Maisha Ni Vile Uyachukuliavyo

Maisha Ni Vile Uyachukuliavyo

mojax

Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
13
Reaction score
23
ELIMU BIASHARA

Usilinganishe Mapito Yako na Ya mtu mwingine, Changamoto zako na Za Mtu mwingine, kwakua zakwako zilipangwa zikupitie wewe na uweze kuzikabili. Hakuna Changamoto nzito au kubwa utakayopewa ambayo hautaweza kuikabili, Mungu hutupa changamoto kutokana na uwezo wetu wa kuzihandle.

Tujifunze kushukuru kwa yote, tujifunze kuwa na positive minds. Unajua kuna tofauti kati ya kusema "Samahani Nimechelewa" na "Asante kwa Kunisubiria Mpaka Muda huu". Japokua yote yana maana sawa na yote yanatumika pale ambapo umefika nje ya wakati, lakini kuna moja lina sound vizuri zaidi.

Kabla mwanao hajatamani kuwa kama Mtu fulani, jitahidi atamani kuwa kama wewe. Kabla mwanao hajatamani angekua na Baba kama wa Fulani, jitahidi ajisikie proud kuwa na Baba wewe. Ulichonacho hakitakua sawa kama utahisi haukistahili au chemyewe hakistahili kuwa nawewe au kuwa kwako, Ili ukishukuru hata kwa hicho utajiona tayari unacho ukitakacho na vingine utavipata kama ziada na vitakuja tu kwakua urisharidhika na kile kidogo.

By Man Dea
 
"Samahani nimechelewa" na "Asante kwa kunisubiria mpk muda huu".
Nimejifunza kitu..
 
Back
Top Bottom