Maisha Si Digrii Wala Cheti

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
4,291
2,466
Sitaki kwenda kwenye details sana ila yupo kijana mmoja pale kkoo kanisababisha kuongeza. Kufikiri katika kuongeza kipato kijasiriamali zaidi. Mjini kuna vyoo vilivyojengwa vya kulipia.

Hivi vyoo aidha ni vya mkubwa fulani au mtu mwenye ushawishi na ambaye ana pesa zake. La, ni vya halmashauri/manispaa husika. Sasa huyu kijana mdogo tu na ambaye ana mke na mtoto mdogo kabisa, akijua hana mtaji wala ushawishi wa kuweza kuomba eneo, kaja na wazo ambalo ndio sehemu yao ya kupatia riziki. Huyu kijana alimtafuta mwenye jengo ambapo nafanyia biashara zangu. Kaongea nae kuhusu kumkodishia choo tunachotumia siku zote. Atawajibika kwa maji, umeme, usafi, na kodi elf 50 kwa mwezi kumpa mwenye jengo. Tuseme kwa siku wanaingia chooni watu 50 kwa tsh 200. Ni elf 10. Jamaa ana sehem zingine mbili kama hizo, na hapo kwetu kamweka mkewe. Kwa mwezi ana laki 9 kabla hajatoa gharama zingine.

Pengine nae wazo kapata/kaona sehemu lakini kakamatia fursa. Maisha ni kujipanga kwa kweli. Kama huyu ana upeo kama huu, je wewe uliyesomasoma?
 
Ila biashara sio constant kama unavyofikiria kwa maana hapo unaasume watu wanafanya kazi mpaka jumapili yani siku 7 kwa wiki x either 28 au 30 days = kwa hesabu za baraka mwezi either una siku 24
 
Ila biashara sio constant kama unavyofikiria kwa maana hapo unaasume watu wanafanya kazi mpaka jumapili yani siku 7 kwa wiki x either 28 au 30 days = kwa hesabu za baraka mwezi either una siku 24
Ni Kweli Hujaelewa. Na Biashara Kutokuwa Constant Si Lazima Wawe Watu 50 Kwa Silu, Wanaweza Kuwa Zaidi Pia
 
Back
Top Bottom