Maisha na fursa Kyerwa

Maisha na fursa Kyerwa

Rusumo one

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
3,548
Reaction score
4,487
Kama heading inavyojieleza.Nimepata kibarua katika H/Wilaya ya Kyerwa naomba kujua fursa na changamoto zilizopo Wilayani pale ndg zanguni.Naomba kuwasilisha kwenu kwa Maoni na mapendekezo.
 
Mkuu huko ndiko alikozaliwa na kukulia JIWE. Fursa iliyoko huko ni kuingiwa na roho ya:- chuki, kisasi, ukatili na roho mbaya. Utakuwa ukiwaona matajiri unataman waishi kama mashetan. Kichwa chako kitabonyea muda c mrefu
fursa pls
 
Utalima maharage na kwenda kuuza Kikagati,Uganda!!!ila ufunge mkanda kweli wilaya hiyo usafir ni wa shida sana na kama ujuavyo wahaya ni watu wenye ukabila sana na ubinafsi kama siyo wa huko,nmemalza
 
Na
Utalima maharage na kwenda kuuza Kikagati,Uganda!!!ila ufunge mkanda kweli wilaya hiyo usafir ni wa shida sana na kama ujuavyo wahaya ni watu wenye ukabila sana na ubinafsi kama siyo wa huko,nmemalza
Nashukuru kwa Maoni yako ndg yangu barikiwa sana
 
Changamoto za kule ni usafiri. Toyota colola inayobeba abiria watano kule inapakia abiria 12. mnakaliana ukifika unakokwenda sharti umeze panado
 
Changamoto za kule ni usafiri. Toyota colola inayobeba abiria watano kule inapakia abiria 12. mnakaliana ukifika unakokwenda sharti umeze panado
Ni kama kenya Gari ndogo za probox zinabeba hadi ukome

 
Huko ndio kwao akina Chachu Ombara na founder wetu wa JF Maxence Melo. Hiyo wilaya imemegwa kutoka Karagwe.
Duuh! Una uhakika?

Mtoa mada nashauri we nenda tu, changamoto zipo kila sehemu. Ile ni wilaya iliyomegwa kutoka Karagwe hivyo bado inajikongoja ukizingatia kabla ya kumegwa makao makuu ya wilaya yalikuwa Kayanga ambayo sasa yamebaki Karagwe. Biashara itakayokulipa ni ya viosk,vilabu vya pombe miksa za kienyeji sana na bodaboda. Sahau kilimo kabisa cha mazao ya chakula maana familia nyingi zinalima. Jikite kwenye zao la kahawa japokuwa vyama vya ushirika vinatunyonya mno.

Hali ya hewa saafi kabisa kuna baridi. Wakati mwingine asubuhi au jioni kunakuwa na ukungu ambao aliye mita 10 huwezi muona.

Ishi na wenyeji vizuri utafurahia, kuna wanyambo,wahaya,wanyarwanda,wanyankole,wahima etc ni wewe tu.

Karibu sana

leo asubuhi karagwe1.jpg
 
Back
Top Bottom