Maisha hayafanani kamwe!

Maisha hayafanani kamwe!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,355
Reaction score
80,008
MAISHA HAYAFANANI KAMWE!

Anaandika, Robert Heriel

Wakati watu wengi wanalazimisha maisha yao yafanane na watu fulani, dunia/nature inaharibu mipango yao na kuwatofautisha na wengine. Kadiri unavyotaka kufanana na mtu mwingine ndivyo unavyozidi kutofautiana naye.

Kadiri unavyotaka kujitofautisha na wengine ndivyo unavyokaribia kusudi la maisha. Kusudi la maisha ni kuishi maisha yako, kwani ndipo utakapoipata furaha ya kweli.

Leo kamwe hauwezi kufanana na jana, na kesho halikadhalika.

Kuna wazazi hupenda kuwasema watoto wao kuwa mbona hawafanani na watoto wengine kimaendeleo, au hawafanani wao kwa wao.

Labda mtoto mkubwa amefanikiwa lakini mdogo hajafanikiwa, basi unakuta mzazi anakuambia mbona hauwi kama kaka au dada yako.

Ndugu zangu hata ufanyeje kwenye hii dunia maisha hayawezi kufanana labda angalau kuelekeana. Hatuwezi fanana mitazamo, fikra, matamanio, falsafa, imani, mianzo, hatma, uzao, bahati, juhudi, nidhamu n.k.

Ndio maana Taikon yeye muda wote anafuraha kwa sababu anaishi maisha yake kadiri anavyopenda. Ninavaa nipendavyo lakini kwa kufuata jinsia, umri na mila na desturi zetu. Nina kula vile nitakavyo, nina fanya matendo ambayo yana nifurahisha mwenyewe pasipo kumuumiza mtu au kujiumiza mwenyewe.

Vijana na mabinti msipende kujipa stress, ati mabinti wanakuwa under pressure wenzao wakiolewa alafu wao wakiachwa solemba. Wanaumia au kuumizwa na jamii kuwa wao labda wanamikosi au kuonekana wahuni, siyo kweli.

Hatuwezi kuoa/kuolewa siku moja au mwaka mmoja. Wapo watakaotangulia na wapo watakaochelewa. Mtu unaweza tangulia kuolewa au kuoa na ukawahi pia kupewa/kutoa talaka ukarudi kwenye hali yako ya awali.

Hatuwezi kupata kazi siku au mwaka mmoja, hatuwezi kupata watoto mwaka mmoja, hatuwezi kujenga nyumba wakati mmoja, hatuwezi kufa wakati mmoja. Maisha kamwe hayawezi kufanana.

Maisha sio siku moja, maisha sio mwaka mmoja, maisha yanaendelea yakibadilika kila siku, lakini katika mabadiliko hayo yanazidi kutofautisha. Siku ukiwa na pesa wale walionazo aidha wamezidi zaidi au wamefilisika.

Siku ukioa wale waliokutangulia aidha wameshatengana na kuchokana au kuwa wajane wewe ndio unaifurahia ndoa yako. Siku ukipata mtoto waliokutangulia wanasomesha au wengine wanaozesha kabisa kama sio kuzika.

Hayo ndio maisha! Kwenye maisha HAKUNA HASARA yoyote, yasikupe pressure.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hii mada yako kwa upande mwingine inaweza kuchukuliwa kama kuwaliwaza walioshindwa, ukiondoa yale ambayo yanakuwa nje ya uwezo wa mtu, mfano kama wapenzi kuachana au mwanaume/mke kuchelewa kuoa/olewa..

Mengine yako ndani ya uwezo wetu, kufanana na mtu kimaendeleo hasa kama utakuwa na elimu hili ni jukumu letu, hapa lazima ufananishwe na wenzako wa level moja.

Hata kama wengine wana ajira, wewe bado unaweza kutafuta rizki yako kwa kutegemea elimu yako na kipato chako ili kujiletea maendeleo yako kwa kutumia mazingira uliyopo.
 
Ninafanya matendo ambayo yananifurahisha mwenyewe pasipo kumuumiza mtu au kujiumiza mwenyewe.
 
Wakati una lalamika mbona age mates, class mates wako wamefanikiwa wewe bado pia jiulize kuna wengine wamekufa wewe bado upo hai
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Hii mada yako kwa upande mwingine inaweza kuchukuliwa kama kuwaliwaza walioshindwa, ukiondoa yale ambayo yanakuwa nje ya uwezo wa mtu...

Ni kweli.
Lakini kama mtu anafanya wajibu wake lakini matokeo huja tofauti unafikiri afanyaje?
 
Back
Top Bottom