walituona kipindi tunaondoka na chakula na mbaya zaidi sababu yangu walikuwa wakituzingatia wakati mwingine kumbe umaarufu siyo dili.

Bwana mipango nikaclose multiplication nikaona vitu vinawezekana kwani kipindi tunatoka na msosi tulikuwa katikati ya FOLENI mbili kati ya sita ina maana zipo nyingine nne hazikutuona twende hukohuko kwenye hizo nyingine.

Utaratibu wakati wa chakula ilikuwa kila KOMBANIA ina jungu lake kwahiyo kila KOMBANIA inapanga FOLENI yake na sisi kwa sababu tulikuwa ni kesi maalum afande alitupeleka kuchukua chakula kwenye jungu la BRAVO hivyo wakati tunarudi tulipita katikati ya FOLENI ya BRAVO na CHARLIE.

Kwakuwa hazikuwa KOMBANIA zetu hivyo mwanya wa KUBASTI ulijichomoza hapo kwani yule mwenzangu alitokea ALFA na mimi kama mnavyonijua ni DANGER Coy.

Tulikwenda bombani kusuuza vyombo kwa ajili ya kufuta ushahidi wa kuwa tumekwishakula ila tulipofika tulimkuta afande Mbega ambaye alikuwa akisimamia zoezi aliloachiwa na afande mpemba.

Wakati huu hakukuwa na fujo kama mwanzo nafikiri ni kwa sababu ya uwepo wake lakini pia watu wengi tayari walikwisha pooza kiu.

“Anhaah KURUTA mmerudi vipi mshakula” aliuliza afande Mbega swali hilo la kitoto kwani si sahani tu lakini pia ukituangalia mikononi utagundua kuwa tayari tumekwishakula.

“Ndiyo afande” nilimjibu bila kupepesa macho.

“Mmeshiba lakini” afande huyo alituuliza swali moja muhimu sana ambalo tulikuwa tukitamani liulizwe kwenye wakati kama huo yaani kwa lugha ya mtaani poti aliingia kwenye mfumo.

“Daah kusema ukweli afande hilo swala la kushiba tusikudanganye bado hatujaona kitu afande”.

“Anhaah basi sawa subirini wenzenu wamalizie muondoke na hizo ndoo mtamwambia afande kule au hayupo KURUTA”.

“Nahisi atakuwepo ila naona anazunguka kwenye FOLENI”.

“Nyie msiwaze hata kama msipomkuta mkiwaambia wapishi au wagawaji hamjala mlikuwa mnafanya kazi ya afande atawaelewa”.

“Sawa afande”

“Mbona mmejibu kwa wasiwasi au nawasubiri twende wote basi” alituambia hivyo afande Mbega baada ya kuona tunajibu kwa kusitasita.

Baada ya maji kuisha katika zile ndoo tulizisuuza na kwenda na afande Mbega mpaka jikoni ambako alitupeleka bahati iliyoje tulikutana na yule mpishi aliyenipatia ndoo pale mwanzo.

“Anhaa dogo umeniletea ndoo yangu siyo”

“Ndiyo dada”

“Ushakula?”

Afande Mbega alitugeukia na kututonya kwa kuwa tayari nilikuwa nimepita kozi kule quba niliweza kumuelewa alichokimaanisha.

“Bado”

“We sema kweli”

“Kweli muulize hata afande hapo tuliachiwa kazi na yule afande anayesimamia foleni”

“Kazi gani hiyo wakati wa kula”

“Watu walikuwa wanamwagamwaga maji ndiyo afande akasema tuchukue ndoo tukinge ndiyo mimi na jamaa tukawa tunawagawia”.

“Dada hawajala bwana wawekee msosi nilikuwa nao bombani”

“Usijali namzingua tu rafiki yangu sasa na wewe umekula? Au umeshiba afande?”

“Hamna sijala ngoja niangalie sahani hapa au unayo ya akiba”.

Tuliwekewa msosi na baada ya mlo tukarudi zetu MAHANGANI ndipo takaulizana muda ilikuwa inasoma kumi na moja kasoro.

ndipo nikagundua kuwa ilikuwa ni haki kuwa na kiu pamoja na njaa kali kiasi kile ikumbukwe tulishinda kwenye jua kwa muda mrefu na pia hatukula kwa muda mrefu kwani kwa ratiba ya kawaida tulitakiwa kula saa nane.


...….……Itaendelea.….….……
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-4

EPISODE 04

Hatukuweza kupumzika hata kidogo tukazisikia filimbi kwa mara nyingine zikituita tulilaani sana kwani tulikuwa tumechoka kutokana na dhahama tuliyokumbana nayo lakini pia tuliona muda umeenda hivyo tulikuwa na hesabu za kulala na kusubiri muda wa chakula cha jioni.

Jeshi halijawahi kuwa na ratiba kama hiyo kwani kwao kila mlo utakaoingia tumboni ni lazima ufanyiwe kazi hauwezi kwenda bure mtaenda kubeba hata vifusi ama mchimbe shimo la taka.

Ni vile tulijisahaulisha lakini katika moja ya nyimbo zao kuna ule unaosema “Kila baada ya kula KOMBANIA” sasa huu utaratibu wa kulala baada ya kula haswa kipindi cha SIXWEEKS ni sawa na kulimodoa jeshi.

Tulifoleni KOMBANIA na kukabidhiwa mikononi mwa jamaa wa mazoezi ya viungo (yaani Physical Training kifupi PT) kama utakuwa unawazingatia vizuri ni wale jamaa wanaotuamsha asubuhi kwenda kwenye MABIO ingawaje wakati mwingine husaidizana na makamanda wa zamu pamoja na makarani.

Walitugawa MABOGI kadhaa na tukaanza mbio hizo za jioni zilizochukua umbali wa kilomita zaidi ya tano kwenda na kurudi kwa upande wetu tulikuwa na jamaa yetu Masare aliyekuwa akituimbisha.

“Masare: Tutampataje kunguru
Sisi: Aaaaai! aai!
Masare: Agaaah!
Sisi: Sote tukae chini tujiulize
Masare: Eeeh na mbawa zake za woga
Sisi: Aaaaai! aai!
Masare: Agaaah!
Sisi: Sote tukae chini tujiulize
Masare: Ana ka kei kadogo
Sisi: Aaaaai! aai!
Masare: Agaaah!
Sisi: Sote tukae chini tujiulize
Masare: Sema mpaka upulize manyoya

Sisi: Aaaaai! aai!
Masare: Agaaah!
Sisi: Sote tukae chini tujiulize
Masare: Kunguru yeye wa Zanzibar
Sisi: Aaaaai! aai!
Masare: Agaaah!
Sisi: Sote tukae chini tujiulizeee
Sisi: Kunguru na Kanga mzuri naniii?
Masare: Mzuri Kanga mwenye madoaaa
Sisi: Kunguru na Kanga mzuri naniii?
Masare: Mzuri Kanga mwenye madoaaa
Sisi: Ina ina inamadoa
Masare: Inaaa inamadoa inaa
Sisi: Ina ina inamadoa
Masare: Inaaa inamadoa inaa”.

Awamu hii mbio zilianzia KOMBANIA tukapita zetu UTAWALA mpaka kwenye makutano ya barabara nne ndipo tukashika ile inayoelekea REST HOUSE tukapita kwenye daraja huku tukiuchungulia mto uliotukumbusha maswahibu tuliyokutana nayo masaa machache yaliyopita.

Mbio hazikuishia kwenye daraja hilo tulinyoosha mpaka tukalifikia geti la Mashariki tukalipita na kutokomea kwenye mashamba ambayo hatukuwahi kufika tukiwa njiani tuliliona bwawa ambalo tulipokuwa kwenye utambulisho tuliambiwa wale wahalifu wanaopigwa risasi kwenye geti hilo miili yao hutupwa kwenye hilo bwawa.

Tulikimbia mpaka mwisho wa mbio na tulipofika tulipooza injini huku tukijuliana hali na kupiga stori za hapa na pale na kusema ukweli ukiachana na tukio lenyewe la utambulisho gumzo namba mbili lilikuwa ni mimi na safari yangu ya kuzimu siyo siri banzi la afande Kalaghe lilizidi kunipandisha chati.

Baada ya MABOGI yote kufika ilianza safari ya kurejea kikosini kama kawaida mwanetu Masare ndiye akawa muimbishaji.

Masare: Pesa pesa pesa imemtoa mwali ndani
Sisi: Pesa pesa pesa imemtoa mwali ndani
Masare: Mara kwanza akasema
Sisi: Wee mama naumia
Masare: Mara ya pili akasema
Sisi: Mdogomdogo ntazoea
Masare: Mara ya tatu akasema
Sisi: Nasikia raha utaaamu
Masare: Jamani raha
Sisi: Utaamu
Masare: Wee nasikia raha
Sisi: Utaamu
Masare: Jamani raha
Sisi: Utaamu
Masare: Mabio raha
Sisi: Utaamu
Masare: Na chenja raha
Sisi: Utaaamu”.

Tulirudi zetu moja kwa moja mpaka MAHANGANI ambako mwenye kuoga alioga na mwenye kulala hakuiachia nafasi hiyo hata kidogo na haikuchukua muda watu walianza kukoroma.

Binafsi niliamua kwenda zangu mtoni kuoga kwani nilikuwa nikijiona kama msukule uliotelekezwa tulitulia zetu mtoni tukipiga porojo za hapa na pale mpaka ulipofika muda wa msosi.

Kwa kuwa bado nilikuwa nikijihisi shibe tumboni mwangu nilijivutavuta nikaenda KUFOLENI kwa kuchelewa hali iliyonifanya kuwa miongoni mwa watu wa mwishoni kwenye FOLENI hiyo.

Chakula kiliisha huku kukiwa na kundi kubwa la watu ambalo bado lilikuwa kwenye FOLENI hali iliyompelekea MZABUNI kulalamika kwani kwa hesabu zake alipika kiasi anachopika siku zote ambacho ndicho kilichopo kwenye mkataba akaweka na ziada ila alishangazwa kimeisha na watu bado hawajala hizi ni ishara za kuanza kwa kozi.

……………………………………….…Itaendelea……………………………………………
 
📢 TANGAZO LA KAZI – HORIZON INSTITUTE 📢

Horizon Institute inafungua nafasi za kazi katika kozi mbalimbali za kuelimisha! Ikiwa una ujuzi au shauku ya kufundisha, hii ni fursa yako ya kuunga mkono jamii ya wanaojifunza.

🌟 Maeneo ya Kazi Yanayopatikana:

🗣 LUGHA ZA KIGENI
✅ English
✅ French
✅ German
✅ Kitaliana
✅ Russian
✅ Romanian
✅ Spanish
✅ Arabic
✅ Kiswahili
✅ Chines

💻 KOZI ZA COMPUTER
✅ Computer Application
✅ Graphic and Design
✅ Video Production
✅ Air Fare and Ticking

🛠 KOZI NYINGINEZO
✅ Tour Guider
✅ Tuition of all level (Nursery mpaka Advanced)
✅ Cleaner Hotel Management
✅ Ususi
✅ Make Up (Upambaji)
✅ Uchoraji wa hinna na piko

⏳ Mwisho wa Kuwasilisha Maombi: 14/12/2025

🌐 Jinsi ya Kuomba:
Tuma ombi lako kupitia website yetu:
👉 Horizon Institute - Mfumo wa Maombi ya Kazi

📞 Kwa maswali au usaidizi, wasiliana nasi kupitia:
📞 0722 186 012
📞 0786 199 664
📧 Amani Magazeti Zanzibar
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…