Maisha ni Safari Usione ukadhani

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
1,823
2,000
Baada ya kusimamishwa kazi serikalini kwa Tuhuma za Vyeti feki miaka mitatu iliopita sijapata Ajira sehemu yoyote ile

Kwa kweli katika kipindi hichi nimejifunza mambo mengi sana kuhusu Maisha

  1. Sasa hivi mimi ni mpishi mzuri sana kwani ilinibidi niingie kwenye kazi hizo kwa sababu ya kukosa mtaji
  2. Sasa hivi nimejua jinsi ya kuongea na mwenye nyumba unapokuwa hauna kodi ya nyumba
  3. Sasa nimejua jinsi ya kuongea na Mangi ili kukopa chakula cha familia
  4. Sasa hivi nimejua kuwa dalali wa nyumba,vyumba viwanja na mashamba
  5. Sasa hivi nimejua kuhusu Vikoba na ni mdau mwaminifu
  6. Sasa hivi nimejua marafiki wa kweli na marafiki feki kama vyeti vyangu
  7. Sasa hivi ninajua kutengenza Simu,Kompyuta
  8. Sasa hivi najua kuendesha gari na pikipiki
  9. Sasa hivi najua kufundisha tuisheni

Sasa hivi najua kwamba Maisha ni Safari na lamuhimu ni kupambana
 

Mirlz B Matthew

JF-Expert Member
Oct 10, 2011
1,733
2,000
Safi sana....maisha hubadilika ndani ya muda mfupi....Maisha ni safari isiyokuwa na likizo..!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom